John Heche: Hizi ni kodi na ushuru wa serikali kwa gari ndogo tu Crown

John Heche: Hizi ni kodi na ushuru wa serikali kwa gari ndogo tu Crown

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,815
Reaction score
103,955
Hizi ni kodi na ushuru wa serikali kwa gari ndogo tu Crown.

Fikiria kijana ambae ameanza maisha hapa Dar, kutokana na adha ya usafiri anajibana ananunua kagari ka usd 6,000 ambazo ni sawa na 14 m.

Hiyo gari ikifika inatozwa ushuru mwingine wa 14 m, yaani fikiria ushuru unalingana na ununuzi wa gari!!!

Yaani gari Machuma yote, engineering iliyopo pale kwenye gari unanunua bei sawa na ushuru wa mtu ambae amekaa ofisini tu na anakuchaji hela yote hiyo!!!!

Wakati mwingine kodi zinakua bei juu kuliko manunuzi!!!!

Huyu kijana awe mkulima au mfanyakazi, anafanya kazi ngumu sana kupata hiyo fedha, then inachukuliwa hivi…

Alafu baada ya mda CAG anasoma ripoti kwamba uwanja ulitakiwa kujengwa kwa bilioni 187 baadae ukajengwa kwa bilioni 337..

Mara umekaa unaambiwa kuna eti Waziri anatumia gari binafsi ya bilioni 2, unajiuliza mtumishi wa umma ametoa wapi bilioni 2 kununua gari na mshahara wake unafahamika, au anamiliki nyumba tano za thamani ya bilioni tatu, nne au tano… aniliki mashamba ya mabilioni, amempa mama mkwe wake nyumba ya bilioni tano na gari la kutembelea la milioni 500.

Pesa zote hizi za mlipa kodi anaeumizwa kiasi hiki na mzigo wa kodi…

Hapa nimesema magari tu, Ukienda kwenye kila kitu kinachoingizwa na kutoka Nchini ni mzigo wa kodi na maumivu kwa Mwananchi..

Na mwisho wa siku badala hizi fedha zitumike kwaajili ya maendeleo yetu zinaishia kwenye mifuko ya vibaka.

Hakuna barabara, hakuna maji, hakuna umeme.. Maisha magumu , mishahara duni hasa kwa walimu na manesi.

Hatuwezi kukubali kuwa watumishi wa vibaka wanaopora mali za umma

hec.png

20260421_081700.jpg
 
Gari unanunua 4mil unakuja Lipa ushuru na makato 8mil eeeh hii ni maajabu only in Tanzania…. Mfano huo hapo juu gari $4,806 kuja kulitoa ulipie 14,279,035.20
Sijui nini kilibadilika. Zamani ukiagiza gari, makato yote yalikuwa yanafikia kama 50% ya CIF. . Wakati huo TRA walikua wanaonea watu kwa kitu kinaitwa "price uplift"

Nadhani walafi waliingia madarakani. Na wengi wao japo wana mahela mengi ya ufisadi mara nyingi kodi hizi wanasamehewa hawalipi
 
Zamani kodi ilikuwa inapangwa na bunge kwa hiyo ikipangwa mwezi wa 7 mabadiliko ni mpaka mwezi wa 7 mwaka ufuatao, sasa hivi ni muamuzi ni kamishna tu na wahuni wenzake wanapanga wanavyojisikia.

Kwa hiyo gari la model flani, unaweza kukalipa kodi tofauti ndani ya miezi miwili. Mfano Aprili kodi inaweza kuwa shilingi milioni 5 na atayeagiza gari kama hilo mwezi Mei akalipa kodi shilingi milioni 5 na nusu
 
Kweli kabisa Mkuu. Kuna wakati Kamishna wa TRA kaenda kwa raisi na kusema kuna mwanya mwingine wa kupata kodi. Magari yote ya exemption yawe yanatozwa kodi ya uchakavu, hata kama hayalipiwi import duty! Raisi akakubali na kumsifia kamishna ana akili ya kutafuta pesa!

Sasa fikiria, gari za exemption zinatozwa kodi ya uchakavu japo hiyo haipo kwenye sheria ya kodi, kwa sababu kamishna kajipendekeza kwa raisi!

Kuna watu wanapenda sifa ni balaa!
 
Kwa Kodi hizi sioni dalili ya kuboresha usafiri wa umma.

Ni kama vile GOv wana kiwanda cha magari nao wauza.

Mjapani akiingiza Milioni 10 na Gov inaingiza milioni 10.

Biashara nzuri sana hii.
Na ukihoji kuwa kwa nini gari linalouzwa Burundi kwenye yard ni bei nafuu kuliko linalouzwa hapa kwetu wakati wa Burundi hawana badari na wametumia bandari yetu, majibu utayopewa ni kuwa uhamie Burundi.
 
Upuuzi sana Mzee. Zambia tuu hapo unaweza pata Harvester nzuri sana bei chee, itoe sasa kule kuileta kwa watoza ushuru. Mbona utaiacha hapo hapo.
Nchi ya kingese sana hii.
 
Na hizo kodi zote zinamuhusu mtanzania mlala hoi wao viongozi haramu wanajipitishia magari yao free.

Gari moja imebeba kodi zaidi ya 7 na bado ukilitoa bandarini unakutana na kujaza mafuta kuna kodi pia.

Mwisho wa siku pesa zote zinaishia kwa wajanja wachache.

Matumizi ya kawaida Tillion 4 pesa za mradi billion 6. Hapo kuna mradi utaisha kweli??
 
Sijui nini kilibadilika. Zamani ukiagiza gari, makato yote yalikuwa yanafikia kama 50% ya CIF. . Wakati huo TRA walikua wanaonea watu kwa kitu kinaitwa "price uplift"

Nadhani walafi waliingia madarakani. Na wengi wao japo wana mahela mengi ya ufisadi mara nyingi kodi hizi wanasamehewa hawalipi
Sahizi latest Cif ni 60% to 100% , wakati rewanda ni 50% na kushuka, ethiopia kwa hari za EV ni 0 kabisa

Majirani zetu ziko low . Sijui hii nchi think tanks wake wakiamka daily wanawaza kodi kubwa

Hawana more ideas
 
Back
Top Bottom