PreGE2025 John Mrema: Hakuna kikao kilichopitisha suala la kuzuia uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Lissu amemaanisha maana kamili ya NRE.Lazima ifike mahali kuwe na mageuzi ya kweli,ambayo yatahitaji watu ambao wako tayari hata kupoteza bhai wao.
Haiwezekani ujanjaujanja ufanyike wakati uko wazi kabisa kua tunachezewa akili.
Wabadili mbinu basi,yaani ujinga ufanyike bila sisi kujua,hii itawaondolea upinzani hawa watawala.
 
Tatizo la John Mrema ni kuwa hakuwa na plan B ya maisha yake, aliamini ile ajira aliyokuwa nayo pale Chadema HQ ni ya kudumu kwake, baada ya mabadiliko ya uongozi na yeye kutupwa nje ndiyo amejenga hii chuki kwani hata hela ya beer moja sasa kwake ni shida ndiyo maana amekubali kandarasi aliyopewa na CCM kuivuruga Chadema. Kama shida ni kugombea mbona ACT Wazalendo wameshawaalika hao G 55 waende huko ili kutimiza ndoto yao ya kugombea Ubunge kwa nini anaendeleza bifu na uongozi mpya wa Chadema?
 
Wewe siyo msemaji wa Chadema, usijiingize kwenye huu upuuzi wa G 55 ambao wanatumiwa na CCM kuleta fujo Chadema, ilinde heshima yako ndogo sana iliyobakia hapa Jukwaani, please.
 
Inaonyesha kamanda John Mrema alikitegemea sana chama kuendesha maisha ya kila siku kutokana na cheo alichokuwa nacho pale makao makuu. Ukiangalia malalamiko anayoyatoa kila uchwao kwa uongozi wa sasa wa CDM utatambua dhahiri ni mtu ambaye amekosa fursa ya kutengeneza fedha binafsi.

Ukiangalia kwa jicho la tatu, utaona ni aina ya mtu ambaye anataka kufaya "pre-emption" ili kuficha aibu ya kuondolewa katika sehemu aliyopiga fedha kwa muda mrefu. Anachokifanya sasa ni kutafuta fursa mpya ya kupiga fedha dhidi ya uongozi wa sasa kwa njia ya upinzani wakificho akiwa ndani ya chama.

Anatambua kukubalika kwa uongozi uliopo kwa wananchi waliokuwa wengi nchini kwa hivi sasa, pia anatambua mvuto waliokuwa nao viongozi waliopo pamoja na ajenda yao nzuri ya mabadiliko wanayoibeba. Ni dhahiri kabisa yeye na kundi lake wanatumika kama maadui waliopo ndani ya chama wakiungana na wale wa nje ili kutaka kudhoofisha mapambano yanayoendelea.

Si ajabu wao pamoja na baadhi ya viongozi fedhuli wa CCM na wa serikali pamoja na baadhi waliopo mahakamani, ndio ambao wanashirikiana na genge la maafisa wa vyombo vya dola ili kuendesha vitendo vya hujuma dhidi ya CDM kwa sasa. Si ajabu nyuma ya pazia anakutana na akina Mulilo ili kuleta drama ya kisiasa inayoendelea hivi sasa katika siasa ili kukipa unafuu chama tawala tuelekeapo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Manabii na wanajimu wamekwisha tabiri kuhusu hatima ya CCM tuelekeapo uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Wote wanatoa hitimisho moja,

MENE, MENE, TEKELI & PERESI (Rejea Danieli 5:25-28)

Ama kwa hakika NENO linakwenda kuthibitika,
MENE - Mungu ameuhesabu utawala wako batili na kuukomesha ....... X 2.
TEKELI - Utawala huu umepimwa katika mizani ya HAKI nao umeonekana kuwa umepungua.
PERESI - Utawala wao na umegawanyika, nao wanaenda kupewa wapinzani wa ndani na nje wa chama chao ili waje na utawala mpya na kuichukua nafasi yao.
 
Huyu Mangi alipiga hela sana za ruzuku na zote alikuwa ananywea pombe alijua atadumu milele pale sasa mfumo umemtema ndiyo mayowe kila siku.
 
Acha uhuni kiongozi mtu mzima huwezi kumtisha kwa staili halali vya chama

Yaani vikao vya ngazi ya juu vikae na posho wapewe kwenda kutishia?
 
Mshkaji ana uchungu sana wa kuwahudumia wananchi, nahisi analia sana usiku akikumbuka no reform no election, anasikia kufakufa anapoona Oct inakaribia kwa kasi sana I gues! 😃

Yani ulaji unapita hivihvi bora jiwe angekuwepo huenda angefika bei
 
Usitumike vibaya we Mzee, unajikosesha heahima bure...
unataka watu waende tena kwenye uchaguzi ili wafe, wapate vilema vya maisha, wapate kesi za mauaji, wafikisiwe siyo
Majuzi tu chini ya uongozi wenu mmepigwa nje ndani vibaya sana Serikali za mitaa hata mtaa mmoja nchi nzima hamkupewa leo eti unautaka tena uchaguzi kwa mazingira yaleyake kwa sheria zilezile - hivi kichwani una kitu chochote we Mzee?

No Reforms No Election... Ukitaka Ubunge tangulia kwa Zitto anakuita na timu njaa wenzako.

Taifa limeshamwelewa Lissu na hii si agenda ya CDM tena bali ya kitaifa zaidi.
 
Mrema ana hoja muhimu. Lissu na utawala wake mpya wangeitisha kikao kuponya majeraha.

Kusikiliza maoni ya wenzao wanaendaje mbele, ikiwezekana zipigwe kura kususia uchaguzi, kuzuia uchaguzi, kukinukisha wakati wa uchaguzi faida na hasara ya kila sera ichambuliwe na kupigiwa kura.

Ruto, Kenya alishinda kwa 51% ilibidi baadaye awaite wapinzani kujenga serikali ya kitaifa. Zanzibar walifanya hivyo hivyo.

Margin ya ushindi inasema wanaotuunga mkono na wanaounga mkono upande mwingine ni nusu nusu, 50/50.

Busara hapo inahitajika, tunaendaje mbele pamoja? sio ubabe.
 
Mbona hamjibu hoja unamjibu mtoa hoja. Hiv demokrasia maana yake nini.
 
Lakin jamaa kazungumziq kuna kuvunja katiba ya chama usiposhiriki uchaguz hilo mnalisemaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…