Bongo tupo millioni 55+, watumishi wa umma ni Kama 500K, wanaofanya maamuzi nchi iende wapi, wanaotunga sera,wanaoweka vipaumbele, ijengwe zahanati au inunuliwe Ndege, ni Kama watu 1000
Sasa kwenye demokrasia,sie wananchi wa kawaida,cinabidi tuwe na uwezo wa kuwachagua, maana sie kwa Kodi zetu, ndio tunawalipa mishahara,sasa kwenye uchaguzi uliopita, hatukupewa nafasi.
Sasa hapo uhuru upo wapi, Kama unakula ugari kwa kuku,unaona mambo safi,kwa nini isiwe ule ugari na kuku, nje imepaki Vogue,na unaweza kuwalipia ada hata watoto wa ndugu zako?
Nani anasema hapo ulipo, ndio unastahili kuwepo?
Wakati huo huo,unajua maana ya kupigwa risasi 18,Tena mchana kweupeee.