PreGE2025 John Mrema: CHADEMA 'imeuzwa' ndiyo maana tumeondoka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
John, kumbe msingi wa kufikiri kwako ilikuwa ni chadema. Now you can not think!
 
Mrema ametufungua macho na akili, bye bye chadema!
 
Huyu Mrema ni taahira sio bure!
 
Chama sio cha mtu mmoja, none sense
 
Sawa ,CHADEMA ,kimeuzwa . Je! Bwana John anawez kutoa maelezo zaidi.
1. Kina nani walihusika kuiuza Chadema.
2. Fedha za mauzo ya CHADEMA alipewa (alizipokea) nani
3.Kina Nani walinufaika na mgawo wa fedha hizo.
4. Je! Baada ya CHADEMA kuuzwa mgawo wa fedha za mauzo uliendaje?
5.Je?, Yeye Kama kiongozo mwandamizi aliyepita alipokea Kiasi gani cha fedha kwenye mgwao huo wa mauzo ya CHADEMA.
6. Anaweza kutueleza CHADEMA imeuzwa kwa Kiasi gani cha fedha za madafu au $USD ngapi.
7.Je ? anawez kutueleza Kati ya waliokiuza Chadema na waliokinunua Nani anaipenda CHADEMA
8.Je? Kwa nini hawataji waliouza CHADEMA badala yake anawataja tu waliokinunua.
9. Je? Anaweza kutueleza kwa nini alipokea mgawo wa mauzo ya CHADEMA Kama kweli alikuwa anakipenda?
 
Mkurugenzi wa kurugenzi ya Habari na Taarifa kwa Umma wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), John Mrema amedai kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 'kimeuzwa' kwa watu wasiokuwa na mizizi na uchungu wa chama hicho ambacho amekieleza kukosa mwelekeo.

Mrema ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika siku ya Jumatano Juni 04, 2025, Mjini Musoma mkoani Mara katika mwendelezo wa Operesheni ya CHAUMMA For Change (C4C).

"Chama chenu leo kimekabidhiwa kwa mtu aliyeishi Ikulu maisha yake yote mpaka alipostaafu, akajiunga nacho 2015, Edward Lowassa akampendekeza awe mbunge, wenzake wawili walisharudi CCM, yeye kumbe alibaki kimkakati, leo kakabidhiwa CHADEMA, ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, halafu mnasema chama hakijauzwa, nendeni mtafakari", ameeleza Mrema.

Your browser is not able to display this video.
 
Kwanini hakujiondoa wakati huo?
 
..mambo ya kati yai na kuku kipi kilianza hayatawasaidia, rekebisha kasoro!
Umetoka nje ya mada. Mrema anasema CHADEMA imeuzwa na kuhusisha ujio wa Lowassa na uuzwaji huo. Sasa wakati Lowassa anakuja CHADEMA kina Mrema si ndiyo walikuwa viongozi waandamizi pale Makao Makuu? Nani alaumiwe!?
 
Sema tunapoteza muda kumsikiliza huyo Mrema wazee daa mshana Jr njoo na nyuzi zako za sitting room nisafishe macho tu..
 
Umetoka nje ya mada. Mrema anasema CHADEMA imeuzwa na kuhusisha ujio wa Lowassa na uuzwaji huo. Sasa wakati Lowassa anakuja CHADEMA kina Mrema si ndiyo walikuwa viongozi waandamizi pale Makao Makuu? Nani alaumiwe!?
..kulaumu waliopo au wasiokuwepo hakusaidii, attention iko kwa aliyetajwa kuwa mwenyekiti wa bodi Lucy mollel..kila siku chadema wanalalama usaliti wakati makosa wanayatengeneza wao wenyewe..wala huyo mama si mwanasiasa, hawezi siasa huo ndio ukweli na hawezi kuwakana hao aliowatumikia hadi akastaafu na ni penshena wao! Jibu ni kumuondoa hapo chama kiwe salama.
 
Sasa hapa unaleta hisia. Kuna watu wengi tu ni wafia CHADEMA lakini zamani walikuwa ni CCM kindaki ndaki.

Unatakaje "Civil servant" wa miaka ya themanini asiwe aliwahi kuwa mwana CCM enzi za mfumo wa chama kimoja?

Hoja yangu Luth Molell kaja wakati kina Mrema wakiwa ni viongozi waandamizi ndani ya chama na wakampokea. Leo miaka 10 baadae ndiyo wanajua kuwa kumbe alikuwa anafanya kazi Ikulu?
 
Dduuu siasa za afrika ni ukichaa mtupu
 
Sio yeye ndo amenunuliwa?
Yaani ujinga ni mzigo!!
 
Ruth Mollel alikulia Ikulu maisha take yote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…