John Heche: Hizi ni kodi na ushuru wa serikali kwa gari ndogo tu Crown

John Heche: Hizi ni kodi na ushuru wa serikali kwa gari ndogo tu Crown

Hatuwezi kukubali kuwa watumishi wa vibaka wanaopora mali za umma
Nini mta 'do!'

Kwani hawajui kuwa hamuwezi kukubali?
Wanajuwa, ndiyo maana inabidi wawaue mnapojaribu kukataa.

Kiukweli, katika tawala zote tulizowahi kuzishuhudia hapa Tanzania; hakuna hata moja iliyokuwa na kiburi cha waziwazi kabisa kwa wananchi wake kama huu wa huyu mwanamke mwovu kabisa.

Tena anafanya hata upige kelele kiasi gani ni kama alivyosema yeye kuwa "chura kiziwi"!

Huyu maswala ya ufisadi ni kama ndiyo ajenda kuu anayoisimamia kuiimarisha zaidi hapa nchini
 
Naichukia sana CCM, yaani hamjui tu.
Ni ngumu sana kukubishia kuhusu hili la kuichukia CCM; binafsi nawachukia zaidi wanaojiita viongozi wa hiyo CCM.
CCM inaweza kubadilika siku yoyote ikiwa na viongozi wanaojali maslahi ya taifa hili; kama ilivyowahi kuwa huko miaka ya nyuma.
 
KULIPA KODI NI LAZIMA SIO HIYARI GENTLEMAN,
NA UKIKWEPA UTANYAKWA TU. lazima kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa letu kuliko kulalamikia vitu vidogovidogo kama hivyo viushuru ambavyo havikwepeki hata utoe machozi ya damu.

Lazima kulipa kodi na ushuru bila mbambamba
Heche alipokua mbunge na liV8 la mkopo la milioni mia4 hakuona huo ushuru wala hiyo kodi mpaka alipofilisika pensioni yote ya ubunge kwenye kubeti.
Unakatwa na baba mkwe kwa nyma
 
Unajuwa kwanini?

Ni kukosa akili ya kubuni vyanzo vipya vya mapato, ccm imeacha sehemu nyingi sana hela zinapotea bure mfano kwenye madini ila wamejikita kukamua sehemu zilezile miaka yote.
Ndio maana sasa hivi wkaanzisha tozo kwenye luku eti kodi ya jengo!
Ccm haina uwezo wowote ndio maana inataka kukusanya kwa mteremko mfano ipo hai, na huyu pimbi wao muuaji wa sasa hivi ndio sifuri kabisa.

Mafisadi watajwe waone aibu.
 
Ni ngumu sana kukubishia kuhusu hili la kuichukia CCM; binafsi nawachukia zaidi wanaojiita viongozi wa hiyo CCM.
CCM inaweza kubadilika siku yoyote ikiwa na viongozi wanaojali maslahi ya taifa hili; kama ilivyowahi kuwa huko miaka ya nyuma.
Kuwa na matumaini kuwa CCM inaweza kubadilika huko mbeleni ni dalili za mtu aliyeingia katika mfumo wao. CCM wanaharibu kwa makusudi halafu wanaahidi kujisahihisha.

Mfumo wa vyama vingi upo ili chama kinapoharibu kiadhibiwe katika sanduku la kura. Kama kwa makusudi wamefunga nafasi zote za kuadhibiwa kinyume cha sheria tulizojiwekea, hiko siyo chama cha kukitumainia wala kukitegemea.
 
Kuwa na matumaini kuwa CCM inaweza kubadilika huko mbeleni ni dalili za mtu aliyeingia katika mfumo wao. CCM wanaharibu kwa makusudi halafu wanaahidi kujisahihisha.
Hapana; sijaingia na wala siwezi kuingia katika huo "mfumo", hata sielewi maana ya huo mfumo ni kitu gani!

Chama chochote cha siasa hakiwezi kuwa na matumaini yoyote kwa wananchi bila ya kuwa na viongozi wanaojali maslahi ya watu wanaowaongoza.
Ni hao hao viongozi wanaolea hiyo inayoitwa mifumo; kwa sababu wanafaidika nayo. Kiongozi anayeweka mbele ufanisi wa nchi ni lazima aondokane na hiyo mifumo.
 
