Pre GE2025 John Heche kumuunga mkono Lissu asema Lissu ni mkweli, muwazi na muadilifu sana

Pre GE2025 John Heche kumuunga mkono Lissu asema Lissu ni mkweli, muwazi na muadilifu sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sifa anazo kikatiba, tatizo anashtumu viongozi wenzake halafu anataka kuwaongoza, wapi umeona duniani hivyo?
Nini maana ya kampeni? Maana ya kampeni ni kusimama na mapungufu ya yule unayeshindana nae
 
Mbowe hajazoea kampeni alizoea kupita bila kupingwa sasa 2024 ipo kivingine lazima madudu ya mbowe yaanikwe kwani si mageni yapo kitambo tokea kipindi cha wangwe zito na wengineo
mbowe kitu cha kufanya ni kuchukua maamuzi ya kukubaliana tu kwamba ni muda wa wengine kuendesha gurudumu. issue ya pesa kwenye chama, idea ya lissu ipo more logical zaidi chama kitafute pesa za chama
 
Mbowe hajajenga chadema peke yake chadema imejengwa na wengi ingawa pesa za chama hufujwa na mbowe peke kwani ndiyo mhasibu wa chama hataki hata katibu mkuu aguse idara ya pesa
 
mbowe kitu cha kufanya ni kuchukua maamuzi ya kukubaliana tu kwamba ni muda wa wengine kuendesha gurudumu. issue ya pesa kwenye chama, idea ya lissu ipo more logical zaidi chama kitafute pesa za chama
Mbowe anaogopa kuachia uenyekiti kwa sababu ya wizi mkubwa wa pesa za chama aliofanya ana hofu akiingia mwenyekiti mpya ambaye hajamuandaa yeye ataibua madudu yake mengi ya kula pesa za misaada michango Rushwa za ngono viti maalum na mambo mengi ya hovyo
 
Tapeli unakimbia kuthibitisha. Mbona wenje kasema alienda na Abdul kwa lisu akawatimua. Thibitsha hiyo Heche kupewa rushwa
Wewe unaishi huko Kongoto mambo mengine huwezi yajua
 
Mbowe alitamani sana kuachia uenyekiti wa Chama kwa heshima na aendelee kuwa mjumbe wa kudumu wa Kamati nyeti. Ila sasa, machawa ambao hawawezi kusurvive bila yeye na baadhi ya watu ndani ya mfumo either wamemconvince aendelee kubaki au wamemtisha kwamba maslahi yake yatakuwa shakani kama ataachia kiti

Hata kama Mbowe atashinda kiti, heshima yake kwa jamii na imani ya wananchi wapenda mabadiliko wasio na kadi za chama chochote cha siasa (ambao ni wengi sana) itapotea kwa Chadema na CCM haitohitaji kuiba kura nyingi hapo October 2025
100/100
 
Hali ilivyo sasa ni kuwa Wajumbe wengi moyoni wapo na Lisu lakini kwa kuogopa Udikteta wa mbowe wameamua kuwa na mbowe usoni wale pesa zake lakini watamnyoosha kwenye sanduku la kura ingawa kamati ya Roho mbaya ikiongozwa na Mdee wenje Bonfire wanajipanga kuiba kura kufanya uchakachuaji kupora ushindi wa Lisu na
 
Rushwa ya ngono viti maalum uliye karibu bado inaendelea? uliye karibu pesa za chama zipo wapi hadi Mbowe kuitisha michango
 
Wewe unaishi huko Kongoto mambo mengine huwezi yajua
Uliye karibu mbona humshauri Mbowe aache kuiba pesa za chama kisha kuzitakatisha kwa kisingizio cha kukopesha chama
 
==
Mhe John Heche anasema yeye waziwazi anamuunga mkono Mhe Tundu Lissu kwa sababu ni mtu mkweli sana ni muadilifu sana na anachukia rushwa kwa moyo na nguvu zake zote.

Mhe John Heche ilitarajiwa na wengi kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa lakini baada ya Mhe Tundu Lissu kuamua kugombea yeye ameamua kumpisha Tundu Lissu kwani anaamini nafasi hiyo ya Uenyekiti anaiweza zaidi na ndio sababu ya kumuunga mkono.

Mpaka sasa haijafahamika kama John Heche atagombea nafasi yoyote ndani ya chama au atabaki pembeni kumuunga mkono Tundu Lissu,

Tusubiri tuone mpaka hiyo tarehe 05.01.2025 ambae ndio mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu Kwa mujibu wa kalenda ya Uchaguzi ya chama.

View attachment 3189380

==
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (@ChademaTz), @HecheJohn, ameonesha dhamira yake ya kuendelea kupigania mustakabali wa chama hicho na Taifa kwa ujumla.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) leo Jumanne Desemba 31, 2024,
Heche ameandika ujumbe mzito akisisitiza umuhimu wa CHADEMA kama taasisi muhimu kwa maslahi ya taifa na wananchi wa Tanzania.

"Tuna taasisi ya kuilinda, tuna nchi ya kutetea, tuna Watanzania wa kupigania. CHADEMA ikifa madhara yake ni makubwa mno kwa nchi yetu," aliandika Heche.

Katika ujumbe huo, Heche amemuelezea mwanasiasa mashuhuri na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara @TunduALissu, kama kiongozi mwadilifu, mkweli, na mwenye uwazi wa hali ya juu.

"Lissu sio muongo ni mkweli, muadilifu na muwazi," aliandika, akionesha imani yake kubwa kwa Lissu.

Lissu, ambaye kwa sasa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, ameendelea kuungwa mkono na viongozi na wafuasi wa chama hicho.

Uchaguzi wa nafasi hiyo unatarajiwa kufanyika tarehe 21.02.2025.
Heche anachukua Form ya umakamu before closing date na atapita
Matokeo tarajiwa
Lissu mwenyekiti
Heche makamu
Viva CHADEMA.. Viva Tanganyika 💪🏿📌💪🏿
 
AMESHAJICHIMBIA KABURI KWA MTU AMBAYE HATASHINDA UENYEKITI SIJUI WATAKIMBILIA WAPI MBOWE HANA CHA KUPOTEZA AKISHINDA HATA CHAMA KIKIFA HANA SHIDA ATAKUWA AMEWANYOOSHA HAO WANAOMKATAA SASAHIVI
Mawazo ya kimasikini hayo... kuishi kwa kumtegemea mtu , Unashauri aishi kwa kumtegemea Mbowe?
 
Back
Top Bottom