John Malecela: Sioni Hoja ya Wanaopinga Uwekezaji wa DP World Bandarini

Huyu mzee tumsamehe bure; atakuwa kachanganyikiwa.
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 

 
Huyu mzee si alibadili dini kwa siri akatska kuuza nchi Nyerere akamuwahi?
Hana moral authority kwa jamii aendelee kula mafao
 
Kwa mafao unayokula mzee huwezi kuwa kinyume na serikali maana huwezi kuukata mkono unaokulisha,tumekuelewa dingi wetu.
 
Huyu si ndo alibadil Dini kuwa muislamu Ili mradi awe Raisi...siyo wazee wote Wana busara..
HuwezI ukaenda Msoga kupata ushauri afu urudi na kitu cha Maana
Ndio maana Akasema wanaopinga Hawana hoja... Kama maelezo yenyewe ndio haya basi Yuko sawa
 
Want a pinga wengi hoja zao siyo uwekezaji bali aina ya Mkataba au makubaliano yalivyo. Mzee ajue hilo.
Ndio maana Mzee anasema wanaopinga Hawana Hoja. Mikataba ya Makubaliano ya Uendeshaji hayajawekwa. Bado hamuelewi.
 
Mzee kaa kwa kutulia,tunza heshima yako tafadhali.Tuache Watanganyika tuipambanie nchi yetu dhidi ya waarabu na wazanzibari.
 
Uzee kwa kweli ni changamoto. Nilimpeleka Baba yangu shambani nikamwambie hizi ni hekari 6 yeye kakomaa ni 3 Tu hizi. Yaani nikamind lkn ikabidi nitulie.

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kiwanda kilitoka dom kwenye zabibu kikaenda mbeya kwenye viazi? [emoji2][emoji2][emoji2] Anhaa manina Hii Nchi
 
Umeanza kunifahamu lini? Leo hii nimegeuka kuwa mwanadawati wa makumbusho?

Ndo mana tukisema hamuna hoja hatukosei kweli maana nyie pinga pinga wote mmejaa ujinga ujinga tu
I'm critical thinker, ukiona napinga ujue Nina sababu za msingi kabisa za kufanya hivyo. Penye kuunga mkono napo pia nimekuwa nikifanya hivyo ninapokuwa na sababu za msingi pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…