John Mnyika ateuliwa kuwa Katibu Mkuu CHADEMA Taifa, Benson Kigaila-NKM Bara na Salum Mwalimu NKM Zanzibar

WanaJF Salaam

Ni siku nyingine muhimu kabisa katika historia ya chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA.

Baraza Kuu jipya la Chadema linakutana leo maalum kuichagua sekretariati mpya ya chama hicho itakayokivusha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho Mwenyekiti wa Taifa atapaswa kupendekeza majina kwa nafasi tatu za Katibu Mkuu na Manaibu wake wawili wa Tanganyika na Zanzibar.Kisha Baraza Kuu litapigia kura mapendekezo ya Mwenyekiti na kuwachagua rasmi watendaji hao.

Kwa sasa habari kuu hapa katika viwanja vya Mlimani City ni kuhusu jina la Katibu Mkuu mpya.Huku majina kadhaa yakitajwa na wajumbe kwa kubashiri.

Majina yaliyoko vinywani vya wajumbe na kuonekana kutajwa sana ni John Mnyika,John Heche,Salum Mwalim,Lazaro Nyalandu na Vicent Mashinji ambaye ni Katibu Mkuu anayemaliza muda wake.

Tunatarajia kuwaletea taarifa kamili ya uteuzi utakaofanywa na Mwenyekiti na tunawaahidi wasomaji wetu wa Jamii Forum kuwa wa kwanza kupata taarifa.

Asanteni sana
Wasalaam
Molemo wa JF

Updates Saa 11 Alfajiri - 20.12.2019

Freeman Aikael Mbowe Mwenyekiti wa chama Taifa amemteua John John Mnyika kuwa Katibu Mkuu Chadema

Pia Mbowe amewateua Benson Kigaila kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara na Salum Mwalimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar

Katika uteuzi mwingine Kiongozi huyo mkuu wa Chadema amemteua John Heche kuwa mjumbe wa Kamati Kuu

Baraza Kuu kwa kauli moja limeridhia uteuzi huu wa Mwenyekiti wa chama na shangwe zimetawala katika ukumbi huu wa Mlimani city.
JJ Mnyika hongera sana, hii ni heshima.kubwa kwako na kwa watanzania, Chadema mmetutendea mambo mazuri sisi watanzania wapenda maendeleo amani na demokrasia.

JJ mnyika.....hoyeeeeeeee!!.

Nimewaza JJM vs Bashiru....
.hahahaaa
 
Mnyika,Kigaila,Salum Mwalimu; wote watu wa field;wanajua operesheni zote za CDM. Mambo mpera mpera, Mbowe atakimbizwa balaa. Lissu anaweza kuachiwa kiti na Mbowe kabla ya miaka 5
 
Freeman Aikael Mbowe Mwenyekiti wa chama Taifa amemteua John John Mnyika kuwa Katibu Mkuu Chadema
Duh.. !, Duh...!, Duh...!.
Naomba hapa nisiseme kitu maana kauli huumba, nisije sema kitu halafu kikaja kutokea ikawa mimi niliyekisema nikawa ndiye nimekiumba!.

Ule ukimya wa JJ.MNYIKA mimi niliutafsiri kuwa tayari ameishajitambua na yuko njia kuu kusibiria tuu kuvunjwa kwa Bunge na kupokea zile milioni 100 za kila Mbunge kuagania, kisha ndipo atangaze ... sasa ndie Katibu Katibu Mkuu!.

Haya na tusubiri maana sisi wengine midomo yetu tukisema tuu kitu...

Anyway hongera sana JJ.Mnyika kuukwaa ukatibu Mkuu wa Chadema, sasa ni kama Dr. Slaa amerudi.
P
 
Molemo thread hii iendelee kuhusu kuteuliwa JJM kuwa katibu mkuu CDM,badala ya kuanzisha nyingine. Ongezea kwenye heading kuwa amepatikana..... Naona Nanyaro Ephata ameanzisha nyingine. Iunganishwe ili tufuatilie vizuri
 
Muda utasema! Wengi walidhani km ulivyodhani ww...

Muda tuu ndio utakao toa jibu sahihi
 
Do
Duh.. !, Duh...!, Duh...!.
Naomba hapa nisiseme kitu maana kauli huumba, nisije sema kitu halafu kikaja kutokea ikawa mimi niliyekisema nikawa ndiye nimekiumba!.

Ule ukimya wa JJ.MNYIKA mimi niliutafsiri kuwa tayari ameishajitambua na yuko njia kuu kusibiria tuu kuvunjwa kwa Bunge na kupokea zile milioni 100 za kila Mbunge kuagania, kisha ndipo atangaze ... sasa ndie Katibu Katibu Mkuu!.

Haya na tusubiri maana sisi wengine midomo yetu tukisema tuu kitu...

Anyway hongera sana JJ.Mnyika kuukwaa ukatibu Mkuu wa Chadema, sasa ni kama Dr. Slaa amerudi.
P
Dodoma waliondoka na akili zote za P!
 
Mbowe hawezi kumpa huyo hazipandi, atataka aweke mtu wa kumpelekapeleka.
 
Molemo thread hii iendelee kuhusu kuteuliwa JJM kuwa katibu mkuu CDM,badala ya kuanzisha nyingine. Ongezea kwenye heading kuwa amepatikana..... Naona Nanyaro Ephata ameanzisha nyingine. Iunganishwe ili tufuatilie vizuri
Nadhani Mods watatendea haki wazo lako zuri
 
JJ Mnyika hongera sana, hii ni heshima.kubwa kwako na kwa watanzania, Chadema mmetutendea mambo mazuri sisi watanzania wapenda maendeleo amani na demokrasia.

JJ mnyika.....hoyeeeeeeee!!.

Nimewaza JJM vs Bashiru....
.hahahaaa
Kwa kweli Mnyika ni Heshima Kubwa kwa Chadema
 
Back
Top Bottom