PostGE2025 John Heche: Walitufuata na kutupa masharti ili Lissu aachiliwe, tumekataa kuwapigia magoti

PostGE2025 John Heche: Walitufuata na kutupa masharti ili Lissu aachiliwe, tumekataa kuwapigia magoti

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
"Lissu, pamoja na kupita magumu yote haya, amekataa kuwapigia magoti hawa wadhalimu... wamejaribu kuweka masharti ambayo sisi tumeyakataa. Mojawapo ya masharti hayo ni kwamba Lissu akubali kuachiliwa lakini aache kufanya siasa ndani ya nchi, aache kuwatetea Watanzania, aondoke akakae nje ya nchi. Lissu amekataa."
Ishara ya "UZALENDO" isiyokuwa na mashaka..

Lissu atatoka gerezani, na hakuna atakayezuia ukombozi wa taifa hili.

Kama swala la kesi yake serikali wameamua lisiendelee, basi ni wakati sasa wa kuanza taratibu nyingine nje ya mahakama kuhakikisha Tundu Lissu anaachiwa huru

ALL OPTIONS ARE LEGITIMATE OUTSIDE OF THE LAW COURTS.
 
Hapa kuna contradiction kubwa sana, waswahili wanasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu. Heche hana kumbukumbu.

Anasema Lissu hali yake kiafya ni mbaya sana na familia wanathibitisha kuwa anapaswa kufanya checkup kila baada ya miezi 3. Halafu anadai kuwa kuna watu wamemfuata kuwa akubali masharti ili aachiwe, ila Tundu amekataa.

Yawesekana checkup ya miezi 3 ni uwongo kwa vile Tundu sasa anamalizai vipande 4 vya miezi mitatu mitatu bila checkup. Angekuwa mtu wa checkup halafu kakosa 2 tu basi hali yake ingekuwa HOVYO au tete.

Pili, hakuna binadamu ana furahi kukaa Rumande hasa kwa mzingira kama aliyopo Tundu. Siamini kwa sasa hivi kama Tundu anaweza kukataa masharti yeyote ya kuwa huru, especially kwa assumption ya kwanza kuwa anaumwa.

Heche ni MWONGO, hizo ni FIKRA zake mbaya baada ya kuvuta bangi kutoka kwa Walenchoka
Kama ulishangilia WaTanzania kuuliwa, utakuwa na lipi jipya kuhusu kudhalilishwa kwa waTanzania?

Wewe umejipambanua kwelikweli kuwa adui wa taifa hili; pamoja na huyo mhalifu Samia Suluhu Hassan mfugaji wako.
Taarifa ni moja tu kwenu: Hamponi.
 
Tundu hawezi kuwa Rais wa Tanzania kwa namna yeyote, iwe ya mapinduzi au ya demokrasia. Watu wa sampuli yake huisha kama Mtikila, Lowassa, Seif Sharrif Hamad, Luatonga Mrema.

Kwa hili nawashauri wote wanaotarajia Tundu ataweza kuwa Rais wa Tz watoke ndotoni, haitokuja kutokea
Ulimuuliza Mhalifu Samia anavyomgwaya Tundu Lissu? Kamzushia kesi ili asikutane naye kwenye kura;na kama hiyo haitoshi bado ikalazimu atangaziwe kura milioni 31 ambazo hazikuwepo.
Na bado huoni aibu kila siku kuja humu JF kujaza uchafu tu wa mtu ambaye waTanzania hawamtaki!

Jiandae kuhamia kwa wajomba; kwa sababu Tundu Lissu hazuiliki tena.
 
Ila mama Ako ndio anasifa za kua Rais
 
Uonevu ni uonevu. Hata angekaa ndani siku moja tulikuwa na haki ya kulalamika. Hata Mandela watu walikuwa wanamlilia kila siku aliyokaa ndani. Mwekeni Lissu hata miaka 30 lakini wapenda haki wataendelea kuwasema kila siku ya hiyo miaka 30.

