PostGE2025 John Heche: Walitufuata na kutupa masharti ili Lissu aachiliwe, tumekataa kuwapigia magoti

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Sasa watu walikuwa wanachoma vituo vya mafuta, wanachoma vituo vya Polisi, Mahakama, TRA na mabasi ya Mwendokasi!! Walikuwa wanachoma mabasi ya watu binafsi, wanapora mali na wanajeruhi watu wenye alama ya wino wa kupiga kura, Je wewe ulitakaje? Waachiwe tu?
Ila waliojitangaza kwa kura 31m za uongo wao ndio walitakiwa kuachiwa.
 
Kuchoma vituo vya Polisi ni uhaini usiopaswa kuvumiliwa na dawa yao ni shaba tu.Baada ya kupigwa shaba wanaotaka kufanya huo uhalifu imebidi wajiulize.
Maandamano ya kuchoma vituo vya kura,vya polisi,vya petroli havikubaliki.Hutaki kupiga kura ni haki yako lakini huna haki ya kunyima wengine kupiga kura kwa kufanya vitendo vya kihalifu.
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche amesema hali ya kiafya ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na mazingira yanayomkabili, ambaye amekuwa akishikiliwa kwa kile alichokiita "kesi ya uongo," amekosa vipindi muhimu vya uchunguzi wa afya yake (check-up) ambavyo vilipaswa kufanyika kila baada ya miezi mitatu.

"Nimeongea na familia yake mara kwa mara na amethibitisha kuwa anahitaji check-up ya afya yake kwa sababu hiyo ilikuwa ni utaratibu wa kila baada ya miezi mitatu anakwenda kufanyiwa check-up na kuhakikisha kwamba afya yake inaendelea kuwa imara. Sasa ni miezi 12, kwa maana hiyo amevuka check-up nne ambazo alipaswa kufanya katika kipindi cha mwaka mmoja ambao anashikiliwa kwa kesi ya uongo."

Heche ameendelea kueleza kuwa Lissu amekuwa akikabiliwa na shinikizo la kukubali masharti fulani ili aachiwe huru, lakini ameyakataa katakata.

"Lissu, pamoja na kupita magumu yote haya, amekataa kuwapigia magoti hawa wadhalimu... wamejaribu kuweka masharti ambayo sisi tumeyakataa. Mojawapo ya masharti hayo ni kwamba Lissu akubali kuachiliwa lakini aache kufanya siasa ndani ya nchi, aache kuwatetea Watanzania, aondoke akakae nje ya nchi. Lissu amekataa."

SIKU 365 ZA TUNDU ANTIPAS LISSU KUWA KIZUIZINI BILA KUHUKUMIWA NA MAHAKAMA

John Heche makamu mwenyekiti CHADEMA taifa, Amani Golugwa naibu katibu mkuu CHADEMA , Edwin Sifuna Katibu mkuu wa ODM chama cha kisiasa nchini Kenya wazungumzia hali hiyo isiyo na afya kwa siasa za Tanzanis

View: https://m.youtube.com/watch?v=1rt9GAU3R4U

1775829694827.jpeg
 
Hapa kuna contradiction kubwa sana, waswahili wanasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu. Heche hana kumbukumbu.

Anasema Lissu hali yake kiafya ni mbaya sana na familia wanathibitisha kuwa anapaswa kufanya checkup kila baada ya miezi 3. Halafu anadai kuwa kuna watu wamemfuata kuwa akubali masharti ili aachiwe, ila Tundu amekataa.

Yawezekana checkup ya miezi 3 ni uwongo kwa vile Tundu sasa anamalizai vipande 4 vya miezi mitatu mitatu bila checkup. Angekuwa mtu wa checkup halafu kakosa 2 tu basi hali yake ingekuwa HOVYO au tete.

