Pre GE2025 John Heche: Makonda anawahoji Polisi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM kwasababu anawaona kama green guard

Pre GE2025 John Heche: Makonda anawahoji Polisi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM kwasababu anawaona kama green guard

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Polisi tunapowaita Policcm kwani Huwa mnapata majibu Gani.
Wanavuna walichokipanda,na Bado.
Makonda anajaribu kuwaonyesha kuwa hawana lolote mbele ya ccm.

Siku za mbele,wataona maana halisi.kama RPC anamfukuza askari,basi itafikia hata kiongozi wa chama Cha ccm atamfukuza Polisi kazi na hakuna atakwenda kulalamika.

Makonda aendelee kuwapekuwa maana hawana maana.

Wana double standard.So,wahenyeshe baba.
 
Kwani hao RPC's ni wakina nani mpaka wasihojiwe na wananchi?

Heche anataka kusema ili kuwahoji hao, kuna sheria maalum imewekwa kuonesha ni wakina nani wanaotakiwa kuwahoji RPC's?

- Kama ni hiyo PGO ndio imeainisha hayo, basi angetuambia ni kifungu kipi ndio kinasema hivyo.

Kama RPC's wamewekwa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi, sioni kwanini wasihojiwe na wananchi wanaowatumikia.

Wale sio mabosi wa wananchi, ni watumishi wa wananchi, na wala hawalipwi mishahara ili wakae ofisini, wanatakiwa kutoka wakasikilize kero za wananchi mitaani.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Acha kufanya watu wajinga kiazi wewe!, Hujui hata mipaka ya kazi!!. Kwahiyo katibu mwenezi wa CCM anawezaje kumhoji?, Au ndio tunatawaliwa kwa akili za kingumbalu Kama zako tutusa wewe.
Makonda awahoji wanachama wake wa CCM sio taasisi ya polisi iliyo na utaratibu wake wakuwajibishana?.
Sema na huyo jamaa ni mpuuzi tu.... Ningekuwa Mimi hayo anayoniuliza ningemjibu yametokea kutokana na uwepo wa CCM... Next time aache upuuzi
 
Sheria zenyewe mnazotaka zifuatwe ndizo hizo hizo mnazolalamikia kuwa zinavunjwa.

Sijui wanasiasa mnasimamia wapi?.
 
Polisi walianza kujiingiza ccm, baadae wakajigeuza kuwa wanachama wa ccm. IGP kadhaa wameruhusu hilo litokee.

Leo Makonda anamuita mtu mwenye level ya RPC anamuhoji kwenye mkutano wa hadhara. Hii inatokea kwasababu Makonda anajua hawa ni wanachama wao.

Polisi wetu wanapaswa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na muongozo wao unaoitwa police general orders (PGOs) ni wapi Makonda na ccm wametajwa kwenye hivyo vitabu..

Kwamba jeshi la polisi lina makosa ni kweli, kwamba watu wanatekwa na serikali ya ccm na wengine kupotezwa kizembe ni kweli. Kwamba polisi wanapaswa kuwajibishwa ni kweli.

Sijwahi kuona hata IGP anawafokea RPCS hadharani.

Lakini RPC anaitwa na kuhojiwa kama mtoto mdogo bila kufuata sheria wala taratibu, huyu anawezaje kusimamia sheria na kutenda haki.

Makonda anawahoji kwenye hadhara kwasababu anawaona nyie ni green guard tu.

Tunahitaji kuunda upya chombo hiki muhimu kitakachoongozwa na watu wenye uwezo na weledi wa kusimamia sheria za Nchi.

Noma sana !
 
!!!!!!!!! Nyie hamna jema hata kidogo !!!!! Mtakushinda uchaguzi mchakuwa mnatembea fimbo na akili zichuwa kama.dish lilioyumba
 
Acha kufanya watu wajinga kiazi wewe!, Hujui hata mipaka ya kazi!!. Kwahiyo katibu mwenezi wa CCM anawezaje kumhoji?, Au ndio tunatawaliwa kwa akili za kingumbalu Kama zako tutusa wewe.
Makonda awahoji wanachama wake wa CCM sio taasisi ya polisi iliyo na utaratibu wake wakuwajibishana?.
Sema na huyo jamaa ni mpuuzi tu.... Ningekuwa Mimi hayo anayoniuliza ningemjibu yametokea kutokana na uwepo wa CCM... Next time aache upuuzi
Wewe mwenye akili hebu tuwekee hapa hiyo sheria inayomkataza Makonda au mwingine yeyote kumhoji RPC.

Iweke hapa wacha kelele. Mnawageuza ma RPC miungu watu kwa ujinga wenu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Haya maagizo kwa polisi yalianza muda mrefu nyuma ya pazia,na polisi wakawa wanatii Kila wanachoambiwa hata amri zilizo kinyume na sheria, yaani maagizo kutoka juu. Baada ya ccm kuona viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wanatii chochote wanachaigizwa bila kujali Sheria, Sasa hivi wanatoka hadharani kuwahoji kwa dharau Ili kupata mtaji wa kisiasa.

Ni kwanini viongozi wa vyombo vya Dola wanawanyenyekea wasiasa?

Kwanza ni kutokana na katiba inayompa madaraka rais ya kuteua Kila kiongozi wa taasisi, na hasa ukizingatia anateua kwa utashi wake bila kushurutishwa na yoyote. Na mara nyingi rais unakuta ni kiongozi wa ccm, hivyo anaweza kumfukuza kiongozi wa taarisisi yoyote bila kuwajibishwa popote.

Pili hizo nafasi za viongozi wa vyombo vya Dola huwa vinaambatana na mshahara mnono, na rushwa kubwa kubwa. Unakuta kiongozi wa chombo Cha Dola amefaidika na rushwa kubwa kubwa, na ana Miradi isiyoendana na kipato chake, hivyo akileta ujuaji anakomolewa kwa kubanwa katika Miradi yake, na wakati mwingine kuishia jela. Hakuna kiongozi yoyote atakubali hayo, Bora adhalilishwe kwa muda kuliko maslahi yake binafsi kuguswa.
[emoji3581]

Sent from my Infinix X6512 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom