John Bocco aandaliwe kama golikipa wa akiba

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Hoja fukunyuku.

Sitegemei Simba kusajili kipa mwingine msimu huu. Nadhani wanafuatilia kwa ukaribu uponyaji wa Aishi Manula na naona kuna juhudi zinafanyika za kuboresha viwango vya Ally Salum na mwenzake Ferooz. Kwa sababu dirisha la usajili halijafungwa, maamuzi ya mwisho bado hayajafanyika.

Kuleta kipa kutoka nje halafu umlipe milioni 15 za kukaa benchi, huo utakuwa ni ufujaji wa fedha. Nafasi ya golikipa siyo ya kufanya rotation kwa hiyo tusitegemee Manula kuja kushea namba na mtu ila timu bado inahitaji uwe na kipa wa ziada wa gharama nafuu ambaye unaweza kumtegemea kwa asilimia fulani.

Safu ya mbele pale Simba sasa hivi haimpi nafasi tena John Bocco kucheza. Mimi nadhani kama tuko tayari, wamfanyie mazoezi ya ukipa awe msaidizi wa Salum/Ferooz hadi hapo Manula atakaporudi.

Bocco ana kimo na mwili mzuri kwa nafasi ya kipa. Akiwa tayari kuurusha na kuutupa mwili wake mara kwa mara kama majukumu ya kipa yanavyotaka, na kuongezewa uwezo wa kudaka, hili wazo linaweza kujaribiwa. Na huwa naamini ukiwa mshambuliaji, ni rahisi kucheza beki/kipa na kinyume chake pia maana unakuwa unajua uchezaji na ufikiriaji wa mtu wa nafasi hiyo.

Pia kwa haraka haraka naona kama Ferooz anaweza kuwa bora zaidi ya Salum ingawa sijawahi kumuangalia katika mechi. Akiongeza utayari, apewe nafasi.

ZIADA: Mwezi wa 2 niliwahi kutoa wazo la Israel Mwenda kuchezeshwa kama beki wa kushoto nikaonekana hamnazo lakini mwishoni mwa ligi alijaribiwa hiyo nafasi na hivi sasa Simba wanaamini wanaweza kweli kumtumia kwenye nafasi hiyo.
 
Teh teh teh anaweza kuinama kwa haraka kweli?
Sina uhakika, sijajua. Kama alishawahi kucheza nafasi hiyo hata kwa mechi chache hiyo ni faida, mengine ni kumfanyia majaribio maeneo kadhaa akionekana kuyamudu basi hiyo nafasi anaiweza akiwa kipa wa akiba. Mazoezi tu sahihi na utayari.

Wengine tumecheza nafasi zote kulingana na uhitaji wa timu wakati huo na nafasi zote tulikuwa tunazimudu.
 
Kweli hoja YAKO fukunyuku hata KUKUJIBU inakuwa changamoto.

1.Simba walikuwa na MPANGO WA kuongeza Golikipa kutoka Brazil.
Baada ya kumchunguza vizuri wameona mapungufu mengi.

2. Wameamua kujikita Cameroon na ivorycost kusaka Golikipa.

Mashindano ya CUF na super cup si MCHEZO.

Boko anaandaliaa UKOCHA.
Nyoni alikataa umanager.
 
Kumbeee
 
Mashindano ya CUF ya Lipumba?
 
Hoja fukunyuku.

Sitegemei Simba kusajili kipa mwingine msimu huu. Nadhani wanafuatilia kwa ukaribu uponyaji wa Aishi Manula na naona kuna juhudi zinafanyika za kuboresha viwango vya Ally Salum na mwenzake Ferooz. Kwa sababu dirisha la usajili halijafungwa, maamuzi ya mwisho bado hayajafanyika.

