John Malecela: Sioni Hoja ya Wanaopinga Uwekezaji wa DP World Bandarini

Nikikumbuka kisa cha Malecela cha miaka ya mwanzoni mwa miaka ya 1990 wakati Melecela bado akiwa waziri mkuu, kisa cha kununuliwa na waarabu ili kuuza nchi yake kisha kubadili dini kutoka kuwa mkristo ili awe muislamu, kisa aliahidiwa kuwezeshwa kuwa rais wa Tanzania (Tanganyika?) kirahisi, huwa ninacheka na kusikitika sana. Kwa hii kauli yake ya sasa kuhusu Dp world wala sishangai, maana historia inaonyesha Malecela ni dalali mkongwe wa kuuza nchi.

Poor Malecela!
 
Huyu mzee ni mwanasiasa aachwe tu,wazee wanaoliona hili jambo kwa macho matatu mmoja wapo ni Joseph Sinde Warioba,taalauma yake ya sheria inampa mwanga zaidi
 
Mtu ambaye hajawahi kusema hapana, ndiyo yake haina nguvu wala maana yoyote.
 
Mzee kasema ukweli! Wengi wanasumbuliwa na chuki, wivu na udini tu. Hawana hoja kabisa wachache makuwadi wa wakenya wanaotaka bandari zetu zisiwe vizuri
 
Kwenye hayo mahojiano yeye ametoa hoja gani ya kuunga mkono? Nauliza tu lakini
 
Huenda anajua zaidi kuliko sisi (sina uhakika Nadhani Mrs wake yupo kati ya wale waliokwenda Dubai) Hence he might know what we don't....

Issue kubwa huenda ni transparency na kuhusisha watu kila kitu kiwe wazi (ukizingatia tumeumizwa mara ngapi, ukiumwa na nyoka hata unyasi utakutisha)...,
Once Bitten Twice Shy...

Anyway badala ya kushangaa watu wanaopinga angepinga vipengele wanavyopinga kama ni vya kweli au wanapotosha na kama hawapotoshi ni vipi vinafaa au havifai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…