PreGE2025 John Mrema: Hakuna kikao kilichopitisha suala la kuzuia uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Na John Mrema kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X

KWA HESHIMA NIMEJIBU ANDIKO LA MWANASHERIA MKUU WA CHAMA DR. RUGEMELEZA NSHALA, GROUP LA MASWALI MAGUMU

Mwanasheria Mkuu wa Chama, salaam. Nimesoma maoni yako ambayo yamejaa uchungu na maumivu ,lawama na kejeli . Umesema kuwa uongozi mpya unasimamia maamuzi ya vikao vya Kamati Kuu na Mkutano Mkuu wa chama, ila hujaweka ushahidi wowote ule kwamba kulikuwa na azimio la KUZUIA UCHAGUZI. Hapakuwa na azimio hilo kama lipo ,tafadhali weka ushahidi mezani ili Dunia ijue na iwapuuze wote wenye hoja kinzani.

Pili, umesema kuwa walioshindwa uchaguzi wa ndani ya chama ndio wanaopinga, ila hujasema ukweli kuhusu ambao hawakuwa na upande ndani ya uchaguzi ule na ambao ni wagombea ambao walishawekeza sana kwenye Kata na Majimbo ya uchaguzi na walitakiwa kufanya maandalizi tangu Tangazo la Katibu Mkuu la Januari ,2023 akiwa Mwanza alipowataka wagombea wote watie nia ya kugombea na waendelee na maandalizi ya kiuchaguzi.

Ushahidi wa hili ni kuwa Mwenyekiti wa Chama alitia nia ya kugombea urais na mpaka leo hajawahi kuiondoa nia hiyo , na wapo wagombea Ubunge ambao hawajaondoa nia zao kwani hapajatoka tangazo rasmi la Chama kuwa hakitashiriki uchaguzi mkuu wa 2025.

Tatu, umesema kuwa Kuna azimio la Mkutano mkuu la no reforms no election ,na kwamba lilisimamiwa na Mwenyekiti Mbowe ; nakuomba ufanye utafiti wako kabla ya kujiingiza kwenye hizo propaganda uchwara ; utafiti wako ujikite kwenye maeneo yafuatayo ili ukweli ukuongoze ;

1. Ajenda ya No reforms no election ; ilianza mwaka gani ,na ilikuwa na malengo gani ,nini ilikuwa tafsiri halisi ya kampeni hiyo ?

2. Mwaka 2020 Januari ,kamati kuu iliyokutana Makueni ,nchini Kenya na kuja na kampeni hiyo ilimaanisha nini? Mbona hatukuzuia uchaguzi wa 2020 kama maana ilikuwa mi kuzuia uchaguzi mkuu?

3. Taarifa ya Baraza kuu kwa mkutano mkuu uliwataka viongozi kwenda kufanya maandalizi ya kuingia kwenye uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuandaa wagombea,ilani ,rasilimali . Kama kulikuwa na kuzuia uchaguzi , kwanini mkutano mkuu uliazimia kwenda kufanya maandalizi hayo ?

4. Kwa nini katibu mkuu hakusaini maadili ya uchaguzi ? Alipewa mamlaka hiyo na kikao gani? Mbona hapakuitishwa vikao kabla ya kufikiwa kwa uamuzi huu mkubwa na wenye madhara makubwa kwa chama chetu? Nani ananufaika na uamuzi huu? CCM inapita bila kupingwa, nani mnufaika wa mpango huu na amelipwa au ameahidiwa kupewa ujira gani?

5. Malengo ya chama chetu kwa mujibu wa katiba ibara ya 4.1.1 ni kushiriki na kushinda Chaguzi......mamlaka ya kuvunja katiba ya chama anayo nani? Adhabu ya kuvunja katiba ya chama ni ipi ? Kama mtu hakubaliani na malengo ya chama anaweza kuendelea kuwa Mwanachama?

6. Ibara ya 5 ya katiba yetu imetoa haki kwa wanachama ikiwa ni pamoja na haki ya kugombea na kuchaguliwa kwenye chaguzi mbalimbali ; Haki hii inavunjwa na uongozi wa chama ,nini adhabu yake ? Au kiongozi anaweza kuvunja katiba ya chama na asikemewe au kuchukuliwa hatua ? Naomba ukikamilisha huo utafiti wako utupatie taarifa ili tuweze kujiongoza vyema .