Pili, hakuna binadamu ana furahi kukaa Rumande hasa kwa mazingira kama aliyopo Tundu. Siamini kwa sasa hivi kama Tundu anaweza kukataa masharti yeyote ya kuwa huru, especially kwa assumption ya kwanza kuwa anaumwa.

Heche ni MWONGO, hizo ni FIKRA zake mbaya baada ya kuvuta bangi kutoka kwa Walenchoka
UWONGO wa Heche hapo ni upi?
Nani asiyejua Lissu kuwa ni Mgonjwa/Mlemavu.
Watu kama wewe ndio sign Wazungu wanatumia kutuona watu weusi tuna Laana.
Lissu kuwa Gerezani wewe Dagaa Mchele unanufaika na nini? Au fuata Mkumbo wenzako wanakula maisha for the serenity.
Humanity must be prevailed & protected, hofu yangu mambo yanabadilika haraka yasije yakaja upande wako na wewe ukawa kwenye Mkondo wa Mateso.
 
SIKU 365 ZA TUNDU ANTIPAS LISSU KUWA KIZUIZINI BILA KUHUKUMIWA NA MAHAKAMA

John Heche makamu mwenyekiti CHADEMA taifa, Amani Golugwa naibu katibu mkuu CHADEMA , Edwin Sifuna Katibu mkuu wa ODM chama cha kisiasa nchini Kenya wazungumzia hali hiyo isiyo na afya kwa siasa za Tanzanis

View: https://m.youtube.com/watch?v=1rt9GAU3R4U

MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA KUZUIWA KIZUIZINI TUNDU ANTIPAS LISSU, LEO ATIMIZA SIKU 365 GEREZANI
Edwin Sifuna katibu mkuu wa ODM chama cha siasa nchini Kenya

View: https://m.youtube.com/watch?v=miw2TClHwZM
 
08 April 2026

365 days of Tundu Antipas Lissu in prison — ODM Kenya's secretary general Edwin Sifuna to intervene

View: https://m.youtube.com/watch?v=Ll4klLvdb1o

CHADEMA party chairperson Tundu Lissu was arrested on April 9, 2025, after a rally in Mbinga, Songea region of Tanzania. The 57-year-old CHADEMA chairman faces treason charges — carrying the death penalty — for speeches and posts in the 'No Reforms, No Elections' campaign. His trial in Dar es Salaam before Tanzania High court has faced questionable court adjournments, several temporary postponement, a number of suspensions of a legal proceeding to a future date and time and bad enough indefinitely (sine die) postponement , solitary confinement in the death row section for the Condemned prisoners who are death row inmates. And a UN ruling in February 2026 declaring his detention arbitrary and demanding release. Supporters mark the anniversary with #FreeTunduLissu calls, while authorities defend the charges as protecting public order amid opposition crackdowns and stalled constitutional reforms.
1775829526914.jpeg
 
Hapa kuna contradiction kubwa sana, waswahili wanasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu. Heche hana kumbukumbu.

Anasema Lissu hali yake kiafya ni mbaya sana na familia wanathibitisha kuwa anapaswa kufanya checkup kila baada ya miezi 3. Halafu anadai kuwa kuna watu wamemfuata kuwa akubali masharti ili aachiwe, ila Tundu amekataa.

Yawezekana checkup ya miezi 3 ni uwongo kwa vile Tundu sasa anamalizai vipande 4 vya miezi mitatu mitatu bila checkup. Angekuwa mtu wa checkup halafu kakosa 2 tu basi hali yake ingekuwa HOVYO au tete.

Pili, hakuna binadamu ana furahi kukaa Rumande hasa kwa mazingira kama aliyopo Tundu. Siamini kwa sasa hivi kama Tundu anaweza kukataa masharti yeyote ya kuwa huru, especially kwa assumption ya kwanza kuwa anaumwa.