Kuleta kipa kutoka nje halafu umlipe milioni 15 za kukaa benchi, huo utakuwa ni ufujaji wa fedha. Nafasi ya golikipa siyo ya kufanya rotation kwa hiyo tusitegemee Manula kuja kushea namba na mtu ila timu bado inahitaji uwe na kipa wa ziada wa gharama nafuu ambaye unaweza kumtegemea kwa asilimia fulani.

Safu ya mbele pale Simba sasa hivi haimpi nafasi tena John Bocco kucheza. Mimi nadhani kama tuko tayari, wamfanyie mazoezi ya ukipa awe msaidizi wa Salum/Ferooz hadi hapo Manula atakaporudi.

Bocco ana kimo na mwili mzuri kwa nafasi ya kipa. Akiwa tayari kuurusha na kuutupa mwili wake mara kwa mara kama majukumu ya kipa yanavyotaka, na kuongezewa uwezo wa kudaka, hili wazo linaweza kujaribiwa. Na huwa naamini ukiwa mshambuliaji, ni rahisi kucheza beki/kipa na kinyume chake pia maana unakuwa unajua uchezaji na ufikiriaji wa mtu wa nafasi hiyo.

Pia kwa haraka haraka naona kama Ferooz anaweza kuwa bora zaidi ya Salum ingawa sijawahi kumuangalia katika mechi. Akiongeza utayari, apewe nafasi.

ZIADA: Mwezi wa 2 niliwahi kutoa wazo la Israel Mwenda kuchezeshwa kama beki wa kushoto nikaonekana hamnazo lakini mwishoni mwa ligi alijaribiwa hiyo nafasi na hivi sasa Simba wanaamini wanaweza kweli kumtumia kwenye nafasi hiyo.
Labda kama una furahisha genge
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Kweli hoja YAKO fukunyuku hata KUKUJIBU inakuwa changamoto.

1.Simba walikuwa na MPANGO WA kuongeza Golikipa kutoka Brazil.
Baada ya kumchunguza vizuri wameona mapungufu mengi.

2. Wameamua kujikita Cameroon na ivorycost kusaka Golikipa.

Mashindano ya CUF na super cup si MCHEZO.

Boko anaandaliaa UKOCHA.
Nyoni alikataa umanager.
Nimetoa angalizo, aangaliwe utayari. Hiyo mada ya Bocco kuandaliwa kuwa kocha nimekuwa nataka sana kuileta humu ila nasahau.
 
Na kwenye derby tunamuweka Bocco pale golini na bado tunawakanda
Unawaza Derby tu , yaani mchezaji amefikisha miaka 30+ uanze kumfundisha kua goals keeper hivi unaijua nasafi ya goal keeping vizuri?
 
Soma vizuri hapo juu, nimegusia maswali yako yote
 
Ungekua kocha timu yako ingeshuka daraja round ya kwanza ya ligi
Nilivyosema Mwenda achezeshwe beki ya kushoto nafasi ya Zimbwe hakuna aliyeniunga mkono ila leo tunaongea habari nyingine.

Yanga waliwahi kuwa na mtu anaitwa Kenneth Mkapa, alikuwa beki wa kushoto, baadaye sana katika career yake akabadilishiwa nafasi kuwa mshambuliaji tena wa kati na ndiyo nafasi aliyobaki nayo hadi anastaafu.
 
Nafasi za ndani unaweza kufanya risk kumbuka kipa akifanya kosa ni goal, beki wa kushoto kucheza kulia ni kawaida wala sio jipya Ila mchezaji mwenye umri wa miaka 30+ umpange golini timu yenyewe Simba! unatafta kuuwawa na mashabiki, angekua below 23 sawa
 
Natambua hilo ila sijui historia yake. Vipi kama aliwahi kuwa kipa huko nyuma na nimesema kipa wa akiba. Ukiniuliza mimi alitakiwa kuachwa ila kama anaendelea kuwepo kikosini sijui anajifunza ukocha, basi avae gloves awe kipa wa 4 huku anaendelea na mafunzo yake.
 
Back
Top Bottom