Pre GE2025 John Mrema: Wanachama na Viongozi wa CHADEMA waliokamatwa hadi sasa ni 427

Pre GE2025 John Mrema: Wanachama na Viongozi wa CHADEMA waliokamatwa hadi sasa ni 427

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), John Mrema amedai kuwa mchakato wa kuwakamata Wanachana na Viongozi wa Chama hicho unaendelea.

Akizungumza na JamiiForums amesema “Hadi kufikia leo Asubuhi (Agosti 12, 2024) jumla ya Wanachama na Viongozi wa CHADEMA waliokamatwa Nchi nzima ni 427, wapo waliokamatwa Morogoro, Dodoma, Iringa, Njombe-Makambako, Mbeya na Rukwa- Sumbawanga.”

Pia Soma:

Aisee very pain , kwa maana nyingine chama kipo ndani kuna jambo la haraka la kufanya , makam mwenyekiti Zanzibar haitishe kikao cha dharula na kuja na tamko moja kwa haraka sana

Organ za chama zifanye kazi sasa , baraza la wazee, baraza la wakina mama , baraza la vijana kila mkoa , mapendekezo yangu
 
Wamefanya kosa gani?

Hebu taja kosa walilofanya na adhabu yake.

Tuanzie hapo.
Kwanini mimi ndiye nilyezuwa kuwa kuna waliokamatwa? Unaumwa nini?

Muulize mleta mada aliyekuja na huo uzushi. Au ni ushuzi?
 
Watakamatwa bila kosa?

Ukileta habari ulete za ukweli.

Wengine tunafahamu, chadomo hawana sera wala ilani, ni wahuni tu waleta fujo. Wakikamatwa hatushangai.
Wamefanya kosa gani,jibu acha upumbavu.
 
Nauona mwisho wa CCM. anayewashauri kukamata kamata wapinzani basi anawapotosha. Kiufupi janga la Kenya halijawapa somo tu viongozi wetu! Watanzania wanewafanya wajisahau sasa. Mama nchi itamshinda!!!
Mara mbili?? Ishamshinda tayari
 
Nijibu mimi badala ya kumuuliza aliyeleta huu uzushi? Au ni ushuzi?

Punguwani wahed.
Pole SANA nasikia upo kwenye EDA 🤣🤣🤣 ndo maana unakuwa mkali, na matumaini ya kurejewa madogo mno😅😅pole sana 🐸
 
.
20240813_125947.jpg
 
Pasi na shaka Mkutano wa Chadema tarehe 12/08/2024 Jijini Mbeya, ulikuwa tofauti kubwa na mikutano mingine ya Chadema iliyowahi kufanyika nchini hivyo Uamuzi wa Serikali kuuzuia umeungwa mkono na baadhi ya wananchi na wanasiasa nchini.

Mohamed Issa Ubuguyu, mwanachama wa CUF, amesema Serikali iko sahihi kuzuia mkutano huo ikiwa imeona Kuna viashiria vya uvunjifu wa amani.

Ubuguyu anasema, wakati mwingine wanasiasa wanatumia vibaya uhuru uliopo kwa nia ya kuanzisha harakati za machafuko ili tu kukidhi matakwa yao.

"Tuwe wakweli jamani, tunataka uhuru wa maoni, ambao tunao tusiutumie vibaya, na Serikali haifanyi kazi kwa kubahatisha, mkutano huo wa Chadema kabisa ulikuwa na viashiria vya vurugu.

"Tufanye siasa, lakini tutangulize maslahi ya umma, amani na utulivu ni kipaumbele Cha kwanza," anasema Ubuguyu.

Justice Mwalambalo, mwanachama wa ACT Wazalendo, anasema bayana kwamba, huenda Kuna kitu nyuma ya mkutano huo wa Mbeya na ndiyo maana nguvu kubwa ilielekezwa huko tofauti na miaka ya nyuma ambayo Bawacha imekuwa ikiadhimisha kongamano la vijana.

"Mbona tangu tumeruhusiwa kufanya siasa za majukwaani hatujawahi kuzuiwa? Wenzetu Chadema walizunguka nchi nzima na agenda ya Katiba Mpya na Mkataba wa Bandari na hakuna aliyewazuia, iweje iwe sasa? Serikali siyo wajinga, yawezekana kabisa kuna kitu wamekiona," anasema Mwalambalo.

