PreGE2025 John Mrema: Hakuna kikao kilichopitisha suala la kuzuia uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huo kaufanyie kwa jirani uliyemthamini kuliko ulivyowathamini wanafamilia yako.
 
Nimemsoma Mrema, ni bahati mbaya sana wapo wanaomshambulia badala ya kujadili hoja. Mrema ndiye mtu aliyetoa taarifa za maamuzi mengi ya vikao ikiwemo ya No Reforms No Election. Anazo pdf zake. Anasema No Reforms No Election haikuazimia CHADEMA igomee uchaguzi.

Tujadili hapo...anayempinga Mrema aweke pdf kwa umma ya uamuzi wa kugomea uchaguzi. 🙏🙏🙏
 
Yani mrema ananini atakachofanya ili uchaguzi usiwe kama wa 2019;
 
Nadhani ungemlaumu kwanza Mwanasheria Mkuu wa Chama ambae alianzisha upya zogo zima. Anachofanya Mrema ni kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake. Maswali yake yajibiwe badala ya kumsimanga. Kusema kuwa alidekezwa na Mbowe na kuwa anaganga njaa ni kukwepa kumjibu. Liability ni wale ambao wanakimbilia kejeli na shutuma zisizo na ushahidi. Mbinu hizo zilifanikiwa wakati wa uchaguzi lakini sio sasa. Jibuni hoja zake.

Amandla...
 
Hivi huyo Mrema bado ni msemaji wa Chadema?
Kama ndivyo,basi alete ushahidi kama ajenda hiyo haikuwepo.
Mrema kauliza swali. Kwa vile document zote ziko ofisini na walioulizwa wana access nazo, wamjibu tu. Yeye hana access kwa sababu hana cheo chochote katika chama.

Amandla...
 
Kinachomsumbua hakujipanga kabisa kuishi maisha ya usekretarieti nje ya chama...kwisha habari yake
 
Huo utayari wa kupoteza uhai wao unatokana na nini wakati kampeni ya NRNE ni ya kuzuia watu kupoteza uhai wao katika uchaguzi? Kwamba wako tayari kupoteza uhai wao kwa ajili ya NRNE lakini wanapata kigugumizi linapokuja suala la kudai haki ifanyike wakati wa uchaguzi! Make it make sense.

Amandla...
 
Nimeona barua inayomhusu huko nadhani atakuwa ameshaipata aanze kwenda mahakamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…