John Mnyika: Watu wenye silaha wamemchukua Mwanachama wa CHADEMA, Mdude Nyagali (Mdude CHADEMA)

John Mnyika: Watu wenye silaha wamemchukua Mwanachama wa CHADEMA, Mdude Nyagali (Mdude CHADEMA)

Hili jambo litafika sehemu litazoereka kama wananchi hatuta badilika kwa hatma ya taifa letu hivi hawa ni akina nani nchi hii kama vipi wajitokeze waseme wako ndio akina nani na wanafanya hivi kwa maslahi ya nani
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nyakibimbili said:
Yana mwisho wake, nchi ni ardhi wenye ulafi nayo wataiacha pia[
And the buck stops with one man and one man alone. His hands are dripping blood, blood of innocent Tanzanians whose only crime was to challenge a regime that has run amok and gone berserk, how sad!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nduganikadema nawashangaeni sana kwakutochukua tahadhar wakati mnajua mnapambana na jiwe ambalo ni humanless,nashaur tembeeni na kila aina ya silaa ili siku tusikie wasiojulikana wamecharazwa mapanga kwa kuvamia watu hamuwez kila siku kulaania,shetani anashughurikiwa kwa moto
Pole kwa mhusika lakin jitahid kuchukua tahadhari na huu utawala wa kimafia
Tata muraa nimekuvulia kofia hivi MTU nisie mfahamu aje anikamate kirahisi bora nipambane kama zakaria kivyovyote vile
 
Wekeni silaha chini muongee myamalize, mtawamaliza vijana maana hawataacha kuongea.., nyumba yenu wote na wote mnahaki sawa... mpira mnaangalia wote, dukani bei moja, hospitali moja, usafiri mmoja, ingekuwa upande mmoja umepunguziwa bei tungeelewa,***** kila siku ugomvi...
 
acha upuuzi wewe, hauyaoni makejeli hayo??
Kwahiyo akikejeli ndiyo ametukana? Nyie ndiye wapuuzi msiotaka kukosolewa😄😄😄😄 mkikosolewa mnatukanwa!!😩😩 kiongozi lazima uwe mstahimilivu
 
Kwanini msichukue hatua?kwani vyombo vya kimataifa hamvijui?
 
Ewe jiwe wanatekwaa ndugu zetu wengine wawapotezwa kisa kukosolewa!! Unawabambikia wapinzani kesi kila mara ili huiridhishe roho yako!!. Ila mungu atakufedhehesha siku moja.Kumbuka hautaishi milele,😄😄😄😄 machungu unaowapa watz wenzio Mwenyeenzi Mungu atakupa Mara mia pamoja na genge lako lote la kitekaji. Mtu akikukosoa kidogo anapotea kwanini? Halafu mnajifanya hamuhusiki!! Kwanini ktk utalala wako ndugu zet u wanapotea sana halafu mpaka Leo watekaji hawajulikani sina shaka kusema utekwaji na ukosoaji vina uhusiano. Kila siku makanisani na bibilia kubwa kumbe wanafki wakubwa, wanaokulinda Leo duniani mbinguni hawatakulinda. Acha kunyanyasa ndugu zetu kwa interest zako.
 
Mbunge wa Kibamba kupitia CHADEMA, John Mnyika kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Twitter amesema kuwa Chadema Mdude amechukuliwa na Watu wenye silaha

Aidha, yeye mwenyewe amesema CHADEMA inafuatiloa suala hilo na taarifa zaidi itatolewa muda si mrefu

======

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA ZA AWALI KUHUSU TUKIO LA MDUDE NYAGALI (MDUDE CHADEMA)


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika hali ya dharura, kinafuatilia kwa karibu, taarifa za Mdude Nyagali (Mdude Chadema) kuvamiwa kisha kuchukuliwa na watu ambao hawajatambulika, akiwa ofisini kwake, eneo la Vwawa, Mbozi, mkoani Songwe, katika tukio lenye dalili za utekaji.

Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda, majira ya jioni ya leo (saa 12 kuelekea saa 1) yalifika magari mawili katika eneo la ofisini kwa Mdude, Vwawa mjini, kisha wakatelemka takriban watu wanne, ambao walimkamata kijana mmoja aliyekuwa nje ya ofisi hiyo wakampeleka kwenye mojawapo ya magari waliyokuja nayo huku wengine wakiingia ndani ya ofisi, alikokuwa Mdude.

Imedaiwa kuwa baada ya muda mfupi kulisikika purukushani, watu hao wakijaribu kumkamata Mdude huku wakimpiga na yeye akipiga kelele za kupinga kitendo hicho na kuomba msaada.