Aisee Nchi ya hovyo sana hii na hiyo ni ya 2012 kazi ipo wameagiza mashine za kukagua magari kwa thamani ya 300 billion wakati wangepunguza kodi tu watu wangeleta magari ya miaka ya karibuni hayo chakavu yangepungua bara barani..
 
Sijui nini kilibadilika. Zamani ukiagiza gari, makato yote yalikuwa yanafikia kama 50% ya CIF. . Wakati huo TRA walikua wanaonea watu kwa kitu kinaitwa "price uplift"

Nadhani walafi waliingia madarakani. Na wengi wao japo wana mahela mengi ya ufisadi mara nyingi kodi hizi wanasamehewa hawalipi
Unajua kuna kitu kimoja watu hawajui, hata ukipata mlima au chumba kilichojaa pesa kwa dhuluma na wizi mwisho wa siku zitaishia kuteseka kwa presha, magonjwa yasiyoisha na figo mbovu na utoona furaha ya kweli ya maisha kwa kuwa uzee wako utakuwa na taabu na majuto.
 
Aisee Nchi ya hovyo sana hii na hiyo ni ya 2012 kazi ipo wameagiza mashine za kukagua magari kwa thamani ya 300 billion wakati wangepunguza kodi tu watu wangeleta magari ya miaka ya karibuni hayo chakavu yangepungua bara barani..
Nchi ambayo kiongozi mmoja anatembea kwenye gari la Tzs 400M Wakati watoto wa shule wanakaa chini, shule nyingine hazina madawati,wananchi wanaangaika barabara na usafiri wa kwenda kazini? Kiongozi ni mtumishi wa umma anatakiwa kuishi maisha ya kawaida sana na ndio sifa ya kutumikia watu, tujifunze kwa wanaotufsdhili, viongozi wao wanaishi maisha ya kawaida sana.
 
Hizi ni kodi na ushuru wa serikali kwa gari ndogo tu Crown.

Fikiria kijana ambae ameanza maisha hapa Dar, kutokana na adha ya usafiri anajibana ananunua kagari ka usd 6,000 ambazo ni sawa na 14 m.

Hiyo gari ikifika inatozwa ushuru mwingine wa 14 m, yaani fikiria ushuru unalingana na ununuzi wa gari!!!

Yaani gari Machuma yote, engineering iliyopo pale kwenye gari unanunua bei sawa na ushuru wa mtu ambae amekaa ofisini tu na anakuchaji hela yote hiyo!!!!

Wakati mwingine kodi zinakua bei juu kuliko manunuzi!!!!

Huyu kijana awe mkulima au mfanyakazi, anafanya kazi ngumu sana kupata hiyo fedha, then inachukuliwa hivi…

Alafu baada ya mda CAG anasoma ripoti kwamba uwanja ulitakiwa kujengwa kwa bilioni 187 baadae ukajengwa kwa bilioni 337..

Mara umekaa unaambiwa kuna eti Waziri anatumia gari binafsi ya bilioni 2, unajiuliza mtumishi wa umma ametoa wapi bilioni 2 kununua gari na mshahara wake unafahamika, au anamiliki nyumba tano za thamani ya bilioni tatu, nne au tano… aniliki mashamba ya mabilioni, amempa mama mkwe wake nyumba ya bilioni tano na gari la kutembelea la milioni 500.

Pesa zote hizi za mlipa kodi anaeumizwa kiasi hiki na mzigo wa kodi…

Hapa nimesema magari tu, Ukienda kwenye kila kitu kinachoingizwa na kutoka Nchini ni mzigo wa kodi na maumivu kwa Mwananchi..

Na mwisho wa siku badala hizi fedha zitumike kwaajili ya maendeleo yetu zinaishia kwenye mifuko ya vibaka.

Hakuna barabara, hakuna maji, hakuna umeme.. Maisha magumu , mishahara duni hasa kwa walimu na manesi.

Hatuwezi kukubali kuwa watumishi wa vibaka wanaopora mali za umma

View attachment 3576665


Ni hatari sana
 
Back
Top Bottom