John Mnyika, kuulalia mkeka uliochanika kunahitaji akili nyingi sana na sio nguvu

Unataka kumaanisha haki ya Mbowe itapatikana kwa huruma ya Rais na siyo kwa mujibu wa sheria? Yaani imefika mahala unataka watu waishi kwa hisani ya Rais? Kwamba utawala wa sheria umekufa?
Nyie ni watu wa aina gani? Kama wanataka kufuta kesi wafute kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria za bunge na siyo hisani ya Rais.
Tukiendelea na mawazo haya ya hisani ya Rais basi ujue hata wewe hauko salama. Utakamwatwa muda wowote atakaojisikia na atakuachia siku ukimpigia magoti bila kujali kuwa sheria zipo na zinafanya kazi
 
Umeongea maneno yenye busara na constructively
 
Halafu chadema sio chama kikuu cha upinzani kina kiti kimoja bungeni hakina kambi rasmi ya upinzani bungeni
 

Ni hivi, Mbowe lazima aachiwe, sio ombi bali ni lazima. Mkiendelea kumuweka ndani mnamuonea, mkimuachia mnamuogopa. Kama mlitegemea mtaombwa msamaha au kunyenyekewa basi mmeukalia. Hakuna mtu ana muda wa kujinyenyekeza kwa watawala majizi ya kura.
 

..kwanini mnataka Chadema wawapigie magoti ktk suala hili?

..hiyo busara inayohitajika kumuachia Mbowe kwanini iwe kwa upande wa Chadema peke yao?

..Je, CCM hawapaswi kuwa na busara, utu, na maadili, ili wasibambikie wapinzani kesi zisizo na msingi?

..Na matumizi mabaya ya madaraka kwa kuonea wapinzani hayatokani na kiburi cha watawala?
 
Inasikitisha kuona Kijana kuwa na akili mgando kwa kiwango hiki
 
Sijui kwanini viongozi hawajifunzi kuondoka kwa JPM kwamba duniani hatuna makao ya kudumu soon wataanza kuondoka kama alivyoondoka jpm. Who knew kwamba jpm pamoja na makeke yote ange expire so soon?
 
Wenye busara wote chadema walishaikimbia humo kuna watu wa wamihemuko ujuaji mwngi wacha walinywe kwa kua wamerikoroga wenyewe
 
Sio

Kwamba Hana makosa anayo
Sasa kama ana makosa Kwa nini unataka aachiwe? Kajumuike na Mazuzu wenzio msherehekee Kwa Amani maana ambaye angewakosesha Raha wakati wa sikukuu Yuko mahabusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…