John Heche: Hizi ni kodi na ushuru wa serikali kwa gari ndogo tu Crown

John Heche: Hizi ni kodi na ushuru wa serikali kwa gari ndogo tu Crown

Na hizo kodi zote zinamuhusu mtanzania mlala hoi wao viongozi haramu wanajipitishia magari yao free.

Gari moja imebeba kodi zaidi ya 7 na bado ukilitoa bandarini unakutana na kujaza mafuta kuna kodi pia.

Mwisho wa siku pesa zote zinaishia kwa wajanja wachache.

Matumizi ya kawaida Tillion 4 pesa za mradi billion 6. Hapo kuna mradi utaisha kweli??
Ok
 
Ukitaka kununua gari Moja weka bajeti ya kununua magari mawili Huwa najiuliza hawa jamaa ni ubinafsi au Nini haingii akilini kwamba Bei ya gari inakuwa ndogo kuliko Kodi Yani hapa lengo ni kuzuia watanzania wasimiliki magari ila wao tu ndio wamiliki alafu barabara mbovu foleni za kutosha hii nchi ni kituko hasa,basi boresheni public transport na barabara hakuna ukifikiria sana hii nji unaweza kuwa mwehu
 
Hizi ni kodi na ushuru wa serikali kwa gari ndogo tu Crown.

Fikiria kijana ambae ameanza maisha hapa Dar, kutokana na adha ya usafiri anajibana ananunua kagari ka usd 6,000 ambazo ni sawa na 14 m.

Hiyo gari ikifika inatozwa ushuru mwingine wa 14 m, yaani fikiria ushuru unalingana na ununuzi wa gari!!!

Yaani gari Machuma yote, engineering iliyopo pale kwenye gari unanunua bei sawa na ushuru wa mtu ambae amekaa ofisini tu na anakuchaji hela yote hiyo!!!!

Wakati mwingine kodi zinakua bei juu kuliko manunuzi!!!!

Huyu kijana awe mkulima au mfanyakazi, anafanya kazi ngumu sana kupata hiyo fedha, then inachukuliwa hivi…

Alafu baada ya mda CAG anasoma ripoti kwamba uwanja ulitakiwa kujengwa kwa bilioni 187 baadae ukajengwa kwa bilioni 337..

Mara umekaa unaambiwa kuna eti Waziri anatumia gari binafsi ya bilioni 2, unajiuliza mtumishi wa umma ametoa wapi bilioni 2 kununua gari na mshahara wake unafahamika, au anamiliki nyumba tano za thamani ya bilioni tatu, nne au tano… aniliki mashamba ya mabilioni, amempa mama mkwe wake nyumba ya bilioni tano na gari la kutembelea la milioni 500.

Pesa zote hizi za mlipa kodi anaeumizwa kiasi hiki na mzigo wa kodi…

Hapa nimesema magari tu, Ukienda kwenye kila kitu kinachoingizwa na kutoka Nchini ni mzigo wa kodi na maumivu kwa Mwananchi..

Na mwisho wa siku badala hizi fedha zitumike kwaajili ya maendeleo yetu zinaishia kwenye mifuko ya vibaka.

Hakuna barabara, hakuna maji, hakuna umeme.. Maisha magumu , mishahara duni hasa kwa walimu na manesi.

Hatuwezi kukubali kuwa watumishi wa vibaka wanaopora mali za umma

View attachment 3576665

KULIPA KODI NI LAZIMA SIO HIYARI GENTLEMAN,
NA UKIKWEPA UTANYAKWA TU. lazima kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa letu kuliko kulalamikia vitu vidogovidogo kama hivyo viushuru ambavyo havikwepeki hata utoe machozi ya damu.

Lazima kulipa kodi na ushuru bila mbambamba
Heche alipokua mbunge na liV8 la mkopo la milioni mia4 hakuona huo ushuru wala hiyo kodi mpaka alipofilisika pensioni yote ya ubunge kwenye kubeti.
 
Kuna shida kubwa sana kwenye "akili" ya hawa wanaojiita "viongozi". Hapo wakisimama kwenye majukwaa wanasisitiza kwa sauti kubwa sana uzalendo wasioweza onyesha kwa vitendo.

Hapo bado unalipia msururu wa Kodi na tozo mbalimbali kwenye Kila Lita Moja ya mafuta utakayotumia kipindi chote Cha uhai wa gari.
 
KULIPA KODI NI LAZIMA SIO HIYARI GENTLEMAN,
NA UKIKWEPA UTANYAKWA TU. lazima kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa letu kuliko kulalamikia vitu vidogovidogo kama hivyo viushuru ambavyo havikwepeki hata utoe machozi ya damu.

Lazima kulipa kodi na ushuru bila mbambamba
Heche alipokua mbunge na liV8 la mkopo la milioni mia4 hakuona huo ushuru na kodi mpaka alipofilisika pensioni yote ya ubunge kwenye kubeti.
CCM ni kenge mpaka damu masikioni.
 
