Jogging pembeni ya barabara zinagharimu UHAI

Jogging pembeni ya barabara zinagharimu UHAI

Asaante kwa Uzi Juma1967 naomba kuchangia uzi kwa sababu mimi ni mdau mkubwa wa mazoezi hasa ya Jogging; Katika kufanya mazoezi hasa ya kufanya jogging ni vema sana kuchukua tahadhari kama ifuatavyo;

1. Kimbia upande wako wa kulia ili kuona kwa urahisi kinachokuja mbele yako.
2. vaa mavazi ya rangi inayoonekana kirahisi kama rangi ya Neon Green
3. Vaa reflectors Mikanda au Arms/Shoe Dim lights ambazo zitawaonesha watumiaji wengine wa barabara uwepo wako. hizi kwa Dar zinapatikana Swahili sweatshop pale Dar Free market, lkn unaeza agizia online kutoka nchi nyingie sio gharama sana.
4. Ikifaa usikimbie peke yako muda huo ili hata ikitokea dharura basi urahisi wa kusaidika uwepo.
5. Pendelea kukimbia route isiyo na magari mengi au route yenye barabara pana ingawa kwa baadhi ya sehemu hizi ni changamoto!!

pole sana kwa kuwapoteza friends, lkn kama wewe ni Mkimbiaji kuna Group la FAMILIA YA WAKIMBIAJI TANZANIA (FWT) ambayo inajumuisha wakimbiaji wengi Tanzania ambao tunasaidia katika Changamoto mbalimbali na tupo mbio kuanzisha FWT Foundation ambayo itasaidia kusomesha watoto wa wakimbiaji wenzetu wanapopatwa na Changamoto mbalimbali ikiwemo Kifo.

Kwa sasa hakuna Kiingilio chochote ukihitaji unaweza kuniona PM ukaja na Namba yako nikuunge kwenye Group la WhatsApp utakutana na taarifa zingine huko.

Pole sana Mkimbiaji kwa kupoteza Rafiki.
Nakuja
 
Tutazika Hadi lini? Barabara mpya ya Makongo magari yanakimbia balaa (hususani gari zisizo na namba za usajili, hata ikikugonga ni ngumu kubaini usajili wake). Madalali wa magari mlimani city hizi gari zisizo na namba mnazikimbiza ili iweje?
 
Mimi siamini kama wote wanaokimbia Barabarani wana show off, pia siamini mtu kwenda barabarani kulimbia 10 min.
Mtu mwenye lengo la dhati la kufanya mazoezi hawezi kufanya hayo unayoyasema.

Kuhusu kukimbia uwanjani pia sikatai lkn kukimbia ni maisha ya kila siku kwa kina sie, je kila siku tutakimbia uwanjani? Jibu ni hapana kwa sababu kukimbia katika mazingira ya aina moja yanachosha. Kuna watu wanakimbia 3hrs- 12hrs, how can u manage kukimbia masaa hayo kwenye eneo moja!

Explore kbl ya kuongea bro!!
Umeongea point sana bro
 
Kukimbia barabarani ni kweli c salama ila pia kukimbia kila siku uwanjani kwenye mazingira yale yale kunachosha
 
Wengi ni Show off,unakuta barabara ni ndogo ila mkimbiaji anajikuta na yy ni gari
 
Pia mnaofanya mazoezi barabarani vaeni nguo zenye rangi ya mg'ao kama reflector !! Mtu anakimbia kama full nyeusi juu chini !!
Mbali na hapo kukimbia barabarani bado sio salama
Wengine wanaweka na muziki kabisa
 
Pia mnaofanya mazoezi barabarani vaeni nguo zenye rangi ya mg'ao kama reflector !! Mtu anakimbia kama full nyeusi juu chini !!
Mbali na hapo kukimbia barabarani bado sio salama
Wengine wanaweka na muziki kabisa
Mi huwa nawahi sana kumi na moja alfajir muda huo magari sio mengi ila kukimbia uwanjani kila siku kunachosha
 
Wengi ni Show off,unakuta barabara ni ndogo ila mkimbiaji anajikuta na yy ni gari
Kaka sio wote ni show off wengine kukimbia uwanjani kunatuchosha kila siku ndio maana tunaamua kubadilisha mazingira japokuwa barabarani sio salama ila kuna raha yake asikwambie mtu
 
Back
Top Bottom