TANZIA Joel Misesemo afariki dunia kwa kujirusha kutoka ghorofani jengo la Derm eneo la Makumbusho, Dar

TANZIA Joel Misesemo afariki dunia kwa kujirusha kutoka ghorofani jengo la Derm eneo la Makumbusho, Dar

Mimi toka rafiki yangu Deo aliyekuwa anawaona wanaojinyonga kama vile hawana akili na yeye akaja kula kitanzi tena mwenyewe baada ya kumfukuza mkewe chumbani haya mambo ya kujiuwa nimekuwa nikiyachukulia kwa kiasi sana.

Naamini hawa wanaojiuwa hadi kufikia hatua hiyo huwa wanapitia moment moja mbaya na ngumu sana isiyoelezeka!wanaume kinachotuumiza siyo wasemaji sana wa yanayotukwaza na siwalaumu,personally siuoni uwezekano wa kusema kwa yeyote nikipata changamoto mbaya zihusuzo maisha hasa ya ndoa that's why kila siku namuomba Mungu aendelee kunipa utulivu ktk familia kuliko kitu chochote.
Mimi nasema vizuri tuu na uzuri Huwa natukana vinaisha ila ukijifanya mwamba utakuja kujitia kitanzi Ufe Kwa aibu Kwa kujinyea kisa kujinyonga au kujirusha gorofani kama huyu Jamaa amejiua kama Msoga.
 
Stori ya shuhuda ni ukweli au uzushi?, maelezo yake: ''Inasikitisha kaamua kukatisha uhai wake... majirani walisikia kishindo ndio kutoka kuangalia mtu kajirusha (ina maana hakuna aliyeshuhudia akijirusha, sasa wanasemaje kajirusha?) .....

Ameumia sana hauwezi kumtambua ila wanasema anaonekana ni mwenyeji wa hapa (sasa hapo mwanzo ilikuwaje akasema marehemu huwa anakwenda kuswali kweli hilo jengo halafu hapo hapa akakiri kaharibika hawezi kutambulika?)''


Bongo nyoso sana
 
Linda vyote ila chunga sana usije ukaharibu afya ya akili yako...
20230521_074021.jpg
 
Dah 😢 ninaamini pasi na shaka yoyote kuwa huu ni wakati sahihi kabisa wa kuzungungumza wanaume wenyewe kwa wenyewe kuwa ni sawa kutokuwa sawa, its really ok not to be ok! Tukae chini wenyewe kwa wenyewe men to men TUONGEE YETU YOTE dah 😔 RIP brother Joel 🙏

Posted @withregram • @millardayo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema linachunguza tukio la kifo cha Mtu aitwae Joel Misesemo Chizi anayekadiriwa kuwa miaka kati ya 35 hadi 40, Mkazi wa Mwananyamala ambaye alijirusha kutoka ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho Kijitonyama na kufariki.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Marehemu alionekana katika jengo hilo leo tarehe 23, Mei 2023 majira ya saa kumi na moja alifajiri na alimwambia Mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye Msikiti uliopo ghorofa ya 15 dani ya jengo hilo lakini muda mfupi baadaye alijirusha.

Taarifa ya Polisi imesema camera za jengo hilo zimemuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya saba kupitia dirishani na kufariki ambapo tayari mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.

Jeshi la Polisi limepata gari la Marehemu aina ya Suzuki rangi ya silver lenye namba za usajili T142 DRM lililokuwa limeegeshwa kwenye maegesho ya magari katika eneo hilo na sasa limehifadhiwa Kituo cha Polisi Oysterbay.
Stress na frustration za maisha
 
Ma MC na ambao ni wanasaikolojia wengi hapa mjini ni watu wake wa karibu na wanaofahamiana sana na ukifuatilia ni mtu alikuwa anawapa watu ushauri wa maisha etc...sasa imekuwaje? Wanasaikolojia wote hao waliomzunguka hakuna hata mmoja aliona tatizo na kumsaidia....
 
Hiyo ni chronic depression...ukimuelezea mtu anaweza asiamini kama kweli unaumwa maana kwa nje unaonekana upo kawaida tu ila kichwani kuna machafuko ya hatari.

Ni vyema kujitahidi kuwa karibu na Mungu na pia kujichanganya na watu, unapojifungia ndani peke yako ndio unazidi kuuchochea huu ugonjwa na demons/devils wanachukua hii nafasi ambayo unakuwa vulnerable kuanza kukupa evil suggestions kuwa njia ya kutatua matatizo yako ni KUJIUA ili upumzike. Hayo mawazo hujirudia kwa kasi ya ajabu moaka mtu anaamua kuukatisha uhai wake.

Ukijiona una matatizo yanasumbua akili yako mtafute rafiki yako wa karibu , kaa chini umueleze yanayokusibu ili upunguze mzigo mzito wa mawazo kifuani na akilini mwako.
Tatizo wangapi wanayajua haya uliyoyaandika hapa?

Huyo niliyemtaja hapo juu tulikuwa wote na jamaa zetu wawili saa kumi na mbili jioni tukaagana wote tunacheka na kufurahi tukiahidiana kuonana kesho but saa tatu napigiwa simu amejinyonga,ni wachache sana wanaojishusha mbele ya changamoto maana kila mwanaume anaamini gumu lolote atalishinda hafikirii hicho mnachoita depression demos sijui devils.
 
Back
Top Bottom