CCM ni kenge mpaka damu masikioni.
Heche na wewe mnaweza kua na ufahamu mdogo ulio sawa,

kwasababu ni vitu nonsense sana,
yaani ukiwa na fursa ya kutoa hoja ya kurekebisha hicho unachotaftia kiki kindezindezi tu mitandaoni, hukufanya hivyo,

eti umeshafilisika pensioni yako yote ya ubunge, umepoteza uelekeo wa kisiasa, eti sasa ndio unakuja kumbwelambwela nonsense jukwaani:pedroP:

kweli ukiparara kiuchumi unaparara kifikra, kiakili na kuparara kila kitu.:pedroP:
 
Shida sio kukusanya kodi, Shida ni Matumizi ya hyo kodi.

Yaani kodi zoote hizo, Mbu piga hesabu:

1.Huduma hospitalini ni mbovu - Hapa unalazimika kwenda private au Nje ya nchi kama issue ni critical

2. Huduma za Elimu ni mbovu - Hapo unalazimika kusomesha private na internationa school

3. Barabara za mitaa ni mbovu - Hapa maintanace cost ya gari inakua kubwa.

4. Foleni kubwa mijini - Fuel cost inakua kubwa.

5.Umeme shida - hapa unalazimisha kua na Solar/Generator.

6.Maji ji shida - Hapa unalazimika kua na matank kama ww ndo DAWASCO, Au uchimbe kisima

Sasa kodi kubwa ila huduma bado ni Duni, Mwisho wa siku kila mtu anaona bora awe mwizi tu, Wafanyakazi wakipata fursa wanapiga, wafanya biashara hawataki kulipa ushuru, Nchi inakua kama failed state.
 
Heche na wewe mnaweza kua na ufahamu mdogo ulio sawa,

kwasababu ni vitu nonsense sana,
yaani ukiwa na fursa ya kutoa hoja ya kurekebisha hicho unachotaftia kiki kindezindezi tu mitandaoni, hukufanya hivyo,

eti umeshafilisika pensioni yako yote ya ubunge, umepoteza uelekeo wa kisiasa, eti sasa ndio unakuja kumbwelambwela nonsense jukwaani:pedroP:

kweli ukiparara kiuchumi unaparara kifikra, kiakili na kuparara kila kitu.:pedroP:

Mida ya ku collect 7000 ndo hii mkuu, sasa wewe zubaa na sisi mawinga tunao jilipia data.
 
Usituone kama matako yako ww ni mzee wa hovyo.
 
Usituone kama matako yako ww ni mzee wa hovyo.

mnabebwa ufala kindezindezi sana gentleman,
yaani mtu aliekua na fursa ya kuibua hiyo kama changamoto na kupendekeza marekebisho akiwa bungeni, halafu eti ameshindwa ubunge na kufilisika pension ya ubunge hali ambayo sasa inamuwia vigumu hata kulipia ushuru wa hako kagari maskini heche dah?

na kama minyumbu na vijana wa hovyo wanaona heche kaongea kitu kipya na cha maana kweli, kumbe kashindwa kulipia ushuru tu :pedroP:

hizo kodi na ushuru zilikuepo tangu zamani na zitaendelea kuongezeka kulingana na ongezeko la bei ya soko na gharama za usafirishaji.

HIYO KODI KAMWE HAIKWEPEKI NA HAIWEZI KUONDOLEWA
 
Mida ya ku collect 7000 ndo hii mkuu, sasa wewe zubaa na sisi mawinga tunao jilipia data.
alivyokua mbunge alinunua v8 ya milioni mia4,
NA WAKATI HUO HAKUONA HUO USHURU NA HIYO KODI KAMA NI GHALI SANA.

sasa heche kafilisika kiuchumi na kifikra mpaka kufikia hatua ya kushindwa kulipia ushuru wa Crown, kweli? :pedroP:

maisha yanaenda kwa kasi sana,
halafu V8 yake aliiuza kwa bei ya mboga sana alipoondamwa na madeni ya kausha damu.
 
Mda wa kuwaondoa CCM umefka...
Wametosha kuiba mali zetu.

Tozo nyingi afu mabalabala hayapitiki.
Miundombinu yote mibovu.

Na mwisho, tanzania tukubari tu hatuna viongozi.
kwan hakuna aliyechaguliwa na mwananchi kama katiba inavosema.

mwisho leo kuwaita majina ya vyeo vya uongoz kama:
RAIS
WAZIRI
MBUNGE
n.k
 
Ndiyo maana tunasema rasilimali za nchi ikiwemo bandari havimnufaishi Mtanzania. Tunajitapa tuna bandari ila wasio na bandari wanafaidika na bandari hiyo kuliko mtanzania mwenyewe. Naichukia sana CCM, yaani hamjui tu.
 
Back
Top Bottom