Heche ni MWONGO, hizo ni FIKRA zake mbaya baada ya kuvuta bangi kutoka kwa Walenchoka
Wewe umejaaliwa kipaji Cha ujinga. Ukiambiwa ndugu ndiyo waliompa taarifa heche. Kwa ujinga unakanusha kama vile wewe ni ndugu wa lisu?
Unafikiri Kila mtu ananunulika kirahisi kama wewe? Mwenzio kapigwa risasi na aliyempiga anajulikana ulishawahi sikia akiogopa?
Ukisikia chochote Toka chadema wewe masikio yanakusimama kama ndezi?
 
Sasa watu walikuwa wanachoma vituo vya mafuta, wanachoma vituo vya Polisi, Mahakama, TRA na mabasi ya Mwendokasi!! Walikuwa wanachoma mabasi ya watu binafsi, wanapora mali na wanajeruhi watu wenye alama ya wino wa kupiga kura, Je wewe ulitakaje? Waachiwe tu?
Kwa nini wewe unataka mtu (samia) aliyesababisha yote hayo aachwe. Huna hata akili ndogo tu ya kukuongoza kutambua hilo?
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche amesema hali ya kiafya ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na mazingira yanayomkabili, ambaye amekuwa akishikiliwa kwa kile alichokiita "kesi ya uongo," amekosa vipindi muhimu vya uchunguzi wa afya yake (check-up) ambavyo vilipaswa kufanyika kila baada ya miezi mitatu.

"Nimeongea na familia yake mara kwa mara na amethibitisha kuwa anahitaji check-up ya afya yake kwa sababu hiyo ilikuwa ni utaratibu wa kila baada ya miezi mitatu anakwenda kufanyiwa check-up na kuhakikisha kwamba afya yake inaendelea kuwa imara. Sasa ni miezi 12, kwa maana hiyo amevuka check-up nne ambazo alipaswa kufanya katika kipindi cha mwaka mmoja ambao anashikiliwa kwa kesi ya uongo."

Heche ameendelea kueleza kuwa Lissu amekuwa akikabiliwa na shinikizo la kukubali masharti fulani ili aachiwe huru, lakini ameyakataa katakata.

"Lissu, pamoja na kupita magumu yote haya, amekataa kuwapigia magoti hawa wadhalimu... wamejaribu kuweka masharti ambayo sisi tumeyakataa. Mojawapo ya masharti hayo ni kwamba Lissu akubali kuachiliwa lakini aache kufanya siasa ndani ya nchi, aache kuwatetea Watanzania, aondoke akakae nje ya nchi. Lissu amekataa."

Kumuenzi na kuadhimisha siku 365 wa kuwekwa kizuizini kama mfungwa wa kisiasa, # Jasusi TV imetengeneza wimbo na video yake, maalum kwa ajili ya maadhimisho ya mwaka mmoja wa mwenyekiti wa Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu

View: https://m.youtube.com/watch?v=85bP-YM4ynQ
 
2030 ingewezekana kama Chadema wangeshiriki uchaguzi wa 2025 ili utabiri wangu huu Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika! utimie!.

But its very unfortunate Chadema happed to be too blind to see fursa ya 2025, hivyo they have missed the chance of clinching the trophy of 2030

Kwa uchaguzi wa 2030, licha ya kufanyika chini ya katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, lakini mshindi wa kiti cha urais ni CCM, na bahati nzuri mimi tayari namjua ni nani Trends Reading: Japo Rais wa 2030 Namjua, Simtaji ili Kumlinda!. Be The First to Know Good News Kawe-2030, MB.ni Mwanamke!, Kawe Itapaa kwa Maendeleo!

I feel very sorry for Chadema kukosa hili bonge la fursa la ule uchaguzi wa 2025
Ila kama ni kuwasaidia, tumewasaidia sana kwa ushauri kupitia maandishi mengi tuu humu

p
Unazeeka vibaya wewe babu ,,,kila siku zinvyokimbia na akili nayo inakimbia.
 
