John Heche anaunga mkono Mbowe kupisha nafasi ya uenyekiti wa Chadema taifa kwa heshima

Mimi naamini Mbowe na Lissu wanawachezesha ngoma wapinzani wao tu !

Mtu mwenye Kutafakari majambo kwa kina atajua tu kwamba Mbowe na Lissu sio watu wa kugombana au wa kuweza kugombanishwa na yeyote yule 😳🙄🤩
Ngoja Tusubiri tuone 🙏
Hili watu wengi wenye akili mhemuko hawawezi kuliona.

Mbowe na Lissu ni kitu kimoja,wamekubaliana kila kitu.
 
John Heche kwenye ukurasa wake wa Twitter ame- repost ujumbe wa David Mfugwa wa Chadema ambao unamtaka Mbowe kustaafu kwa heshima na kulinda heshima yake ndani ya Chadema. Hii ina maana kuwa hata Heche hakubaliani na kauli ya #Mi5tena.

Msimamo wetu hautaturudisha nyuma. Ni ama Mwamba avuke na hao machawa wanaoitakia mabaya Chadema au Chadema ivuke kwa kishindo huku Mwamba akishuhudia matunda yake ya kujenga wengine kisiasa. Hii chansi ni ya muhimu sana isichezewe.
View attachment 3180129
Safi sana, Heche anamkubali Lissu imagine mwenyekiti Lissu na Katibu Heche ndio tutaona upinzani halisi.
 
Kwa mara ya kwanza kabisa ninashuhudia makamanda wakigawanyika humu jukwaani katika makundi mawili! Kundi moja linaunga mkono Kamanda Mbowe awe Mwenyekiti wa maisha, na kundi lingine linataka apishe ili na Lissu naye apokee kijiti.

Na kutokana na huu mgawanhiko wao, hata matusi nayo naona yamepungua kwa sehemu kubwa; na hasa kwa sisi wapenda mabadiliko tusio na vyama, na ambao tangu uchaguzi wa mwisho kufanyika, tulishauri kamanda mkuu awaachie wengine! Lakini tuliishia tu kupingwa, na hata kutukanwa.
 
Siku zote muda ni muamuzi wa haki.
 
John Heche kwenye ukurasa wake wa Twitter ame- repost ujumbe wa David Mfugwa wa Chadema ambao unamtaka Mbowe kustaafu kwa heshima na kulinda heshima yake ndani ya Chadema. Hii ina maana kuwa hata Heche hakubaliani na kauli ya #Mi5tena.

Msimamo wetu hautaturudisha nyuma. Ni ama Mwamba avuke na hao machawa wanaoitakia mabaya Chadema au Chadema ivuke kwa kishindo huku Mwamba akishuhudia matunda yake ya kujenga wengine kisiasa. Hii chansi ni ya muhimu sana isichezewe.
View attachment 3180129
Kama mnaamini kweli katika demokrasia kwa nini hamtaki Mbowe agombee? Kama muda wake umepita na mnamtaka Lissu si mumpigie tu kura Lissu? Kwa nini mnataka Lissu apite bila kupingwa? Waache washindane, waeleze makusudio yao na chama halafu wenye mamlaka ya kupiga kura waamue.

Amandla...
 
Hivyo Henche naye kajiunga kwenye ule msafara wa Lissu wa kung'atuka chadema uliotanguliwa na Msigwa. Msafara unazidi kuwa mrefu. CCM wachekelea.
 
Mzee Mbowe ndio shida ,hiki chama atabaki na wamangi watupu
 
Mimi naamini Mbowe na Lissu wanawachezesha ngoma wapinzani wao tu !

Mtu mwenye Kutafakari majambo kwa kina atajua tu kwamba Mbowe na Lissu sio watu wa kugombana au wa kuweza kugombanishwa na yeyote yule 😳🙄🤩
Ngoja Tusubiri tuone 🙏
Wewe una matatuzo hii sio movie kama ulidhani hivyo umepotea
 
Back
Top Bottom