Vijana wanaopiga kelele kuwa Mbowe asisamehewe ni wale wanaoshinda wanachangisha michango kwenye mitandao ya kijamii, kwa Wanachama na Wadau mbali mbali.
Shida Mbowe akitoka watapata wapi tena hela za kupiga? Biashara itakuwa imeisha.
Mbowe anatakiwa atoke hayo mengine wakapambane baadaye, Mnyika ashazidiwa na akina Tundu, Lema ambao nao wananufaika na biashara hii. Huu ni muda muafaka familia ya Mbowe kusimama kidete kuhakikisha mpendwa wao anatoka waache kusikiliza makelele ya wasaka tonge ambao sasa wanaenda kula keki mahakamani eti Mshikamano...NONSENSE...
Sugu aliwahi toka kwa msamaha wa Raisi, baadaye akafuata taratibu mahakama imsafishe..
Familia ya Mbowe hakikisheni mpendwa wenu anatoka kwa njia yeyote, only that ni muhimu kwa sasa hayo mengine baadaye.
Familia kumbukeni akina Lisu wanachokitakaa kesi ifike mwisho mnaweza kuja juta, kama mnajua kuna udhalimu je wakifika mwisho wakamfunga? Mtakuwa mmefaidika nini? Angalieni trend ya kesi inavyoenda, ni muhimu Familia mhakikishe kuwa mnasimama kidete mpendwa wenu anatoka, msimamo wenu kama familia ni muhimu sana kwa sasa, kumbukeni Mbowe ni kiongozi wa Chadema anazungukwa na watu wema, wanafiki, wanaokitaka cheo chake, wanaotaka kunufaika na kesi hii na wengine wengi sio kila ushauri mnaukubali..