NABII MTARAJIWA
JF-Expert Member
- Sep 11, 2024
- 425
- 609
Tatari alishaachana na urais baada ya kupigwa Knokout na Trump. Sasa anaandaa majabidhiano.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha utoto basi. Au kama hujui nyamaza! Tanzania ilijipeleka? Unajua Lobito railway inaanzia wapi hadi wapi na kwanin Tanzania imealikwa? Tumia hii simu kupata taarifa sahihi. 🙏🙏🙏Lengo lilikuwa sio kukutana na Tanzania, Tz kajipendekeza tu Ndio maana kapuuzwa kusikilizwa
Wakiwa Angola, Joe Biden anaonekana akisinzia wakati makamu wetu wa Rais akizungumza.
Babu Biden kachoka. Arudi kwao huko Delaware akapumzike na wajukuu wake.
Hii ni aibu.
View: https://youtu.be/3jqHuRkI6EE?si=Df4KXUIbUnRGzmxb
Video ndefu zaidi hii hapa….
View: https://youtu.be/Ikyt0nNX5lI?si=fj6waQjv-t4m6aC3
Wakiwa Angola, Joe Biden anaonekana akisinzia wakati makamu wetu wa Rais akizungumza.
Babu Biden kachoka. Arudi kwao huko Delaware akapumzike na wajukuu wake.
Hii ni aibu.
View: https://youtu.be/3jqHuRkI6EE?si=Df4KXUIbUnRGzmxb
Video ndefu zaidi hii hapa….
View: https://youtu.be/Ikyt0nNX5lI?si=fj6waQjv-t4m6aC3
Asiyetakiwa na wewe na mama yako kwa kuleta zigo lisilokuwa na akili nchiniKama hizi ndo sera zenu basi hamtakiwi nchini
MshafeliAsiyetakiwa na wewe na mama yako kwa kuleta zigo lisilokuwa na akili nchini
Unajibu kama bwabwa keshafeli nani sasa jinga kbsMshafeli
Mkuu umeona mbali😂Mkuu, napenda kutofautiana na wewe kidogo kuhusu usinzifu wa Joe Biden.
Nadhani anachofanya huyu Mwamerika ni kulipiza kisasi kwa kile alichofanyiwa katika sekeseke na songombingo za uchaguzi wa urais Marekani.
Iko hivi: Japo Kamala na JB wanatokea chama kimoja cha Democrats, JB hakufurahia kufurushwa kwake urais halafu akapewa Kamala Harris.
Ndiyo maana JB alikuwa na furaha sana baada ya Kamala kupigwa chini na Trump, na hata hotuba yake ya kwanza kwa umma baada ya anguko hilo ilikuwa kemkemu kiasi kwamba hakuwa akijing'atang'ata na kugugumia kama tulivyomzoea.
Inadaiwa pia kwamba aliwaambia watu wake wa karibu kwamba kama angeingia kwenye sanduku la kura angemshinda Trump kirahisi - katika namna fulani za kukebehi kushindwa kwa Harris.
Na wengine wametia chumvi kwamba huenda JB hata hakumpigia kura Kamala; kwamba alimpigia Trump.
Sasa huu usinzifu wa kisasi unakujaje? Uhusiano wa karibu wa uswahiba kati ya Kamala na Dkt. Sa100 uko wazi kama mchana.
Si ajabu safari za rais zilikuwa nyingi nyingi kwenda Marekani sijui Q-ba, wakati wa uchaguzi wa Marekani, mpaka wengine wakasema anaenda kumfundisha Kamala jinsi ya kumshinda Trump kwa bao la mkono.
Kwa hiyo Kamala Harris na Sa100 ni chanda na pete, halafu Biden na Kamala haziivi. Halafu adui wa rafiki yangu (au rafiki wa adui yangu) ni adui yangu, siyo? Umeona? Patamu hapo!
Unakuja sasa mkutano muhimu kama huu. Biden, hasimu wake Kamala, ambaye Kamala ni swahiba wa Sa100 anategemea Sa100 awe moja ya wageni muhimu waalikwa mkutanoni.
Dkt. Samia, kwa sababu ya huba yake kwa Harris, anaamua kuususia kiaina mkutano wa JB.
Anamtuma makamu wake kwenda kumwakilisha. Kimsingi huku ni kususiwa, kwa sababu kwa cheo cha JB, mgeni mwalikwa alipaswa kuwa Sa100 na wala si Dkt. Mpango.
Sasa JB kuona hivyo kwamba amesusiwa, anaamua kupiga kaunta-attack ya Kiukreni! Naye anamsusia Dkt. Mpango (makamu wa Sa100, Sa100 swahiba wa Kamala, ambaye ni hasimu kwa sasa wa JB!)
JB anaamua kujisinzilisha bhana! Anajipigisha mbonji ya kutuma ujumbe kwa Sa100 na Kamala kinamna akiwaambia kimyo moyo, Gotcha!
Ni yeye alyeanzisha miradi ya kimkakati. SGR, Bwawa la umeme, maji,kupunguza rushwa, elimu bure,kujenga international airport, port mbalimbali,mfumo.mpya wa malipo serikalini, passport mpya,Nilitegemea nawe kumpenda, kama maudhui ya majadilano haya yalipo tukutanishia. Lakini naona taratibu unajiweka pembeni, umebaki tu kuwa mtu wa kupenyeza viswali hapa na pale, huku mjadala ukibadilika!
