TANZIA Joel Misesemo afariki dunia kwa kujirusha kutoka ghorofani jengo la Derm eneo la Makumbusho, Dar

TANZIA Joel Misesemo afariki dunia kwa kujirusha kutoka ghorofani jengo la Derm eneo la Makumbusho, Dar

A
Pale Mwanga Tower, Makumbusho limetokea tukio la mtu asiyefamika kujirusha kutoka gorofani, ambapo inasemekana tukio hilo limetokea mapema leo majira ya saa kumi na moja asubuhi.

Mpaka majira ya saa mbili asubuhi bado mwili wa mtu huyo ulikuwa eneo hilo. Taarifa zaidi zitakujia kadri zitakavyopatikana.

View attachment 2632805
Joel Misesemo enzi za uhai wake​

=====

Kijana asiyefahamika aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35 amefariki baada ya kujirusha kutoka gorofa ya 15 katika jengo la Derm lililopo Makumbusho, Dar es Salaam.


UPDATE: Polisi yathibitisha aliyejiua, kufanya uchunguzi


POLISI: KAMERA ZIMEONESHA JOEL MISESEMO AKIJIRUSHA MAKUSUDI KUTOKA GHOROFA YA 7
Kufuatia tukio la kifo cha Joel Misesemo Chizi mwenye umri kati ya miaka 35 hadi 40, Mkazi wa Mwananyamala, Jeshi la Polisi limesema chanzo cha awali ni mhusika kujirusha kutoka ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho Kijitonyama.

Imeelezwa kuwa Joel alifika eneo hilo akiwa na gari aina ya Suzuki rangi ya silver (T142 DRM) na kuonekana katika jengo hilo Saa 11 Alfajiri ya Mei 23, 2023, akamwambia Mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye Msikiti uliopo ghorofa ya 15 ndani ya jengo hilo, muda mfupi baadaye alijirusha.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema kamera za jengo hilo zimemuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya 7 kupitia dirishani na mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi Zaidi
Atakuwa alikuwa anaruka sarakasi zake
 
Hakufa palepale alikimbizwa hospital. Huenda alifia njiani au hospital
Mbaya zaidi tukio lilikuwa linarushwa live na ITV wakakatisha matangazo. Yule njomba kut0ka Ntwara ilikuwa kazi yake michezo ya kupanda majengo marefu na kujirusha ndani ya tank za maji huku akiongozwa(guided) na kamba asidondokee nje ya tank.
Pale alifeli kukokotoa urefu wa jengo, uzito wake, na kina cha maji ili kutambua atakuwa submerged urefu gani ndani ya maji ili asiguze sakafu ya tank kwa mshindo mkubwa. Aliidharau Gravitional force (g). Alipotumbukia wanashangaa hatoki nje mwenyewe wakawahi kumtoa kavunjika viungo.
Yani yule alikufaa mbele ya familia yakee...baba na mama aiseee
 
Depression nyingine huletwa na mashetani ambao huuvamia mwili wa mwanadamu na kuanza kumshawishi afanye mambo ya ajabu .Kwa ambaye hajapitia haya hawezi kuamini ila mi nishapitia hali hiyo!

Nilikuwa heavily depressed, muda mwingi najifungia ndani, sihitaji kuonana na mtu yeyote na vilevile hayo mawazo ya kujiua yalikuwa yakinijia sana, yaani unasikia kabisa vitu masikioni vikikushawishi ufanye uovu huo!!

Nikaja kuchukuliwa nyumbani kinguvu na wazazi wangu kwenda kutibiwa kwa sheikh kwa kisomo cha Ruqyah!!

Nilipofika tu kwake nikawa situlii, yaan kana mtu mwenye wasiwasi mzito, tumbo linajaa gas, napiga sana miayo n.k. Sheikh akaniangalia akasema ni signs za kuwa nina jini (shetani) baya limeuvaa mwili wangu.

Akanitibu kwa kunisomea Quran...ghafla nikaanza kupoteza uwezo wa kuona nikaanguka chini, akanisomea baadae nikarejea katika hali yangu ya kawaida baada ya lile shetani kunitoka. Na tokea hapo ile hali ya wasiwasi iliyopitiliza na depression ikanitoka.

So usimshangae jamaa huenda kichwani kwake alishavamiwa na mashetani na yalikuwa yakimpelekesha kumshawishi ajitupe ili aende akapumzike kuzimu huko.

Kama mmesoma biblia kuna story ya yesu anaposhawishiwa na shetani kwenda kujiua




MATHAYO 4​

Kujaribiwa kwa Yesu
(Marko 1:12-13; Luka 4:1-13)

1Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.
2Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.

3Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”

4Yesu akamjibu, “Imeandikwa:
‘Mtu haishi kwa mkate tu,
ila kwa kila neno asemalo Mungu.’”

5Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu, 6 akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa:
‘Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako;
watakuchukua mikononi mwao,
usije ukajikwaa kwenye jiwe.’”

7Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia:
‘Usimjaribu Bwana, Mungu wako.’”

8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,

9akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.”

10Hapo, Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Imeandikwa:
‘Utamwabudu Bwana Mungu wako
na kumtumikia yeye peke yake.’”

11Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia."

Nb
hivyo Joel wakati anapanda juu ya ghorofa alikuwa chini ya ushawishi wa ibilisi (shetani). Ulikuwa ni mtihani kwake aweze kuushinda kwa kuyakataa mawazo maovu ya ibilisi but unfortunately alishindwa na kuamua kujitupa chini.

Njia pekee ya kuweza kuyashinda majaribu haya ni kuwa karibu na Mungu tu.
 
Kwasisi waislam ukijiua ina maanisha kuwa umeshajichagulia siti yako ndani ya moto mkali wa jahannam.Ibilisi na majeshi yake wapo kuhakikisha wanazama motoni pamoja na mwanadamu.

Hivyo kwenye maisha wanafanya kila wawezalo kumshawishi mwanadamu afe katika hali itakayo hakikisha anakwenda motoni. Ndio maana hata kwenye biblia utaona jinsi Ibilisi alivyomchukua yesu na kumpeleka juu ya mnara na kisha kumshawishi ajirushe chini ili ajiue (huku akimpa ahadi ya uongo kuwa malaika watamdaka kabla hajafika chini)...Yesu mwana wa Mariam alishtukia lengo la ibilis na kisha akamjibu imeandikwa usimjaribu Mungu wako.

Kuona hiyo haiyoshi akampeleka juu ya mlima mrefu na kisha kumpa ahadi ya uongo kuwa akimuabudu yeye iblis (akimshirikisha Mungu) basi atampa ufalme wote wa dunia.
Yesu akashtuka tena janja ya ibilis na akamwambia kuwa ameamrishwa amuabudu na kumtumikia MUNGU peke yake pasi na kumshirikisha na yeyote au kitu chochote kile.

Ushirikina ni tiketi nyingine ya mwanadamu kujichagulia siti ndani ya moto wa jahannam. Hivyo Ibilis alijikita katika sehemu mbili , Kujiua na Kunshirikisha Mwenyezi Mungu ili tu lengo lake la kujumuika pamoja na mwanadamu motoni litimie.
 
Back
Top Bottom