John Heche: Tunaongozwa na watu waliokosa maarifa

John Heche: Tunaongozwa na watu waliokosa maarifa

annetta

Senior Member
Joined
Dec 3, 2025
Posts
101
Reaction score
305
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche amesema Serikali ya CCM inaongozwa na watu waliokosa maarifa badala yake wamebaki kutishia wapinzani na kufungua mitandao ya kijamii.

Ameyasema hayo Agosti 12 katika maadhimisho ya vijana kimataifa yaliyofanywa na chama hicho jijini Dodoma.

 
Wizara ya Kilimo ni kama haina mchango wowote kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula nchini.Ubunifu hakuna,zaidi ni upigaji tu.
 
Anaposema "tunaongozwa na watu wenye akili za matope" anamaanisha nini? Yaani kwenye vichwa vya hao watu kumejaa matope badala ya ubongo! Au ni mimi ndiyo sijaielewa hii kauli!!!
 
Uzuri wa mijadala ya mitaani hakuna kuzimwa na Spika wa CCM na miongozo ya Waziri wa Uratibu wa Bunge

John Heche leo Dodoma amesema:

Tunaongozwa na watu wenye akili za matope

Saudi hawana maji hata ya mto mmoja, wanatuuzia ngano
Saudi Arabia si Jangwani? Heche ameongea chumvi hapa🤣🤣
 
Saudi Arabia wanazalisha tani 1.1 millions za ngano. Tanzania tunazalisha tani 120,000. Pamoja na kuwa jangwani wanalima ngano Mara 10 ya Tanzania.
Mkuu Saudi arabia ni nchi kubwa mara 2 na zaidi kushinda tanzania, sio kila sehemu katika hiyo nchi ni jangwa wana miradi ya kisasa na wana pesa hasa.
 
Wao Saudi Arabia wanazalisha kiasi gani cha ngano na Sisi tunazalisha kiasi gani?....Tuna mazingira mazuri Sana ya kuzalisha Hili zao japo Saudia pesa wanazo, Bila kutafuta takwimu nahisi Saudi Arabia wametupita kwenye kuzalisha Hili zao....Wizara ya Kilimo wao kazi Yao sijui huwa ni nini, kile kitambi cha Chongolo ni cha kukitoboa na PINI...
 
Mama weeeee!!!!

Nimeenda nimerudi nimekuta topic imebadilishwa.... huu ni uwongo wa wazi wazi wa moderators wa jamvi hili

WAPI CHUO GANI HICHO MLIFUNDISHWA KULAINISHA NUKUU ZA MANENO YA MTU NDIO UANDISHI ?????

Heche hakusema hivyo na hii sio thread yangu, na sikuandika hivyo

HECHE KASEMA TUNANUNUA NGANO KUTOKA SAUDIA. SAUDI HAWANA HATA MTO MMOJA. HIZO SIO AKILI NI MATOPE.

TENA KABLA YA HAPO ALISEMA NI VIONGOZI NI VICHAA

NA AMETOA MIFANO MIZITO YA KUSUKUMA POINTI ZAKE

SASA KUNA UBAYA GANI KUNUKUU MANENO YA MTU AKIKUMBUSHA NA KU POINT OUT AKILI FINYU ZA JAMII YAKEEEEE ?????

MNALAINISHA NINI MANENO YALIYOSEMWA KWENYE UKUMBI WA WAZ ?????
 
Back
Top Bottom