Jonas Mkude aishtaki Mohammed Enterprises kwa kutumia picha yake bila idhini, adai fidia Tsh. Bilioni 1

Jonas Mkude aishtaki Mohammed Enterprises kwa kutumia picha yake bila idhini, adai fidia Tsh. Bilioni 1

View attachment 2793697

Mchezaji wa Klabu ya Yanga, Jonas Mkude amefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiidai Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) fidia ya Sh 1 bilioni kwa kutumia picha zake katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram na Twitter (sasa X) bila idhini yake.

Mkude amefungua kesi ya madai 192 ya mwaka 2023 mbele ya Jaji Butamo Philip dhidi ya kampuni hiyo akiidai fidia hiyo Kwa kuvunja haki yake ya msingi.
Amepata mwalimu mzuri sana ila kipindi cha kwenda kupimwa mkojo hakufungua mashitaka
 
View attachment 2793697

Mchezaji wa Klabu ya Yanga, Jonas Mkude amefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiidai Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) fidia ya Sh 1 bilioni kwa kutumia picha zake katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram na Twitter (sasa X) bila idhini yake.

Mkude amefungua kesi ya madai 192 ya mwaka 2023 mbele ya Jaji Butamo Philip dhidi ya kampuni hiyo akiidai fidia hiyo Kwa kuvunja haki yake ya msingi.
Aaaaahaa
 
Huyu kijana anatumiwa vibaya,,,,

Picha alipiga akiwa na jezi ya Simba as team "Group" na Melt wanamkataba na Simba sc ,,so yeye aende mahakamani akaombe tafsiri ya mkataba wake na Simba but I know that mkataba wa kwanza wa mkude na Simba una mfanya image yake kusalia Mali ya Simba forever...
Mwache ajichanganye si alisain mkataba ilimradii
Kumbe Real Madrid sasa hivi wanaweza mtumia Benzema kwenye matangazo! nlikua sijui
 
Anatafuta za kunywea pombe. Mambo ya hakimiliki unapoteza haki zako kama umejiuza kwa kusaini mkataba. Hata Diamond anaweza akautumia wimbo wa Harmonize aliouimba wakati akiwa chini ya lebo ya Wasafi
 
akiwa katika jezi zao anatumika vizuri kabisa. Ingia kwenye Channel ya MUTD (Man United) utakuta wanafanya biashara na kuingiza hela kwa kuonyesha mechi za enzi za akina Giggs na Porbosky
Mechi sawa nafahamu maana zina copyright nazunguzia image, mfano Man U sasa hivi wanaweza tengeneza tangazo kwa kutumia image ya Lukaku? Nb:mimi sio mjuzi wa hayo mambo
 
Back
Top Bottom