PreGE2025 John Mrema: CHADEMA imeua ndoto za waliotaka kugombea, mpaka 2030 sina uhakika kama tutakuwepo

PreGE2025 John Mrema: CHADEMA imeua ndoto za waliotaka kugombea, mpaka 2030 sina uhakika kama tutakuwepo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwa tulichoshuhudia 2019,2020 na 2024 kushiriki uchaguzi chini ya mifumo ile ile na usimamizi wa watu wale wale na wenye nia ovu zile zile itakuwa kitendo cha kipumbavu. Hawa G 55 ambao inaaminika nyuma yao yupo Freeman Mbowe wanajiaminisha kuwa watatangazwa kutokana na makubaliano binafsi ya Mbowe na Rais Samia ya Chademakuachiwa majimbo 40,ila wakumbuke 2020 Magufuli alifanya makubaliano binafsi na James Mbatia kuwa NCCR Mageuzi itaachiwa majimbo 20 na kukifanya kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni lakini hata diwani mmoja hakuachiwa. Mbowe aache kuwajaza ujinga G 55 CCM hawawezi kukubali kuwatosa wabunge wao na kuwaachia wao hiyo ni ghilba na hadaa tu.
 
Wakuu,

Akiwa anazungumza leo, John Mrema amesema kuwa CHADEMA imeua ndoto za wanachama wengi waliotaka kugombea kwenye Uchaguzi ba kuongeza kuwa hana uhakika kuwa kama chama hicho kitakuwepo hadi kufikia mwaka 2030

"Jambo la pili ni chama chetu kutosaini kanuni za maadili ya uchaguzi na kukifanya sasa chama chetu kujiondoa rasmi kwenye uchaguzi. Jambo hili limeua ndoto za wanachama wa CHADEMA, wapo watu wapo CHADEMA kwasababu wanawiwa kuwa madiwani wawawakilishe wananchi kwenye kata zao, wapo akina mama wanawiwa kuwa madiwani wa viti maalumu wakakiwakilishe chama na wananchi wao kwenye kata zao, kina mama hawa ndoto zao zimekufa.

"Wapo watu wanataka kuwa wabunge, kwa kutosaini kanuni, ndoto za watu hawa zimekufa mpaka mwaka 2030, hatuna uhakika kama tutakuwepo , CHADEMA itakuwepo ama laa..lakini tunawasikia viongozi wetu wakisema bora chama kife, nimemsikia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA bara John Heche."

"Wanafika mahali wanajaribu kuonesha kwamba bado kuna mlango wa kimiujiza unaweza kufunguka, tumemsikia mwanasheria mkuu wa chama akisema kuwa wanaweza bado kwenda kushiriki uchaguzi, kanuni kifungu cha 1.5 kinasema wazi chama kisichosaini maadili hakitakuwa na haki ya kushiriki uchaguzi, kanuni zimeshachapishwa kwenye gazeti la serikali, sasa ni rasmi kwamba CHADEMA haitashiriki uchaguzi mkuu wa 2025"

"Watu hawa waliokuwa na ndoto za muda mrefu na wengine wamekitumikia chama hiki kwa miaka mingi, ndoto zao zimeuawa kwasababu tu ya kiburi cha viongozi wetu"
No reform no election. Waende ACT
 
Sio lazima wagombee kupitia CHADEMA.

Mbona kakiri mwaka 2019 Wagombea walienguliwa 100%

Tuingie uchaguzin Uhuni kama huo urudie???.
Hao jamaa kumbe hawakuwa wapinzani wana mabadiliko bali wasaka nafasi wabadilishe maisha!
Bora wamejulikana mapema!
Hasa huyo Mrema kipindi cha nyuma alikuwa anabana pua kutoa matamko kumbe ni mnafiki pro max!
 
Back
Top Bottom