Mara hii wamekalia kuti kavu ama unaweza kusema wameyatimba!, ingekuwa lissu naweza kumfananisha na mnyama basi nisingejisumbua kumfananisha na wanyama wakubwa wenye sifa kedekede!. lissu anasifa ya mnyama "NYEGERE" huyu mnyama ni king'ang'a haswa hana masihara kwenye jambo lake, huyu mnyama ni kiboko ya nyuki, nyoka n.k
vipimo vyake vya wivu na hasira hakuna mzani unapima!..View attachment 3569949
Honey badger dont give a f…k, small but agile and fearless.
 
Hapa kuna contradiction kubwa sana, waswahili wanasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu. Heche hana kumbukumbu.

Anasema Lissu hali yake kiafya ni mbaya sana na familia wanathibitisha kuwa anapaswa kufanya checkup kila baada ya miezi 3. Halafu anadai kuwa kuna watu wamemfuata kuwa akubali masharti ili aachiwe, ila Tundu amekataa.

Yawezekana checkup ya miezi 3 ni uwongo kwa vile Tundu sasa anamalizai vipande 4 vya miezi mitatu mitatu bila checkup. Angekuwa mtu wa checkup halafu kakosa 2 tu basi hali yake ingekuwa HOVYO au tete.

Pili, hakuna binadamu ana furahi kukaa Rumande hasa kwa mazingira kama aliyopo Tundu. Siamini kwa sasa hivi kama Tundu anaweza kukataa masharti yeyote ya kuwa huru, especially kwa assumption ya kwanza kuwa anaumwa.

Heche ni MWONGO, hizo ni FIKRA zake mbaya baada ya kuvuta bangi kutoka kwa Walenchoka
Kwa hizo akili huwezi kumuelewa John Heche!
 
Una hotuba yeyote ya Lissu akiwataka wafuasi wake wachome vituo vya kupigia kura? Yeye alisema uchaguzi hautafanyika. Haukufanyika?
Na tangu lini kuchoma kituo cha kupigia kura imekua uhaini? Inakuwaje uone sawa wachoma kituo wauawe lakini wale wanaojaza kura katika maboksi ya kupigia kura wasifanywe kitu?

Amandla...
Whether ni uhaini au siyo uhaini tutajuwa siku ya hukumu.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
SIKU 365 ZA TUNDU ANTIPAS LISSU KUWA KIZUIZINI BILA KUHUKUMIWA NA MAHAKAMA

John Heche makamu mwenyekiti CHADEMA taifa, Amani Golugwa naibu katibu mkuu CHADEMA , Edwin Sifuna Katibu mkuu wa ODM chama cha kisiasa nchini Kenya wazungumzia hali hiyo isiyo na afya kwa siasa za Tanzanis

View: https://m.youtube.com/watch?v=1rt9GAU3R4U

View attachment 3570585

Huyu sasa ndiyo anastahili kuwa Rais wa nchi! Kwanza ameenda shule, ni mzalendo wa kweli, mpambanaji, na siku zoye huwa anasimamia kile anacho kiamini. Mtu wa aina hii huwezi kumlinganisha na muimba taarab aliyesoma elimu ya hapa na pale.
 
Hapa kuna contradiction kubwa sana, waswahili wanasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu. Heche hana kumbukumbu.

Anasema Lissu hali yake kiafya ni mbaya sana na familia wanathibitisha kuwa anapaswa kufanya checkup kila baada ya miezi 3. Halafu anadai kuwa kuna watu wamemfuata kuwa akubali masharti ili aachiwe, ila Tundu amekataa.

Yawezekana checkup ya miezi 3 ni uwongo kwa vile Tundu sasa anamalizai vipande 4 vya miezi mitatu mitatu bila checkup. Angekuwa mtu wa checkup halafu kakosa 2 tu basi hali yake ingekuwa HOVYO au tete.

Pili, hakuna binadamu ana furahi kukaa Rumande hasa kwa mazingira kama aliyopo Tundu. Siamini kwa sasa hivi kama Tundu anaweza kukataa masharti yeyote ya kuwa huru, especially kwa assumption ya kwanza kuwa anaumwa.

