John Mnyika ateuliwa kuwa Katibu Mkuu CHADEMA Taifa, Benson Kigaila-NKM Bara na Salum Mwalimu NKM Zanzibar

Acha kuonyesha ujinga wako hadharani! Fedha ya jimbo ni kiasi gani au unaropoka kwa sababu una mdomo?
hatakama ni mia tuambieni ziko wapi zimefanya nini? sijaona hata kisima kimoja wala wamama wakigawiwa cherehani
 

Acha ujinga huu toka lini mbunge akujengee zahanat na daraja kwani kodi anakusanya yeye? Kazi ya mbunge unaijua kwel na kuna mahali umeona Mnyika hajatimiza wajibu wake kama Mbunge?
 
hatakama ni mia tuambieni ziko wapi zimefanya nini? sijaona hata kisima kimoja wala wamama wakigawiwa cherehani
Haya amekula na kugawia familia yake. Umeridhika?
 
nina imani na J.Heche
Heche is overrated! Alipokuwa kiongozi Bavicha mlikuwa mnaponda style yake ya uongozi. Sijui kafanya nini sasa aonekane anafaa kwa nafasi hii kubwa.

Kwa viwango vyote hakuna mwanasiasa Chadema level za Mnyika. Kama Dr Slaa alifanikiwa au kushindwa kujenga vijana kisiasa basi Mnyika ndio top cream ya Dr Slaa.

Najua Mbowe amewinda nini kumuweka Mnyika pale ( 90% ni bridge to Catholic church ) then mengine yanafuata.

Binafsi kuna imani imerejea kidogo lakini Mnyika ana kazi kubwa hasa eneo la nidhamu. Kuna watu wameota sharubu kweli kweli. Dr Slaa alikuwa mkali na umri wake ulimpa nguvu ya hekima kudhibiti chama na kuweza kukemea yoyote.

Pia kulegea kwa intelijinsia ya chama kunahitaji kufanyiwa kazi sambamba na kurejesha siasa za hoja, kuaminiana, kuacha matusi kwa watu wenye hoja kinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kaka yangu Paskali Siku hizi umekuwa mbashiri ama msoma nyota na unataka watu wote wakuanini kwa usoma nyota wako. Lakini pia kwenye maandiko yako umekuwa too biased ambayo kwa mchambuzi unayejiita makini unapwaya. Tatu kama una hizo intelijensia unazosema unazo ambazo CHADEMA hawana angalau ungewapongeza kwa kumuondoa Mashinji ambaye alikuwa pandikizi.

Kwahiyo nadhani ungekuwa unatoa maoni yako kama mtu wa Mengi fulani not a neutral analyst ambaye hayuko neutral kiuhalisia.

Sasa kama tunaenda kwa hoja maybe tuanzie hapo. Hoja ipi tuijadili kama analysts tukiweka mahaba kanda kwanza ili pale unapozidiwa kwa hoja ukubali. Tatizo la kuchagua upande kabla huwa haikupi nafasi ya kuona positive kwenye upande mwingine


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Uko sahihi kwa mantiki ya kuwa iwapo cdm itakosa wawakilishi kutokana na siasa za kishenzi. Na kwa bahati mbaya paskali ww ni mmoja ya watu mnaoshabikia siasa za kihayawani.
Mkuu Tindo, ukiona mtu anatembea kwenye reli huku umesikia kingora cha treni inakuja, ukamwambia atagongwa, atakufa, na kweli treni ikampitia, ikamgonga, ikamua, jee kitendo cha kuripoti kabla kuwa atakufa na kweli akaja kufa, jee huko ndiko kushabikia kifo cha huyo jamaa?.

Chadema sio chama makini and it has never been serious even once!, kilizoea siasa za matukio na siasa za confrontation na majitaka. Alipoingia tuu hili jembe Magufuli, tukawaeleza humu kuwa this is a game changer, the political game has changed, there is no more room for mediocrity, now it's time for real politics.


Chadema hamkusikia, Lawrence Masha ndio mtu wa kwanza kuwaaga na akawaandikia kabisa waraka wa matatizo yenu

Mlipoanza kukimbiwa na viongozi na wanachama wenu, kuna kitu niliwaeleza humu


Mliposusia uchaguzi wa serikali za mitaa nikawauliza what did you wish to achieve?

Kwa vile mlifanyiwa figisu, akina sisi tukajitoa, tukabembeleza tukakubaliwa

Licha ya kusamehewa lakini bado mliendelea kuwaka mpira kwapani na matokeo yake

Nikatoa somo la matatizo yenu

Ndipo nikawashushia lawama hizi
Na kuwaeleza if you are not going to do the right thing, you're going to die.?

Sasa Chadema ikifa baada ya kuambulia patupu 2020 unaweza kunilaumu mimi kuwa nashabikia kifo cha kujitakia?.
P
 

Mzee unajua kazi ya mbunge? Kazi yake sio kukuletea maji na zahanati ila kusema bungeni ili serikali ifanye so hatumii hela zake za mfukoni. Lakini serikali imesema haipeleki walipochagua wapinzani kwahiyo usimlaumu kwa maendeleo kutokuja huko kwenu bali kwa serikali kutoleta maendeleo pamoja na kwamba wanalazimika kufanya hivyo. Lakini kama unahisi njia rahisi ni kuchagua CCM 2020 chagueni ili serikali ilete maana imejinasibisha hivyo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Paskali narudia tena, acha kushabikia siasa za kishenzi. Usitake kunionyesha kuwa hizo post zako ndio zimebeba mapungufu ya cdm, tofauti na huu uhayawani unaoendelea kwenye siasa za sasa. Kwa macho yangu nimeona wakati wa uchaguzi wa marudio wasimamizi wa cdm wakipigwa na polisi ili kujaza karatasi za matokeo ya kupika kuwa mgombea wa ccm kashinda. Nimeshuhudia kwa macho yangu wasimamizi wa uchaguzi wakifunga ofisi ili wagombea wa cdm wasirudishe fomu ili mgombea wa ccm apite bila kupingwa. Wengi tuliona tukio live likirushwa na ITV mabox ya kura yakitolewa vituoni kwenda kujazwa kura za ccm, na ITV wakatishiwa kuonyesha ushenzi ule.

Hayo matukio hapo juu ndio unaita siasa za kweli? Hivi majuzi wananchi wengi wamesusia kujiandikisha kupiga kura kutokana na siasa za kishenzi zinazoendelea hapa nchini, ambazo ww unaziita siasa za kweli. Acha kuleta mapost marefu na kuweka link kibao wakati tunaona fika kinachoendelea ni siasa za kipuuzi. Ona aibu bro kushabikia siasa za kishenzi. Hakuna cha game changer zaidi ya matumizi mabaya ya madaraka. Kama umeamua kushabikia hayo kwa masilahi yako binafsi sio tatizo, maana hamna mtu anakuzuia kupata, ila haya sio ya kushabikia.
 
Kama inakuuma chomoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anashabikia siasa za kihutu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…