Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Bila shaka shida hapo ni chademaphobia na sii lingine kwa uratibu wa genge kijani
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, ameonesha masikitiko yake kuhusu taarifa iliyotolewa na chama hicho kuhusiana na tukio la shambulio dhidi ya kiongozi wa wanawake taifa wa chama hicho (BAWACHA). Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani Twitter), Mrema alieleza sababu kadhaa zilizomfanya kutoridhishwa na taarifa ya chama.

Mrema ameeleza kuwa chama hakikuona haja ya kulaani kitendo cha kiongozi wa wanawake kupigwa na kuumizwa na mwanaume, badala yake kinadai kuwa ni taarifa zinazosambazwa mitandaoni. Alisema kuwa hatua hii inaonesha kutokuwepo kwa mshikamano wa ndani ya chama na kutojali hali ya mwanachama aliyeathirika.

Aidha, ameeleza kushangazwa na chama kushindwa kutoa pole kwa kiongozi huyo, ikizingatiwa kuwa mara kadhaa kimekuwa kikitoa pole hata kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanapopatwa na majanga.

Sambamba na hilo, amesema kuwa kutotoa pole kwa mgonjwa kunaleta maswali kuhusu utamaduni wa chama katika kushughulikia masuala ya ndani.

Mrema pia amelalamikia kauli ya chama inayodai kuwa kinachunguza tukio hilo, huku wakati huo huo kikitoa vitisho kwa mhanga wa shambulio hilo. Alieleza kuwa hatua hiyo inazua taharuki na inaweza kuathiri upatikanaji wa ukweli kuhusu tukio husika.

Zaidi ya hayo, Mrema amekosoa kauli za chama ambazo alizilinganisha na kauli zilizokuwa zikitolewa wakati wa uongozi wa Hayati John Magufuli, akihusisha na matukio ya watu kupotea na ukandamizaji wa haki za binadamu.

Katika tamko lake, Mrema amesisitiza kuwa analaani vikali kitendo cha kiongozi wa wanawake kupigwa na wanaume, akikitaja kuwa ni ukatili wa kijinsia unaopaswa kupingwa na kila mtu mstaarabu bila kujali ni nani aliyekumbwa na tukio hilo.

Ameongeza kwa kusema kuwa ukatili huu hauna tofauti na vitendo vingine vya kikatili vinavyowakumba wanawake nchini, na hivyo akatoa wito wa mshikamano wa pamoja katika kupinga matendo kama haya, ndani na nje ya vyama vya siasa.
 

Attachments

  • 1743422363479.jpg
    591.2 KB · Views: 17
Team Mbowe kumeanza kuchangamka. Bado wana wenge la kushindwa uchaguzi. Mbona Msigwa aliponyang'anywa ushindi wa mwenyekiti kanda ya Nyasa na Mbowe chama hakikumlaani Mbowe?
 
Huyo mrema naye aende CCM tu bado wanapokea makapi toka Chadema akiwepo huyo chapombe anayeigiza kupigwa.
 
John Mrema ana akili kuliko viongozi wote wa Chadema jumlisha na wafuasi wake mapuruzai!
 
Kila siku mnalia lia kuwa chama kimekufa, Jiwe alijaribu akaishia kufa yeye. Chadema imekupa ajira ya buku 7 kwa siku, bila chadema ungepost na kulipwa na nani? Au ungepost mambo ya Chauma?
Msishiriki uchaguzi muone kama hakijajufia
 
Wanachunguza? Lini chadomo wamekuwa jeshi la polisi?
Ni lini policcm wamechunguza soka na wenzake mpka sasa hawajapatikana ni Uchunguzi gani wanaofanya?

Kiufupi hakuna jeshi kuna genge la ccm linalovaa sare za polisi.
 
Uyu nae atulie kama anaenda ccm aende, kuna watu kumbe walikua chadema kimkakati sasa ndo tunaanza kuwajua, ichi chama kilikua kinaenda kufa aisee, wenda wote waliokua wamemzunguka Mbowe walikuwa mamluki ,usiku wapo ccm, mchana wapo kuchekacheka kwa Mbowe
 
Vijana wa ccm badala ya kumsafisha mama na mabilion ya hela yaliyopotea wao wanacheza mziki wa chadema.
 
Nategemea taarifa ya uchunguzi wao itakuja na sintofahamu zote
Ccm imempa mtu script mwenye uwezo mdogo wa kuicheza. Saa hii itabidi wamtibu hadi apone, ama waendelee kuwataka madactari wamuache hapo hosptalini kwa minajili ya siasa za kiki. Wanacdm wengi na wanaccm wako mahospitalini na hawana uwezo wa matibabu, mbona ccm haiwapatii fedha za matibabu, ama kuwatembelea ili kudhihirisha wema wao?
 
#UPDATES Aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, ameonesha masikitiko yake kuhusu taarifa iliyotolewa na chama hicho kuhusiana na tukio la shambulio dhidi ya kiongozi wa wanawake taifa wa chama hicho (BAWACHA). Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani Twitter), Mrema alieleza sababu kadhaa zilizomfanya kutoridhishwa na taarifa ya chama.Mrema ameeleza kuwa chama hakikuona haja ya kulaani kitendo cha kiongozi wa wanawake kupigwa na kuumizwa na mwanaume, badala yake kinadai kuwa ni taarifa zinazosambazwa mitandaoni. Alisema kuwa hatua hii inaonesha kutokuwepo kwa mshikamano wa ndani ya chama na kutojali hali ya mwanachama aliyeathirika.Aidha, ameeleza kushangazwa na chama kushindwa kutoa pole kwa kiongozi huyo, ikizingatiwa kuwa mara kadhaa kimekuwa kikitoa pole hata kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanapopatwa na majanga. Sambamba na hilo, amesema kuwa kutotoa pole kwa mgonjwa kunaleta maswali kuhusu utamaduni wa chama katika kushughulikia masuala ya ndani.Mrema pia amelalamikia kauli ya chama inayodai kuwa kinachunguza tukio hilo, huku wakati huo huo kikitoa vitisho kwa mhanga wa shambulio hilo. Alieleza kuwa hatua hiyo inazua taharuki na inaweza kuathiri upatikanaji wa ukweli kuhusu tukio husika.Zaidi ya hayo, Mrema amekosoa kauli za chama ambazo alizilinganisha na kauli zilizokuwa zikitolewa wakati wa uongozi wa Hayati John Magufuli, akihusisha na matukio ya watu kupotea na ukandamizaji wa haki za binadamu.Katika tamko lake, Mrema amesisitiza kuwa analaani vikali kitendo cha kiongozi wa wanawake kupigwa na wanaume, akikitaja kuwa ni ukatili wa kijinsia unaopaswa kupingwa na kila mtu mstaarabu bila kujali ni nani aliyekumbwa na tukio hilo. Ameongeza kwa kusema kuwa ukatili huu hauna tofauti na vitendo vingine vya kikatili vinavyowakumba wanawake nchini, na hivyo akatoa wito wa mshikamano wa pamoja katika kupinga matendo kama haya, ndani na je ya vyama vya siasa.#EastAfricaTV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…