Negativity can be a way to blame your discomfort on someone or something else, it may make you feel better at first. But at the end it's the sign of stress.Lengo lilikuwa sio kukutana na Tanzania, Tz kajipendekeza tu Ndio maana kapuuzwa kusikilizwa
Inawezekana pia hotuba ya Makamu wetu wa Raisi ilikuwa inaboa. Labda alianza kuingiza uchawa akajisahau Biden sio kama Raisi wa Tanzania anaefurahia kusikia uchawaWakiwa Angola, Joe Biden anaonekana akisinzia wakati makamu wetu wa Rais akizungumza.
Babu Biden kachoka. Arudi kwao huko Delaware akapumzike na wajukuu wake.
Hii ni aibu.
Mkuu 'Lookmasin', basi nikadhani tumekwisha agana huko juu, kumbe bado kuna viporo huku chini vinahitaji kumaliziwa!Ni yeye alyeanzisha miradi ya kimkakati. SGR, Bwawa la umeme, maji,kupunguza rushwa, elimu bure,kujenga international airport, port mbalimbali,mfumo.mpya wa malipo serikalini, passport mpya,
Barabara, NIDA, hospitali, shule, vyuo, kujenga vivuko,vituo kama magufuri stand. Ni ubishi na chuku binafsi zinaweza kushindwa kuelewa mchango wake jambo alikuwa na mapungufu mengine hasa kuhusu demokrasia. Hakuamini kivile kwa hii aina ya demekrasia.
Nikiangalia SSH, Mbowe, Zitto sioni tofauti.
Naona Warioba ndiyo muwakilishi wa ukweli.
Wewe tukupe uongozi leo utakuwa na kasoro zako, blind spots zako labda utaangalia waliokuunga mkono ukawapa vipaumbele.Mkuu 'Lookmasin', basi nikadhani tumekwisha agana huko juu, kumbe bado kuna viporo huku chini vinahitaji kumaliziwa!
hayo uliyo eleza hapo juu kumhusu Magufuli, sina lolote ninalo weza kunyoosha uso wangu na kuyakataa hayo mema yaliyo lenga nchi yetu. Ukinisoma humu kumhusu Magufuli tokea mwanzo wake utatambua kuwa sijawahi hata siku moja kumnyima haki yake kuhusu hayo; isipo kuwa labda katika njia za utekelezaji wa baadhi ya mambo hayo. Uwanja wa kimataifa Chato lilikuwa ni kosa moja lililo onyesha udhaifu wake katika uongozi. Hilo sikukubaliana nalo hata mara moja, na jinsi alivyo shughulikia kwa upendeleo maalum kwa eneo lake. Huo ulikuwa ni udhaifu wa uongozi.
Lakini tukitazama upande wa pili wa Magufuli; upande ambao kwangu na wengi wengine ulimwondolea sifa stahiki kwa hayo mazuri yake, ni tabia zake kama binaadam, ambazo zilikuwa hazilingani kabisa na heshima ya uongozi wa nchi.
Alipenda sana kusifiwa, nadhani hata hii dhana ya "uchawa" kwa mama imeanzia huko kwa Magufuli.
Sijui kama kweli alikuwa na dhamira ya kweli juu ya "wanyonge" alio kuwa akiwaimba mara kwa mara kila alipoona anastahiri sifa. nahoji hili, kwa sababu halikuendana sana na matendo yake ya kutaka kuwainua wanyonge hao. Nilichoona ni kama alikuwa akitafuta wanyonge wawe upande wake zaidi kwa nadharia tu, sikuona vitendo thabiti toka kwake.
Tabia za kiongozi kukiuka au kutofata taratibu na sheria zilizopo; hili lilionekana wazi zaidi toka kwake, na Samia sasa hivi anatembelea humo humo, hastuki. Chukulia mfano wa chaguzi za 2019/2020 zilivyo kuwa; na sasa 2024 tayari tumejionea wenyewe, na tunasubiri tu kumaliza kwa kishindo hapo 2025. Huu ni mfano mmoja tu wa ukiukwaji wa taratibu na sheria ulio kuwa ni sehemu ya ungozi wa Magufuli; uongozi usio kuwa na heshima hata kidogo.
Mambo ya uonevu kwa watu wengine ambao walionekana kuwa na maoni yanayo pingana na ya kwake. Angalau ange jitahidi kuonyesha njia mbadala za kuwa zuia, kama kuwapeleka mahakamani, hata kwa uigizaji, kidogo ingempunguzia mwonekano mbaya alio uonyesha kama kiongozi.
Kama ulivyo sema, yapo mengi ya kumpendea Magufuli, kama hayo uliyo orodhesha hapo juu, na hata pengine kwa baadhi ya mabaya yake kama nilivyo jaribu kuyaeleza hapo juu.
Ndiyo maana sasa, hata mimi ukiniuliza sasa hivi ni kiongozi gani Tanzania inamhitaji kutokana na wananchi wa nchi hii walivyo sasa; nitakwambia bila kuficha kwamba tunamhitaji MAGULI mwingine asiye kuwa na baadhi ya mabovu zaidi aliyo kuwa nayo Magufuli...., kama uonevu, na ukiukwaji wa sheria.
Tukimpata kiongozi wa aina hiyo, hata hizi nyimbo za Demokrasia mimi hazinisumbui sana. Kiongozi awe ni mtu anaye ipenda Tanzania na wananchi wake wote kwa moyo thabiti. Huyo ndiye tunge bahatika kumpata; nchi yetu ingetulia kabisa..
Nadhani kwa kumpenda zaidi Magufuli, inawezekana ukawa unakosa uwazi wa akili unao takiwa kuwa nao. Mimi sijasema kuwa Magufuli hakuwa na mazuri. Nisome vizuri unielewe; labda lugha niliyo tumia kidogo inafanya nisieleweke kirahisi.Lakini kwa ujumla ukiwa fair unaweza kusema kweli Magufuli hakusaidia Watanzania, hakuwa Mzalendo?