SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Hoja fukunyuku.
Sitegemei Simba kusajili kipa mwingine msimu huu. Nadhani wanafuatilia kwa ukaribu uponyaji wa Aishi Manula na naona kuna juhudi zinafanyika za kuboresha viwango vya Ally Salum na mwenzake Ferooz. Kwa sababu dirisha la usajili halijafungwa, maamuzi ya mwisho bado hayajafanyika.
Kuleta kipa kutoka nje halafu umlipe milioni 15 za kukaa benchi, huo utakuwa ni ufujaji wa fedha. Nafasi ya golikipa siyo ya kufanya rotation kwa hiyo tusitegemee Manula kuja kushea namba na mtu ila timu bado inahitaji uwe na kipa wa ziada wa gharama nafuu ambaye unaweza kumtegemea kwa asilimia fulani.
Safu ya mbele pale Simba sasa hivi haimpi nafasi tena John Bocco kucheza. Mimi nadhani kama tuko tayari, wamfanyie mazoezi ya ukipa awe msaidizi wa Salum/Ferooz hadi hapo Manula atakaporudi.
Bocco ana kimo na mwili mzuri kwa nafasi ya kipa. Akiwa tayari kuurusha na kuutupa mwili wake mara kwa mara kama majukumu ya kipa yanavyotaka, na kuongezewa uwezo wa kudaka, hili wazo linaweza kujaribiwa. Na huwa naamini ukiwa mshambuliaji, ni rahisi kucheza beki/kipa na kinyume chake pia maana unakuwa unajua uchezaji na ufikiriaji wa mtu wa nafasi hiyo.
Pia kwa haraka haraka naona kama Ferooz anaweza kuwa bora zaidi ya Salum ingawa sijawahi kumuangalia katika mechi. Akiongeza utayari, apewe nafasi.
ZIADA: Mwezi wa 2 niliwahi kutoa wazo la Israel Mwenda kuchezeshwa kama beki wa kushoto nikaonekana hamnazo lakini mwishoni mwa ligi alijaribiwa hiyo nafasi na hivi sasa Simba wanaamini wanaweza kweli kumtumia kwenye nafasi hiyo.