Mfikirishi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,418
- 13,747
Hivi gari ndo zinaleta HIV hadi zitozwe tozo hiyo??View attachment 3576775
Gari unanunua 4mil unakuja Lipa ushuru na makato 8mil eeeh hii ni maajabu only in Tanzania…. Mfano huo hapo juu gari $4,806 kuja kulitoa ulipie 14,279,035.20
Kwa Kodi hizi sioni dalili ya kuboresha usafiri wa umma.
Ni kama vile GOv wana kiwanda cha magari nao wauza.
Mjapani akiingiza Milioni 10 na Gov inaingiza milioni 10.
Biashara nzuri sana hii.
Usisahau mkuu 'Tate', hakuna aliyekubali' wote tunatawaliwa kwa mabavu!Kwa hali hii kuna mtu mwenye akili timamu kichwani atakubali kweli kuendelea kutawaliwa na haya majambazi!
Nini mta 'do!'Hatuwezi kukubali kuwa watumishi wa vibaka wanaopora mali za umma
Ni ngumu sana kukubishia kuhusu hili la kuichukia CCM; binafsi nawachukia zaidi wanaojiita viongozi wa hiyo CCM.Naichukia sana CCM, yaani hamjui tu.
Unakatwa na baba mkwe kwa nymaKULIPA KODI NI LAZIMA SIO HIYARI GENTLEMAN,
NA UKIKWEPA UTANYAKWA TU. lazima kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa letu kuliko kulalamikia vitu vidogovidogo kama hivyo viushuru ambavyo havikwepeki hata utoe machozi ya damu.
Lazima kulipa kodi na ushuru bila mbambamba
Heche alipokua mbunge na liV8 la mkopo la milioni mia4 hakuona huo ushuru wala hiyo kodi mpaka alipofilisika pensioni yote ya ubunge kwenye kubeti.
calm down kama huna hoja gentlemanUnakatwa na baba mkwe kwa nyma
Kuwa na matumaini kuwa CCM inaweza kubadilika huko mbeleni ni dalili za mtu aliyeingia katika mfumo wao. CCM wanaharibu kwa makusudi halafu wanaahidi kujisahihisha.Ni ngumu sana kukubishia kuhusu hili la kuichukia CCM; binafsi nawachukia zaidi wanaojiita viongozi wa hiyo CCM.
CCM inaweza kubadilika siku yoyote ikiwa na viongozi wanaojali maslahi ya taifa hili; kama ilivyowahi kuwa huko miaka ya nyuma.
Hapana; sijaingia na wala siwezi kuingia katika huo "mfumo", hata sielewi maana ya huo mfumo ni kitu gani!Kuwa na matumaini kuwa CCM inaweza kubadilika huko mbeleni ni dalili za mtu aliyeingia katika mfumo wao. CCM wanaharibu kwa makusudi halafu wanaahidi kujisahihisha.
Unajua kuna kitu kimoja watu hawajui, hata ukipata mlima au chumba kilichojaa pesa kwa dhuluma na wizi mwisho wa siku zitaishia kuteseka kwa presha, magonjwa yasiyoisha na figo mbovu na utoona furaha ya kweli ya maisha kwa kuwa uzee wako utakuwa na taabu na majuto.Sijui nini kilibadilika. Zamani ukiagiza gari, makato yote yalikuwa yanafikia kama 50% ya CIF. . Wakati huo TRA walikua wanaonea watu kwa kitu kinaitwa "price uplift"
Nadhani walafi waliingia madarakani. Na wengi wao japo wana mahela mengi ya ufisadi mara nyingi kodi hizi wanasamehewa hawalipi
Nchi ambayo kiongozi mmoja anatembea kwenye gari la Tzs 400M Wakati watoto wa shule wanakaa chini, shule nyingine hazina madawati,wananchi wanaangaika barabara na usafiri wa kwenda kazini? Kiongozi ni mtumishi wa umma anatakiwa kuishi maisha ya kawaida sana na ndio sifa ya kutumikia watu, tujifunze kwa wanaotufsdhili, viongozi wao wanaishi maisha ya kawaida sana.Aisee Nchi ya hovyo sana hii na hiyo ni ya 2012 kazi ipo wameagiza mashine za kukagua magari kwa thamani ya 300 billion wakati wangepunguza kodi tu watu wangeleta magari ya miaka ya karibuni hayo chakavu yangepungua bara barani..
Wao wanachangia nini kwenye kapu?Mapato mengi hupelekwa zanzibar ndiyo maana tunakamuliwa vya kutosha.31%ya marathon yanaenda zanzibar kwa length eti kudumisha muungano
Ndio, hujui jinsi magari yanavyotumika kwenye mambo ya ovyo? Natania asee, ni swali kuntu linalohitaji majibu ya kweli.Hivi gari ndo zinaleta HIV hadi zitozwe tozo hiyo??
Ni hatari sanaHizi ni kodi na ushuru wa serikali kwa gari ndogo tu Crown.
Fikiria kijana ambae ameanza maisha hapa Dar, kutokana na adha ya usafiri anajibana ananunua kagari ka usd 6,000 ambazo ni sawa na 14 m.
Hiyo gari ikifika inatozwa ushuru mwingine wa 14 m, yaani fikiria ushuru unalingana na ununuzi wa gari!!!
Yaani gari Machuma yote, engineering iliyopo pale kwenye gari unanunua bei sawa na ushuru wa mtu ambae amekaa ofisini tu na anakuchaji hela yote hiyo!!!!
Wakati mwingine kodi zinakua bei juu kuliko manunuzi!!!!
Huyu kijana awe mkulima au mfanyakazi, anafanya kazi ngumu sana kupata hiyo fedha, then inachukuliwa hivi…
Alafu baada ya mda CAG anasoma ripoti kwamba uwanja ulitakiwa kujengwa kwa bilioni 187 baadae ukajengwa kwa bilioni 337..
Mara umekaa unaambiwa kuna eti Waziri anatumia gari binafsi ya bilioni 2, unajiuliza mtumishi wa umma ametoa wapi bilioni 2 kununua gari na mshahara wake unafahamika, au anamiliki nyumba tano za thamani ya bilioni tatu, nne au tano… aniliki mashamba ya mabilioni, amempa mama mkwe wake nyumba ya bilioni tano na gari la kutembelea la milioni 500.
Pesa zote hizi za mlipa kodi anaeumizwa kiasi hiki na mzigo wa kodi…
Hapa nimesema magari tu, Ukienda kwenye kila kitu kinachoingizwa na kutoka Nchini ni mzigo wa kodi na maumivu kwa Mwananchi..
Na mwisho wa siku badala hizi fedha zitumike kwaajili ya maendeleo yetu zinaishia kwenye mifuko ya vibaka.
Hakuna barabara, hakuna maji, hakuna umeme.. Maisha magumu , mishahara duni hasa kwa walimu na manesi.
Hatuwezi kukubali kuwa watumishi wa vibaka wanaopora mali za umma
View attachment 3576665