upupu255
Senior Member
- Sep 4, 2024
- 119
- 144
Hapo jana Februari 12, akiwa kwenye mkutano wake wa hadhara Sirari, jimbo la Tarime vijijini, Makamu Mwenyekiti Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche amehoji juu ya kukamatwa na kunyimwa dhamana kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Wilbroad Slaa na pia endapo akifariki taarifa itakayotolewa itakuwa ya aina gani.
Soma: Kesi ya Dkt. Slaa imeahirishwa mpaka Februari 18, 2025
"Mzee kama Dkt. Slaa mzee wa miaka 76 amekuwa mbunge kwa miaka 15, amekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA amekuwa Balozi,unamkamata kesi ambayo ina dhamana unatumia mahakama kumuangamiza, hivi akikufia Rais Samia unamtoaje unatuambiaje watu? kwamba amekufa tu kifo cha kawaida, leo wakakuambia Dkt. Slaa hatupo naye tena unawaambiaje watanzania"