Amandla...
Hakuna uonevu kwa suala la Tundu. Kauli za kihaini alitoa mwenyewe na wote tumezisikia, tuiachie Mahakama itoe maamuzi yake
 
Kwamba miaka 27 ndio SI Unit ya kukaa magereza? Au huko Africa Kusini walikaa Kimya na kuanza kudai Mandela aachiwe huru baada ya kufikisha miaka 27 jela? Ama ni mimi sielewi unaongea ukhanithi gani?
Na nyinyi ndiyo mmewapeleka Kenya akina Twaha, Maria Sarungi, Rose Mayemba kwa ajili ya kufanya mpambano kwenye kambi za wakimbizi? Sawa
 
Unaishi kwa kukalili watanzania wa Leo sio wale Lyatonga Mrema na mtikila
Kumjibu mtu ambaye hajui tofauti ya "r" na "l"ni kichefuchefu. Siyo "kukalili" bali ni "kukariri". JF inaruhusu hata mabwege wa comment
 
Kama ulishangilia WaTanzania kuuliwa, utakuwa na lipi jipya kuhusu kudhalilishwa kwa waTanzania?

Wewe umejipambanua kwelikweli kuwa adui wa taifa hili; pamoja na huyo mhalifu Samia Suluhu Hassan mfugaji wako.
Taarifa ni moja tu kwenu: Hamponi.
Sasa watu walikuwa wanachoma vituo vya mafuta, wanachoma vituo vya Polisi, Mahakama, TRA na mabasi ya Mwendokasi!! Walikuwa wanachoma mabasi ya watu binafsi, wanapora mali na wanajeruhi watu wenye alama ya wino wa kupiga kura, Je wewe ulitakaje? Waachiwe tu?
 
Ulimuuliza Mhalifu Samia anavyomgwaya Tundu Lissu? Kamzushia kesi ili asikutane naye kwenye kura;na kama hiyo haitoshi bado ikalazimu atangaziwe kura milioni 31 ambazo hazikuwepo.
Na bado huoni aibu kila siku kuja humu JF kujaza uchafu tu wa mtu ambaye waTanzania hawamtaki!

Jiandae kuhamia kwa wajomba; kwa sababu Tundu Lissu hazuiliki tena.
Mkamia maji hayanywi
 
Hakuna uonevu kwa suala la Tundu. Kauli za kihaini alitoa mwenyewe na wote tumezisikia, tuiachie Mahakama itoe maamuzi yake
Tangu lini kauli imekuwa kitendo? Ingekuwa hivyo jela zingejaa watu walioitakia mabaya wapinzani na viongozi wao! Watu wametamba hadharani kuwa walikuwa sehemu ya vikundi vya kuwashughulikia wapinzani na hawakufanywa kitu. Watu wamesema hadharani kuwa safari ijayo watawachoma sindano za sumu hawakufanywa kitu ingawa hiyo ni kukiri kuwa walihusika katika jaribio la mwanzo. Watu wamepigwa picha wakimpiga tofali la kichwa mwanachama wa Chadema lakini mko kimya.

Kusema kuwa atakinukisha sio uhaini. Labda alikusudia watu wake wapasue mayai viza wakati wa uchaguzi. Kuwataka watu wasishiriki katika uchaguzi sio uhaini kwa sababu kupiga kura sio mandatory. Kusema kuwa watahakikisha uchaguzi haufanyiki sio uhaini maana kuna njia za kuzuia uchaguzi bila kufanya fujo. Kuna kuomba Mahakama izuie. Kuna kuwataka watu wasipige kura. Kuna civic disobedience. Yote hayo sio uhaini.

Mwisho, hivi kweli mnataka kumnyonga Lissu kwa kauli ya kukinukisha? Inasikitisha sana.

Amandla...
 
Umeambiwa alitakiwa kufanyiwa check up, sio kupewa tiba mpya. Hizo check up zingethibitisha tu kuwa hali yake si mbaya sana. Lakini inaweza kugeuka wakati wowote kama kuna matatizo ambayo yangegunduliwa wakati wa check up.

Mbona watu wa aina hiyo wako wengi. Mmojawapo ni Rugemarila wa IPTL alikataa plea bargaining ya mchongo na kusema heri aendelee kukaa rumande kuliko kukiri kosa ambalo hakufanya. Mwisho wa siku walimuachia.
Mandela alipasua mawe kwa miaka 27. Si ajabu kwa mtu anayeamini katika wito wake kukataa kutoka rumande kwa masharti yanayopingana na msimamo wake.
Lissu hafurahii kukaa rumande lakini anakubali kuwa hiyo ni gharama ya msimamo wake na yuko tayari kuilipia. Kitu kilichokuwa wazi ni kuwa iko siku watamuachia au atafia mikononi mwao.

Hayo ya bangi yameingiaje?

Amandla...

Huyo Stuxnet ni mvuta bangi ambaye hafanyi lolote analoamini ni gumu bila ya kuvuta bangi. Hivyo anaamini watu wote wapo kama yeye mvuta bangi. Just ignore this brain paralyzed creature called Stuxnet.
 
Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda huyu kiumbe ili ifikapo 2030 aweze kutukomboa Watanganyika tuliolala fofofo, kutoka mikononi mwa hawa wahuni.
2030 ingewezekana kama Chadema wangeshiriki uchaguzi wa 2025 ili utabiri wangu huu Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika! utimie!.

But its very unfortunate Chadema happed to be too blind to see fursa ya 2025, hivyo they have missed the chance of clinching the trophy of 2030

Kwa uchaguzi wa 2030, licha ya kufanyika chini ya katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, lakini mshindi wa kiti cha urais ni CCM, na bahati nzuri mimi tayari namjua ni nani Trends Reading: Japo Rais wa 2030 Namjua, Simtaji ili Kumlinda!. Be The First to Know Good News Kawe-2030, MB.ni Mwanamke!, Kawe Itapaa kwa Maendeleo!

I feel very sorry for Chadema kukosa hili bonge la fursa la ule uchaguzi wa 2025
Ila kama ni kuwasaidia, tumewasaidia sana kwa ushauri kupitia maandishi mengi tuu humu

p
 
Tangu lini kauli imekuwa kitendo? Ingekuwa hivyo jela zingejaa watu walioitakia mabaya wapinzani na viongozi wao! Watu wametamba hadharani kuwa walikuwa sehemu ya vikundi vya kuwashughulikia wapinzani na hawakufanywa kitu. Watu wamesema hadharani kuwa safari ijayo watawachoma sindano za sumu hawakufanywa kitu ingawa hiyo ni kukiri kuwa walihusika katika jaribio la mwanzo. Watu wamepigwa picha wakimpiga tofali la kichwa mwanachama wa Chadema lakini mko kimya.

Kusema kuwa atakinukisha sio uhaini. Labda alikusudia watu wake wapasue mayai viza wakati wa uchaguzi. Kuwataka watu wasishiriki katika uchaguzi sio uhaini kwa sababu kupiga kura sio mandatory. Kusema kuwa watahakikisha uchaguzi haufanyiki sio uhaini maana kuna njia za kuzuia uchaguzi bila kufanya fujo. Kuna kuomba Mahakama izuie. Kuna kuwataka watu wasipige kura. Kuna civic disobedience. Yote hayo sio uhaini.

Mwisho, hivi kweli mnataka kumnyonga Lissu kwa kauli ya kukinukisha? Inasikitisha sana.

Amandla...
Kwani hukuona vikundi vya wahuni vikichoma vituo vya kupigia kura tarehe 29/10? Aliyoyasema yalitokea kweli
 
Hapa kuna contradiction kubwa sana, waswahili wanasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu. Heche hana kumbukumbu.

Anasema Lissu hali yake kiafya ni mbaya sana na familia wanathibitisha kuwa anapaswa kufanya checkup kila baada ya miezi 3. Halafu anadai kuwa kuna watu wamemfuata kuwa akubali masharti ili aachiwe, ila Tundu amekataa.

Yawezekana checkup ya miezi 3 ni uwongo kwa vile Tundu sasa anamalizai vipande 4 vya miezi mitatu mitatu bila checkup. Angekuwa mtu wa checkup halafu kakosa 2 tu basi hali yake ingekuwa HOVYO au tete.

Pili, hakuna binadamu ana furahi kukaa Rumande hasa kwa mazingira kama aliyopo Tundu. Siamini kwa sasa hivi kama Tundu anaweza kukataa masharti yeyote ya kuwa huru, especially kwa assumption ya kwanza kuwa anaumwa.

Heche ni MWONGO, hizo ni FIKRA zake mbaya baada ya kuvuta bangi kutoka kwa Walenchoka
Lissu sio nyanya kama wewe.
Usimuuzie woga wa kijinga kama huo.
Angekuwa mwoga asingerudi Nchini baada ya kupigwa risasi.
 
Kwani hukuona vikundi vya wahuni vikichoma vituo vya kupigia kura tarehe 29/10? Aliyoyasema yalitokea kweli
Una hotuba yeyote ya Lissu akiwataka wafuasi wake wachome vituo vya kupigia kura? Yeye alisema uchaguzi hautafanyika. Haukufanyika?
Na tangu lini kuchoma kituo cha kupigia kura imekua uhaini? Inakuwaje uone sawa wachoma kituo wauawe lakini wale wanaojaza kura katika maboksi ya kupigia kura wasifanywe kitu?

Amandla...
 
Back
Top Bottom