Mzee wa kupambania
JF-Expert Member
- Aug 14, 2022
- 21,111
- 53,092
AlialikwaHuyo mwenye ushungi nani kampeleka huko
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
AlialikwaHuyo mwenye ushungi nani kampeleka huko
hana point km matundu ya choo anaomba usaid.
Kuna mambo ndani ya nchi hii, na baadhi ya watu wanao yasukuma kuwa mambo ya hovyo sana. Bado kuna waTanzania wanao amini anako tokea mtu (kabila, kanda, dini) ni muhimu zaidi na kumpa sifa ya juu kuliko wengine.Nikukumbushe tu mkuu Kalamu, 2020 Kimei alivyoamua kugombea ubunge Vunjo, tulisoma maandiko mengi humu kuwa Mpango ajiandae kukabidhi wizara ya Fedha kwa Kimei.
Hayakuwa mawazo mabaya, lakini binafsi yalinishtua yalipotoka kwa wafuasi wa ccm na chadema. Inawezekana, hata leo, Mpango anaonekana si competent kwa kuwa tu hatokei kule tulikotaka atoke.
Mpango ni mpango wa Mungu. 2015 hakuwa na ndoto hata ya kugombea udiwani, leo ni makamu wa rais.
Sasa umejuaje kuhusu mimi mkuu 'Lookmasin'. Wewe unajuaje kuwa ninakogwa sana na hayo mawimbi ya sauti kuliko kilichomo kwenye hayo mawimbi?Yes, on speaking. Nyerere, Mkapa, Obama will not have such issue. Msikilize Rais wa Zambia hapo anavyotema madini. Sauti ya mamlaka, kauli thabiti anavyoongea kwa kujiamini. Akianza kuongea hata wewe huwezi kulala. Hakuna kujiumauma.
Sasa mtu anaomba matundu ya choo utaacha kusinzia kweli!Hahahaaa hapana bana. Biden kachoka.
Analazimisha tu hiyo kazi ya urais.
Tofauti ya masaa kati ya Marekani na Angola ni kubwa vya kutosha.
Wakiwa Angola, Joe Biden anaonekana akisinzia wakati makamu wetu wa Rais akizungumza.
Babu Biden kachoka. Arudi kwao huko Delaware akapumzike na wajukuu wake.
Hii ni aibu.
View: https://youtu.be/3jqHuRkI6EE?si=Df4KXUIbUnRGzmxb
Video ndefu zaidi hii hapa….
View: https://youtu.be/Ikyt0nNX5lI?si=fj6waQjv-t4m6aC3
Ni baba zangu wa kirohoInaonekana unapenda sana ma padri..??
Mkuu, napenda kutofautiana na wewe kidogo kuhusu usinzifu wa Joe Biden.Biden sio anasinzia. Anashangaa aina ya hoja zinatolewa na Tanzania. Yeye amezoea kusikiliza hoja za nchi nyingine zimetayarishwa na marekani yenyewe😆
Una maana angalikuwa ni Samia mwenyewe hangalisinzia? Sababu wala siyo uzee kivile kwani kwa WHO definition uzee ni kuanzia umri wa miaka 80. Biden is just 81 years old, ndiyo tu kauanza uzee na ndiyo maana alipenda kuendelea kuwa rais.Mpango anavyoongea hata wewe utasinzia tu...
Viongozi wote wa kiafrika walikuwa brilliant speakers. Kutoka Marcus Garvey, Kwame Nkurumah, Malcolm X, Luther King Jr, Nyerere, Mandela nk.Mentality ya kitumwa ingekuwa ni kiongozi mwafrika hakuna rangi angeacha kuona.Akifanya mzungu anatafutiwa sababu Inferiority complex ni tatizo kubwa sana.
Kalamu, uwa maoni mazuri sana. Lakini wakati mwingine ukubali unakuwa mbishi.Sasa umejuaje kuhusu mimi mkuu 'Lookmasin'. Wewe unajuaje kuwa ninakogwa sana na hayo mawimbi ya sauti kuliko kilichomo kwenye hayo mawimbi?
Ni hivi. Wewe ulisema hapa kuwa mimi ni mbishi, lakini inaonekana wewe ni mbishi asiye kuwa na aibu. hata unapo ambiwa ukweli hutaki kuuelewa ukweli huo.
Kama una maswala yako mengine na Mpango, hayo ni mambo yenu, hatuyajui, lakini huwezi kusema Philip Mpango ni 'incompetent' kwa vile tu hukupenda sauti yake.
Sioni sababu ya kuendelea kupoteza muda na hili hapa. Tuendelee na m mengine.
mh! na mimi ni nani yako wa kiroho!Ni baba zangu wa kiroho
Ni hivi Watanzania 80% hawaikubali CCM hata watu makini ndani ya CCM kama Warioba wako wengi watalendo..Ila hakuna alternative.Kuna mambo ndani ya nchi hii, na baadhi ya watu wanao yasukuma kuwa mambo ya hovyo sana. Bado kuna waTanzania wanao amini anako tokea mtu (kabila, kanda, dini) ni muhimu zaidi na kumpa sifa ya juu kuliko wengine.
