Hakuna watu wanao furahia (enjoy) kutumia hesabu walizo soma secondary level education hadi university level kama wanaofanya kazi zao za kila siku kwenye kazi za uhandisi na software development, computer programming.
Uhandisi karibu fani zote mfano mekanika, ujenzi, metal fabrication, computer engineering, electrical machine manufacturing, e.t.c.
Nilipokuwa busy na software development nilijikuta nikitumia sana mbinu au kanuni (formulas) za math.
Nilipokuwa na project binafsi za ujenzi niliona au nilishauri mafundi matumizi ya kanuni za hesabu hasa applied math. Mfano niliwapa vipimo vya kujenga kisima au tank za maji. Nilitumia kanuni ya kutafuta volume of a cylinder kujenga kisima cha Lita 30,000 shambani.
Nilitumia sana hesabu za modulo operation ( finding remainders) kwenye kutengeneza system flani za computer au hesabu za encryption ya kuficha data flani n.k.
Shukrani waalimu wangu wa jalalani (UDSM) na elimu ya sekondari.