TANZIA John Nyerere afariki dunia

TANZIA John Nyerere afariki dunia

Haka ka Steve Nyerere na kenyewe ni katoto ka Familia hii ya Mwalimu au
 
pole nyingi sana wafiwa , ukiacha makosa ya kibinadamu , hakika Nyerere alikuwa mzalendo halisi , mpaka leo familia yake inatibiwa Muhimbili , bali mafisadi wengi wa chama alichokianzisha hutibiwa INDIA , ULAYA NA AMERICA .

Yaani hata majina yawanawe siyajui zaidi ya huyo makongoro
 
MAMIA ya wakazi wa Dar es Salaam leo wanatarajia kutoa heshima za mwisho kwa John Nyerere (58), ambaye ni mmoja wa watoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

John alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alikokuwa amelazwa.Makongoro Nyerere ambaye ni mtoto mwingine wa Mwalimu Nyerere, alisema Dar es Salaam jana kuwa mwili wa John utasafirishwa kesho kwenda Mwanza na kisha kupelekwa kijijini kwao Butiama Mkoa wa Mara kwa maziko.

"Misa ya kumuombea John itafanyikahapa Msasani nyumbani kwa Mwalimu na kufuatiwa na utoaji wa heshima za mwisho," alisema Makongoro, ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

John alitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na alishiriki Vita vya Kagera vya 1978 na 1979, vilivyolenga kumng'oa nduli Iddi Amin wa Uganda.

Watoto wengine wa Mwalimu ni Andrew, Magige, Madaraka, Anna na Rose.


Chanzo:
Habari Leo
 
Mbona Jackton Manyerere alisema jana kwamba mmeishafika Butiama kwa ajili ya mazishi keshokutwa
 
R.I.P John.

Utaendelea kuishi maana maisha ya binadamu waliofanya 'fujo' zao duniani kwa manufaa ya wengine si kiwiliwili pekee. Ni yale aliyofanya wakati akiwa hai.

Utakumbukwa daima.
 
Nakumbuka story za John tangu akiwa mwanafunzi wa Mkwawa sekondari. Alikuwa toto tundu na kumlazimisha JK akampigie magoti mwalimu mkuu kuepusha mwanae John asifukuzwe shule.

Likawa somo kubwa sana kwa viongozi kwamba heshima kwa taratibu za shule iheshimiwe. Mwalimu mkuu alipandishwa cheo kwa kumfukuza John badala ya mategemeo ya wengi kwamba rais angemfukuza.

Siku hizi watoto wa wakubwa hawaguswi kuepusha zari kwa wakuu wa shule hizo kuchomekewa kila aina ya adha. Very intelligent John alikuwa kioo cha wanafunzi wenye kupenda kujifunza kwa matukio ya John na usomaji wake.

RIP John.
 
Mungu amlaze mahali pema peponi. Ni dhahiri watoto wa mwalimu hawataki makuu! Kafa akiwa mtanzania halisi.
 
Back
Top Bottom