Tabia hii ilikuwa imeanza kufifia kwenye miaka ya 70; 80; lakini sasa haya mambo ndiyo yame pamba moto sana kila sehemu. Viongozi wa kisiasa ndio wanao yapa nguvu badala ya kuyakemea.
Hii inaifanya Tanzania kuwa hovyo zaidi hata pengine kulko Kenya tuliko kuwa tukiona mambo haya yakiwaumiza zaidi.
Sasa hapa ubishi ni upi. Wewe binafsi unaona kuwa na "sauti" fulani ni sifa ya uongozi, mimi sioni hivyo. Tatizo ni nini?Viongozi wote wa kiafrika walikuwa brilliant speakers. Kutoka Marcus Garvey, Kwame Nkurumah, Malcolm X, Luther King Jr, Nyerere, Mandela nk.
Ukiwa kiongozi hujajifunza kuongea na hadhira yako ndio utumwa, wenyewe.
Kalamu, uwa maoni mazuri sana. Lakini wakati mwingine ukubali unakuwa mbishi.
Hakuna tatizo. Ni maoni tofauti.Sasa hapa ubishi ni upi. Wewe binafsi unaona kuwa na "sauti" fulani ni sifa ya uongozi, mimi sioni hivyo. Tatizo ni nini?
Nahofia kuweka namba, kama hiyo ya asili mia 80. Jamii yetu mahali kwingi haijawa na ufahamu wa kutoa maoni wazi bila ya kuvutwa na vitu visivyo kuwa na maana sana maishani mwao. Wewe angalia tu hata humu JF.Ni hivi Watanzania 80% hawaikubali CCM hata watu makini ndani ya CCM kama Warioba wako wengi watalendo..Ila hakuna alternative.
Nahofia kuweka namba, kama hiyo ya asili mia 80. Jamii yetu mahali kwingi haijawa na ufahamu wa kutoa maoni wazi bila ya kuvutwa na vitu visivyo kuwa na maana sana maishani mwao. Wewe angalia tu hata humu JF.
Lakini, ndiyo, ninakubaliana na wewe kuhusu ubovu wa CCM. Laiti kama pange tokea tukapata njia ya watu kuamua kwa haki na uhuru wote bila ya woga wowote, nami naamini kwamba CCM kwa sasa hivi inge kataliwa vibaya sana.
Lakini tatizo pia lina changiwa na kutokuwepo chama makini sana kinacho aminiwa na wananchi. CHADEMA wangeweza, lakini naona wanavurugana ndani kwa ndani, hasa viongozi wao.
lakini ngoja nikupeleke mahali tofauti kidogo na hayo niliyo eleza hapa.
Kwa hali yetu ilivyo, Tanzania kwa sasa hivi inahitaji "a strong man". Kiongozi ambaye hababaiki na anao msimamo hasa kuhusu maslahi ya nchi. Kiongozi huyu asiwe mwonevu kwa yeyote kwa sababu za kibinafsi. Kiongozi anaye heshimu taratibu na sheria. Kiongozi mkweli. Akisema kitu watu hawatilii mashaka juu yake.
Huyu ni kiongozi ambaye akipatikana kwa sasa, Tanzania itatulia; bila kujali hizo
LOooooh!Hi hivi Ata mkipata strong man kama Magufuli mtampigia kelele sababu ya ukabila wenu. Hamtamtambua wewe na genge lenu. Nafikiri mnataka Mbowe achukue nchi.atafanya mageuzi gani kwa akili hizi, zake?
Unafikiri kwanini nchi ilimpenda?LOooooh!
Sasa mimi 'Kalamu', nami nimekuwa na "genge"?
Magufuli alikuwa 'strongman' asiye kuwa na busara ndani yake. Na ni kweli kuhusu hayo ya ukabila na kuendekeza makundi, tabia mbaya kabisa aliyo kuwa nayo.
Hapana. Sizungumzii "strongman" aina ya Magufuli, ingawaje yapo mambo ambayo 'instinctively' alikuwa akiyafanya kuonekana kuwa ya maslahi ya nchi; wakati huo huo aki-'sabotage' hata uzuri huo; kwa mfano kujenga uwanja wandege kwao na kupeleka raslimali nyingi huko isivyo kuwa na taratibu.
Lakini pamoja na haya yote, inashangaza sana kwamba alikoga roho nyingi za waTanzania. Na sababu yake ni hizo kelele alizo kuwa akifanya kuhusu "wanyonge".
Anahitajika kiongozi mwenye uelewgia mzuri wa haya ya 'wanyonge' lakini pia asiwe mtu wa kuburuza tu watu katika maamuzi yake.
Sasa mkuu 'lookmasin'; kama kweli unataka kuniweka kwenye 'genge', basi nitafutie genge lisilo yumbishwa na chochote kuhusu maslahi ya Tanzania. Hilo genge nitalifurahia sana.. Vinginevyo, unanivunjia tu heshima.