Taarifa za awali ambazo Chama kimezipata kutoka kwa mashuhuda hao zimedai kuwa baada ya kusikika kwa purukushani na kelele hizo, baadhi ya wananchi walijitokeza kutaka kujua kinachoendelea na kutoa msaada, ghafla watu hao waliokuwa wakimpiga Mdude wakatoa silaha aina ya bastola na kuwatishia wananchi hao, kitendo kilichowaogofya wananchi na kukimbia kwa hofu. Imedaiwa kuwa watu hao walimuingiza Mdude kwenye 'buti' ya mojawapo ya gari hizo, wakamuachia yule kijana mwingine kisha wakaondoka na Mdude kuelekea kusikojulikana.

Tayari CHADEMA kupitia kwa Viongozi wa Chama katika eneo husika na Mbunge wa Mbozi Mashariki, Pascal Haonga, kimevitaarifu vyombo vya dola mkoani Mbeya, kwanza kutoa taarifa ya tukio hilo lenye mazingira ya utekaji pia kutaka kujua kama kuna askari waliopewa kazi ya kwenda kumkamata Mdude.

Hadi sasa haijulikani Mdude yuko wapi! Tupaze sauti zetu sote kulaani tukio hili na kutaka Mdude arudishwe au aachiliwe akiwa salama.

Katika hatua ya sasa, CHADEMA kwa nguvu zote kinalaani vikali tukio hilo. Tunavitaka vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi lenye wajibu wa kulinda raia na mali zao, kufuatilia taarifa za tukio hilo kama zilivyoripotiwa kwa polisi katika eneo husika na kuhakikisha Mdude anapatikana na wahalifu waliotenda tukio hilo wanajulikana, kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.

Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi kadri itakavyohitajika.

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

View attachment 1088177


Zaidi, soma;



EEeh tutauwawa watu wako Mpaka lini??

Tunamtaka Mdude arudi akiwa salama bila kuhughudhiwa kwa lolote.

Magufuli Magufuli huyaoni haya??
 
Watanzania yani kama hili suala mtalichukulia la kawaida kila mara mtu anachukuliwa na magari yasiyo na plate number na pia polisi kuendele kukana kwamba hawahusiki hili jambo tutalizoea na itakuwa shida.
Ifikie mahali tulikatae kwa umoja ikiwezekana wakitokea watu wa hivyo wananchi tusiogope silaha tutoke mbele tuonyeshe mfano kwa wachache hao watekaji kuwapiga na kuua hata wengine watajifunza.
Tuacheni uoga na ss tuanze kutega mitego ya kuwanasa,ifikie mahali hali hii ikome mara moja kwa kuwaadabisha.

Pia nimshauri mwenyekiti wa cdm taifa ita vyombo vya habari elekeza kuwa inapotokea jambo kama hilo na sisi tuwajibike kujibu lkn ukikaa kimya kila linapotokea tunaona kawaida litazoeleka.
Viongozi mfike mahali muelewe tu kwamba pia hampendwi ktk taifa hili hasa wa upinzani hivyo hakuna haja ya kuweka ustaarabu mbele,haki lazima ipiganiwe kwa vitendo sio maneno ya faraja faraja kama watu wako msibani,tunapigania uhai wetu wapinzani.

Swelana.
 
Watanzania yani kama hili suala mtalichukulia la kawaida kila mara mtu anachukuliwa na magari yasiyo na plate number na pia polisi kuendele kukana kwamba hawahusiki hili jambo tutalizoea na itakuwa shida.
Ifikie mahali tulikatae kwa umoja ikiwezekana wakitokea watu wa hivyo wananchi tusiogope silaha tutoke mbele tuonyeshe mfano kwa wachache hao watekaji kuwapiga na kuua hata wengine watajifunza.
Tuacheni uoga na ss tuanze kutega mitego ya kuwanasa,ifikie mahali hali hii ikome mara moja kwa kuwaadabisha.

Pia nimshauri mwenyekiti wa cdm taifa ita vyombo vya habari elekeza kuwa inapotokea jambo kama hilo na sisi tuwajibike kujibu lkn ukikaa kimya kila linapotokea tunaona kawaida litazoeleka.
Viongozi mfike mahali muelewe tu kwamba pia hampendwi ktk taifa hili hasa wa upinzani hivyo hakuna haja ya kuweka ustaarabu mbele,haki lazima ipiganiwe kwa vitendo sio maneno ya faraja faraja kama watu wako msibani,tunapigania uhai wetu wapinzani.

Swelana.
Wewe unaishi kwenye nchi ya kusadikika ya Tz......Tz yupi wa kubizana na mtu mwenye bunduki
 
Back
Top Bottom