Habari kutoka ndani ya chama jimbo la Kibamba zinasema mbunge wa sasa wa Kibamba Mheshimiwa John John Mnyika ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA mpaka muda wa kuchukua fomu unaisha alikuwa hajachukua fomu ya kutetea kiti hicho.
Kama hizi habari ni za kweli je ni nini sababu? Ametosheka au anajipa muda wa kuitumikia nafasi ya katibu mkuu?
====
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema hatogombea ubunge katika uchaguzi ujao ili apate muda zaidi wa kushughulikia masuala ya uongozi wa chama, waweze kupata ushindi. Mnyika amekuwa mbunge kwa vipindi viwili akiwakilisha Jimbo la Ubungo (2010-2015) na Kibamba (2015-2020).
POLITICS: CHADEMA's SG, John Mnyika, has declared that he will not run for any political position, including a Member of Parliament position, in this year's general election.
Mnyika has been a Legislator for the past 10 years, currently is the MP of Kibamba Constituency in Dar.
Ni kwamba mnyika amesoma alama za nyakati, anajua kabisa hawezi kupata, ndomana aliacha kabisa kufanya mikitano, kukutana na wananchi achilia mbali kutembelea japo maeneo ya Jimbo lake alijua hatagombea tena
Ni vyema sana kama ni kweli. Maoni yetu wananchi kwenye rasimu ya Warioba tulitaka mwisho wa ubunge iwe 10yrs. Ni vyema cdm wangeanza kutekeleza hili kwa vitendo lingeleta maana zaidi.
Mbona hili alilisema tangia mwezi december mwaka jana? Inshaalah na mimi nitakuwa mjengoni mwezi Novemba maana hakuna wakunishinda ndani ya CCM. Tutawapiga washangae