Heche ni MWONGO, hizo ni FIKRA zake mbaya baada ya kuvuta bangi kutoka kwa Walenchoka
Wewe kweli hamnazo

Kwa ishu ya kuachiwa kwa masharti hayo, wewe "unafikiri tu" lakini wenzio wana "reality" in their hands

===Unachokataa na kubishia ni nini hasa wakati wenzio (watoa hoja) top officials wa CHADEMA Heche, John Mnyika na wenzao wanathibitisha kufuatwa kupewa masharti yaliyo nje ya utaratibu wa kimahakama (kumbuka kesi Iko mahakamani) ili mwenyekiti wao aachiliwe?

===Unachokataa na kubishia ni nini wakati wenzako wanathibitisha pasipo shaka kuwa Tundu Lissu mwenyewe kawaambia kuwa wameshamfuata mara kadhaa gerezani kumpa masharti ili huyu mwanamke (Samia) mshenzi na muuaji eti ili amsamehe na kumwachia?

##Tundu Lissu alimwambia kitu kimoja tu: Wewe Samia unanisamehe mimi Tundu Lissu kwa kosa gani? Kama unataka jambo hili liishe salama, tumia mlango huu huu wa mahakama uliotuma watu wako kunishitaki kwa kesi ya uongo kuifuta ili dunia na kila mtu aone kama walivyoona wakati unanileta mahakamani kwa mbwembwe na kuanza kunishitaki.

===Ndugu Stuxnet Tundu Lissu hawawezi kumpata kwa kutumia "FREEMAN MBOWE STYLE EXIT" mwaka 2021 walipompachika kesi ya uongo ya ugaidi. Huyu huyu mwanamke mshenzi na muuaji akamtolea mlango wa nyuma ya mahakama, kinyume cha sheria. Na kwa sbb ya ulafi wa pesa (kulambushwa asali) wa Freeman MBOWE, tukio hilo liliharibu kabisa heshima yake aliyojijengea miaka mingi ktk siasa za Tanzania na linamgharimu mpaka leo, na litamgharimu mpaka kesho!!

===Na kwa taarifa yako, tuwaambie sasa kuwa, si tu masharti hayo aliyoyasema Heche. Pia, deal hilo linaambatana na hongo kubwa ya fedha na nyadhifa za madaraka serikalini kwa baadhi ya viongozi akiwemo Heche, John Mnyika na wengine iwapo CHADEMA watakubali masharti hayo. Lengo kuu likiwa ni kuua nguvu ya CHADEMA forever kama ilivyowahi kufanyika kwa vyama vingine kama NCCR MAGEUZI, UDP na CUF. Ni bahati njema kuwa CHADEMA hii ina viongozi madhubuti kwelikweli waliokataa kuuza utu na heshima yao kwa vipande vya fedha. Na hii inatengua usemi ule kuwa "hakuna mkate magumu kwa chai" na sasa twaweza kusema bila shaka kuwa "ipo mikate migumu kwa chai" na mmojawapo ni CHADEMA ya Tundu Lissu!!

👉👉Mimi nilidhani utakuwa na akili ya kumtaka aende mbele zaidi awataje na watu wa Samia waliowafuata kuwapelekea hilo deal 🤝 lakini cha ajabu umeamua kubisha kijuha na kilevi tu

Ndugu Stuxnet, kwenye uchafu huu uliosemwa na John Heche, yapo mengi ya kusema yakiwa na ushahidi madhubuti lakini si wakati wake sasa. When the right time comes, we will spit all. Kwa sasa ni kupambana mwenyekiti atoke gerezani and get assured kuwa, as for now they have no other option isipokuwa kumwachia mwenyekiti wetu VERY SOON KWA MASHARTI YAKE NA SIO KWA MASHARTI YAO!!
 
Back
Top Bottom