Juma Mpula, mkazi wa Mtaa wa Mwakibete Jijini Mbeya amejaribu kuunganisha matukio huku akirejea kauli zilizotolewa na baadhi ya wanaharakati na wafuasi wa chama hicho siku chache kabla ya mkutano.

"Ukweli ni kwamba Chadema imekuwa ikifanya mikutano ya kisiasa na hata maandamano katika maeneo mbalimbali nchini kuelezea ajenda na masuala mbalimbali kuhusu itikadi za chama hicho pasipo kuzuiliwa na mamlaka za Serikali."

Mkutano wa Chadema uliopangwa kufanyika tarehe 12/08/2024 ulilazimika kuzuiliwa na mamlaka za Serikali kutokana na sababu kadhaa, zikiwemo viashiria vya uchochezi na uvunjifu wa amani.

Mpula ametolea mfano Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA, Moza Ally, ambaye katika moja ya kauli zake alisikika akisema: “Kama kijana yeyote unayeipenda nchi yako ya Tanzania umeshalia miaka yako yote, siku hiyo ya Agosti 12, 2024 tunakwenda kuweka hatma ya taifa letu la Tanzania mkoani Mbeya, kwa hiyo kijana yeyote uliyepo popote Tanzania njoo Uwanja wa Ruanda Nzovwe, Mbeya..... Tupo Serious na jambo hili, kwa hiyo vijana wote wa Chadema kama ambavyo vijana wa Kenya wamejitambua siku ya Tarehe 12/08/2024 tunakwenda kuacha uteja kwa serikali, vijana wa Kitanzania na kuweka maazimio makubwa ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2025.” mwisho wa kunukuu.

Mpula akasema: "Ukiangalia kauli zile utabaini kwamba kulikuwa na jambo walilokuwa wanalikusudia, sasa wamezuiwa wanaona azma yao haijatimia na wanataka huruma ndiyo maana wanapiga kelele," anakumbusha.

Mpula ameonya kwamba vyama vya upinzani visitengeneze matukio ili kuungwa mkono na wananchi, kwani kitendo hicho kinaweza kuleta athari ya amani na utulivu nchini.

Mwanamvua Nyambi, Mkazi wa eneo la Mbalizi amesema, vyama vya siasa na viongozi wao wawafikirie zaidi wananchi kwa kudumisha amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.

"Hiki ni kipindi kigumu sana, lakini ndicho wanasiasa wanaotafuta 'kiki' hukitumia kujijenga bila kujali kitakachowapata wananchi. Matukio kama haya yaliwahi kutokea huko nyuma, walioumia ni wananchi wa kawaida tena kwa ukaidi wa viongozi wa kisiasa baada ya kuzuiwa kukusanyika," anakumbusha Mwanamvua.

My take

Naiomba Serikali iendelee kusimamia haki pale panapostahili na kuzuia machafuko ikiwa vyombo vya Dola vitabaini mikutano hiyo inaweza kuleta uvunjifu wa amani nchini.
 
Tume kuwa tuki jiuliza juu ya kutekwa na kupotea kwa ndugu zetu watanzania kwa ombwe kubwa, lawama zilipelekwa kwa polisi na vyombo vingine vya usalama huku polisi kumpitia IGP na waziri Masauni wakitoka hadharani na kukanusha, ili fika mahali hadi Mh Rais aka wajibu Watanzania kwa vijembe kwamba wana jiteka wenyewe.

Kwa hili la juzi Mbeya, watu kukamatwa na polisi, badala ya kupelekwa mahali walipo kamatwa wana pelekwa Iringa, Njombe, Dar, Mwanza huu sii utekaji? Hawa si ndio wanao fanya mambo ya wasio julikana? Kwanini watuhumiwa wasafirishwe usiku bila kjpewa taarifa au hata ndugu na marafiki kujulishwa?

Polisi watoke hadharani wajibu hizi shutuma. Tuna hitaji utawala wa sheria na sio utawala wa kimabavu..
 
Relax,

uhalifu na mipango mikakati ya kihalifu kwa mgongo wa kufanya siasa au mikutano ya hadhara inayohatarisha umoja amani na utulivu wa wananchi havitavumiliwa hata sekunde moja.

magenge ya kihalifu yatadhoofishwa, yatadhibitiwa, yatasambaratishwa na kwakweli yatatokomezwa kabisa bila kuzingatia maoni ya wahalifu wenyewe 🐒
 
Back
Top Bottom