LOooooh!
Sasa mimi 'Kalamu', nami nimekuwa na "genge"?
Magufuli alikuwa 'strongman' asiye kuwa na busara ndani yake. Na ni kweli kuhusu hayo ya ukabila na kuendekeza makundi, tabia mbaya kabisa aliyo kuwa nayo.
Hapana. Sizungumzii "strongman" aina ya Magufuli, ingawaje yapo mambo ambayo 'instinctively' alikuwa akiyafanya kuonekana kuwa ya maslahi ya nchi; wakati huo huo aki-'sabotage' hata uzuri huo; kwa mfano kujenga uwanja wandege kwao na kupeleka raslimali nyingi huko isivyo kuwa na taratibu.
Lakini pamoja na haya yote, inashangaza sana kwamba alikoga roho nyingi za waTanzania. Na sababu yake ni hizo kelele alizo kuwa akifanya kuhusu "wanyonge".
Anahitajika kiongozi mwenye uelewa mzuri wa haya ya 'wanyonge' lakini pia asiwe mtu wa kuburuza tu watu katika maamuzi yake.
Sasa mkuu 'lookmasin'; kama kweli unataka kuniweka kwenye 'genge', basi nitafutie genge lisilo yumbishwa na chochote kuhusu maslahi ya Tanzania. Hilo genge nitalifurahia sana.. Vinginevyo, unanivunjia tu heshima.