Johannes Rebmann: Mtu aliyegundua mlima Kilimanjaro

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
Ni maajabu sana. Kulingana na machapisho mbalimbali mlima maarufu unaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 3 million iliyopita hakuna mkazi yeyote wa aliwahi kujua kuna mlima mrefu kaskazini mwa Tanganyika hata wale wakazi wenyewe hawakujua 😁.

Johannes Rebmann.

Mlima Kilimanjaro uligunduliwa na bwana Johannes rebmann ambaye alikuwa mmissionary kutoka Ujerumani mnamo 1848.

Kutokana na bwana huyo aliyekuwa na mwenzake aitwaye Johann Lidwig Krapf, habari ziliweza kusambaa maeneo mengi ya ulaya kuwa kuna mlima wenye kilele cha barafu karibu sana na ikweta. Lakini habari hizo hazikuaminika kwa watu mpaka miaka kadhaa baadae.
 
Hako kabeberu kalifika hapo Moshi kakakuta Mangi amekamata vijana ambao walikuwa wanapanda mlima kilimanjaro na kufanya shughuli zao kinyume na sheria akauliza hawa vipi akaambiwa kosa lake na yeye akataka kupanda mlima basi Mangi(sikumbuki Mangi gani) akatupia jicho akamchagua kijana mmoja amsindikize Beberu kupanda mlima..kinachotucost Waafrica ni ile ishu ya documentation tunajazana ujinga eti chuo cha kwanza duniani kilikuwa Timbuktu University mara sijui Al Azar University mbona hatukusoma sasa? Ni ule uvivu wetu wa asili maana hata Mansa Mussa alifika Marekani kabla ya hata Columbus na Columbus alipofika America wenyeji walimwambia hilo ila yeye akawa mjanja kudocument
 
Mabeberu kutoka Wikipedia wanasema hivi.
Johannes Rebmann (January 16, 1820 – October 4, 1876) was a German missionary, linguist, and explorer credited with feats including being the first European, along with his colleague Johann Ludwig Krapf, to enter Africa from the Indian Ocean coast

. In addition, he was the first European to find Kilimanjaro.[1] News of Rebmann's discovery was published in the Church Missionary Intelligencer in May 1849

Hii mada yako reference yako sijui wapi inayodai kuwa yeye ndie aliegundua mlima Kilimanjaro.
 
Watu weupe wana propaganda flani za kiajabu ni kweli yaweza kuwa whiteman wakwanza kufika eneo fulani ila watabadili stori. Hivyo hivyo walifanya kwa ziwa Victoria na zaidi.
 
Siyo propaganda,huwa wanajiona wao ni watu na wewe ni mnyama anaefanana na wao
 
Mgunduzi kiaje yan? Inamaana kulikiwa hakuna watu maeneo hayo au ya karibu yake? Ama ndio uongo ili tuone wanajua kila kitu?
Mi nahis ilitakiwa iwe ni mzungu wa kwanza kufika Kilimanjaro na sio mgunduzi hii ni sawa na wanavyosema Christopher Columbus ndio mgunduzi wa bara la america wakati mda anafika huko alikuta kuna watu wanaishipo tayar
 
Ni maajabu sana. Kulingana na machapisho mbalimbali mlima maarufu unaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 3 million iliyopita hakuna mkazi yeyote wa aliwahi kujua kuna mlima mrefu kaskazini mwa Tanganyika hata wale wakazi wenyewe hawakujua 😁.

Johannes Rebmann.

Mlima Kilimanjaro uligunduliwa na bwana Johannes rebmann ambaye alikuwa mmissionary kutoka Ujerumani mnamo 1848.

Kutokana na bwana huyo aliyekuwa na mwenzake aitwaye Johann Lidwig Krapf, habari ziliweza kusambaa maeneo mengi ya ulaya kuwa kuna mlima wenye kilele cha barafu karibu sana na ikweta. Lakini habari hizo hazikuaminika kwa watu mpaka miaka kadhaa baadae.
kuna vitu hutakiwi hata kuvisoma au kutaka kujua maana vinachafua moyo sana
 
Back
Top Bottom