Huu mtindo wa kulaumu watu na kuwapa majina hauwezi kusaidia Chama, na kumbuka chama cha siasa sio pressure group. Chama kina malengo ya kisiasa tofauti na wanaharakati ambao malengo yao ni ya muda mfupi tu na wanaendana na upepo kadiri unavyovuma ,ila chama cha siasa malengo yake ni kushinda chaguzi na kutumia sera zake kuwaondolewa wananchi matatizo makubwa kama vile sheria kandamizi,kutumia rasilimali kwa manufaa ya wote ,kuondoa ukandamizaji nk.

Unapokimbia uchaguzi utaweza vipi kufikia malengo hayo ? Siasa ni mapambano ya kudumu, yapo na yataendelea kuwepo mpaka malengo yatakapofikiwa ,tofauti na wanaharakati ambao ajenda zao sio za kudumu, watapambana na mazingira, ikija covid watahamisha magoli ,ukija ukimwi watahamia huko na mengineyo mengi .

Blame game is equal to zero sum game ! Alamsiki
Huo kaufanyie kwa jirani uliyemthamini kuliko ulivyowathamini wanafamilia yako.
 
Nimemsoma Mrema, ni bahati mbaya sana wapo wanaomshambulia badala ya kujadili hoja. Mrema ndiye mtu aliyetoa taarifa za maamuzi mengi ya vikao ikiwemo ya No Reforms No Election. Anazo pdf zake. Anasema No Reforms No Election haikuazimia CHADEMA igomee uchaguzi.

Tujadili hapo...anayempinga Mrema aweke pdf kwa umma ya uamuzi wa kugomea uchaguzi. 🙏🙏🙏
 
Yani mrema ananini atakachofanya ili uchaguzi usiwe kama wa 2019;
 
Kamanda John Mrema kama upo humu jukwaani, nina ushauri kwako! Kubali tu matokeo Kamanda. Maana hiki unachokifanya mpaka sasa, kinaonesha bado hujakubali matokeo.
Na sababu kubwa ya kuendelea kuwa na kinyongo kisichoisha, inawezekana kimesababishwa na kile kitendo cha kuondolewa kwenye ulaji pale makao makuu ulipodumu kwa miaka mingi!

Natambua fika Kamanda Mbowe alikulea na kukudekeza kama mtoto wake wa mwisho! Lakini sasa mambo yamekuwa tofauti! Hivyo ni wakati sasa wa kuingia mtaani ili ujitafutie chakula chako kwa jasho. Huna sababu ya kuleta upinzani usio na kichwa wala miguu ndani ya chama. Na ukisema uende ccm au chama kingine cha upinzani, utaishia tu kufa njaa! Kutokana na ukweli kwamba, wewe siyo asset! Wewe ni liability.
Nadhani ungemlaumu kwanza Mwanasheria Mkuu wa Chama ambae alianzisha upya zogo zima. Anachofanya Mrema ni kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake. Maswali yake yajibiwe badala ya kumsimanga. Kusema kuwa alidekezwa na Mbowe na kuwa anaganga njaa ni kukwepa kumjibu. Liability ni wale ambao wanakimbilia kejeli na shutuma zisizo na ushahidi. Mbinu hizo zilifanikiwa wakati wa uchaguzi lakini sio sasa. Jibuni hoja zake.

Amandla...
 
Hivi huyo Mrema bado ni msemaji wa Chadema?
Kama ndivyo,basi alete ushahidi kama ajenda hiyo haikuwepo.
Mrema kauliza swali. Kwa vile document zote ziko ofisini na walioulizwa wana access nazo, wamjibu tu. Yeye hana access kwa sababu hana cheo chochote katika chama.

Amandla...
 
Kinachomsumbua hakujipanga kabisa kuishi maisha ya usekretarieti nje ya chama...kwisha habari yake
 
Lissu amemaanisha maana kamili ya NRE.Lazima ifike mahali kuwe na mageuzi ya kweli,ambayo yatahitaji watu ambao wako tayari hata kupoteza bhai wao.
Haiwezekani ujanjaujanja ufanyike wakati uko wazi kabisa kua tunachezewa akili.
Wabadili mbinu basi,yaani ujinga ufanyike bila sisi kujua,hii itawaondolea upinzani hawa watawala.
Huo utayari wa kupoteza uhai wao unatokana na nini wakati kampeni ya NRNE ni ya kuzuia watu kupoteza uhai wao katika uchaguzi? Kwamba wako tayari kupoteza uhai wao kwa ajili ya NRNE lakini wanapata kigugumizi linapokuja suala la kudai haki ifanyike wakati wa uchaguzi! Make it make sense.

Amandla...
 
Nimeona barua inayomhusu huko nadhani atakuwa ameshaipata aanze kwenda mahakamani
 
Back
Top Bottom