John Mnyika, kuulalia mkeka uliochanika kunahitaji akili nyingi sana na sio nguvu

Umeandika mashudu matupu
 
Kuna watu hata mahabusu hawaijui ipoje lakini wanavyoshadadia Mwenyekiti aendelee kukaa ndani utashangaa.
 
Toa upuuzi tangu lini haki ikanunuliwa
 
Umeongea maneno yenye busara na constructively
Mkuu, hawa watu ndiyo wanatuumbia miungu watu kwenye ofisi za umma. Hatuwezi kuendelea kuishi kwa kutegemea huruma ya Rais.
Wamemtuhumu Mbowe kuwa ni gaidi na wamemfikisha mahakamani wakiamini kuwa wanao ishahidi wa kumtia hatiani. Sasa kwa nini wasiiache mahakama imtie hatiani na kumpa kifungo anachostahili au imkute hana hatia na kumuachia huru?
Madhara ya kutaka aachiwe kwa huruma ya Rais ni kwamba akija Rais mwingine atamkamata tena na kumshtaki maana mahakama haikutamka kwamba ana hatia au hana hatia. So atalazimika maisha yake yote kuishi kwa kutegemea huruma ya Rais
 
Hongera sana
 
Kuna wakati tuache ukweli usemwe na usemwe vizuri. CHADEMA wamekuwa wakitumia lugha zisizofaa dhidi ya polisi, majaji na mahakama kwa ujumla, bila kujua taasisi hizi zina watu na watu hao wana hisia, lakini pia wana mamlaka. Binfasi naamini kuwa lugha hizi ni moja ya sababu kubwa ndugu yetu Mbowe kuendelea kuwa mahabusu, kwa sababu kwa akili ya kawaidia ni vigumu kutegemea leo unamtukana jaji kisha kesho akufanyie wepesi.

Ni mawazo tu, sio lazima sote tuamini, ila mimi nayaamini. Merry Christmas
 
Muwape watu kesi za uongo halafu muabudiwe
 
Mbowe hahitaji msamaha kwakuwa hana kosa. Mbowe anahitaji kuachiwa awe huru na kujumuika na familia yake na wana CHADEMA.

That is simple and plain.

Haki huwa haiombwi mzee wangu huwa inatakiwa na kutolewa.
Kwa maana hiyo basi, Hanna haja ya kuloloma. Subirini kesi iishe ionekane hana hatia aachiwe huru au ana hatia apigwe mvua za kutosha.
 
Nakupinga vibaya sana !
 
Chadema wamepiga hatua kwenye kesi ya Mbowe kwa sbb saiz mazombie ya Lumumba yaliyoshangilia yy kupewa kesi ya kihuni wanataka aachiwe kihuni.Bahati nzuri mwamba wa uchagani ni mtu imara sana.Yanaweweseka hayalali yakimlazimisha mipango ili Mbowe aombe msamaha!Hata kama mkubwa hakosei kwenye hili hapana
 
Yaani saizi mazombie ya Lumumba yanahangaika Mbowe aachiwe kwa kuomba msamaha!!Kweli Tz inavivutio vingi vya maajabu hapo Lumumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…