Jonas Mkude aishtaki Mohammed Enterprises kwa kutumia picha yake bila idhini, adai fidia Tsh. Bilioni 1

Jonas Mkude aishtaki Mohammed Enterprises kwa kutumia picha yake bila idhini, adai fidia Tsh. Bilioni 1

[emoji599] JUST IN: Kiungo wa Yanga, Jonas Mkude amefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiidai kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) fidia ya Sh 1 Bilioni kwa kutumia picha zake katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram na Twitter bila idhini yake. [[emoji2786] Mwanaspoti]

[emoji15]
View attachment 2793797
Inahitajika elimu khs IRC kwa wachezaji wetu na mawakala /ma menej wao
 
MeTL wamekuwa wakitumia picha ya Mkude kibiashara kitambo sasa.

Tena kinyume na taratibu za kikanuni za hadhi ya wachezaji.

Mwana amekaa na Mwanasheria wake wamegundua kuwa picha zile zimemuingizia Mo kiasi kikubwa sana cha pesa sawa na Bilioni 1 za kitanzania.

Kama vile tulivyo msaidia Feo Toto apate haki yake, ninawaasa wadau tuunge mkono jitihada za Mkude. Tutambue kuwa mpira ndio kazi yao.
IRC lipo ktk mikataba yao? Ila image ya mchezaji huwa ni ya club na inatakiwaa iwe sehemu ya mkataba kuwa ,image ya mchezaji itatumika na mdhamimini
 
Kwa sisi watu wajasiriamali tunaobeti ukijiunga na kampuni ya kuweka madau (bookmark), kwa kitendo chako cha kujisajili tu maana yake umekubali vigezo na masharti yote ya kampuni.

Sasa ukijipa muda wa kupitia vigezo na masharti kwa bookie walio wengi wana kipengele hiki au kinachofanana na hiki hapa chini;

Iwapo utashinda pesa nyingi, kampuni itakutaka kupiga picha ambayo itakuwa mali ya kampuni. Kampuni itakuwa na haki ya kutumia picha hiyo kwa mwaka mzima katika matangazo na promosheni mbalimbali za kampuni.

Iwapo utakataa kupigwa picha, kampuni ina haki ya kutokukupa kiasi hicho cha ushindi. Kiasi hicho kitajumlishwa mwisho wa mwaka kama mapato halali ya kampuni.

Usikute ndugu yetu aliingia mikataba ya namna hii tunayoingia watu tunaobeti bila kusoma.
 
Huyu kijana anatumiwa vibaya,,,,

Picha alipiga akiwa na jezi ya Simba as team "Group" na Melt wanamkataba na Simba sc ,,so yeye aende mahakamani akaombe tafsiri ya mkataba wake na Simba but I know that mkataba wa kwanza wa mkude na Simba una mfanya image yake kusalia Mali ya Simba forever.

Mwache ajichanganye si alisain mkataba ilimradii
Sijui labda kwasababu sina utaalamu wa sheria kwamba kwasababu Joti alikuwa tiGO na mkataba na sasa yupo Airtel,wale tiGO wataendelea kutumia image yake forever kwasababu alisaini mkataba? Kuna mkataba usio na kikomo? Ngoja vijana wale wachache wanaofaulu pale mawasiliano waje
 
MeTL wamekuwa wakitumia picha ya Mkude kibiashara kitambo sasa.

Tena kinyume na taratibu za kikanuni za hadhi ya wachezaji.

Mwana amekaa na Mwanasheria wake wamegundua kuwa picha zile zimemuingizia Mo kiasi kikubwa sana cha pesa sawa na Bilioni 1 za kitanzania.

Kama vile tulivyo msaidia Feo Toto apate haki yake, ninawaasa wadau tuunge mkono jitihada za Mkude. Tutambue kuwa mpira ndio kazi yao.
Upo sahihi sana
 
Kama thamani ya mtu haipimwi kisheria unaweza kuniambia kwanini Mkude anaenda mahakamani?

Kipi kilichomfanya mkude aweke demand ya 1B?

Anaenda mahakamani kudai fidia ya 1B, je alidhulumiwa?

1B anayodai ilitokana na mauziano ya bidhaa gani ?

Nini kilichomfanya afikiri 1B ndio kiwango sahihi anachostahili kulipwa?

Kama sio ishu inayo determine thamani ya mtu unaweza kuniambia kwanini haku demand laki 1 au 50,000?
Ukiona mru anadai kiasi fulani kwa case kama hiyo ya Jonas maana yake hay9 ni makadirio ya kiasi cha pesa kinachoweza kuwa kimepatikana kutokana na picha yake kuwepo mahali pale lakini haina maana muhusika ana thamani hiyo.
 
Huyu kijana anatumiwa vibaya,,,,

Picha alipiga akiwa na jezi ya Simba as team "Group" na Melt wanamkataba na Simba sc ,,so yeye aende mahakamani akaombe tafsiri ya mkataba wake na Simba but I know that mkataba wa kwanza wa mkude na Simba una mfanya image yake kusalia Mali ya Simba forever.

Mwache ajichanganye si alisain mkataba ilimradii
Hana akili. Anadhani dewj atamkamata. Wacha ajichanganye afu akishindwa anafunguliwa kesi ya kuichafua kampuni ya metl na fidia ni hiyo hoyo bilion sijui ata lipiwa na nani
 
View attachment 2793697

Mchezaji wa Klabu ya Yanga, Jonas Mkude amefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiidai Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) fidia ya Sh 1 bilioni kwa kutumia picha zake katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram na Twitter (sasa X) bila idhini yake.

Mkude amefungua kesi ya madai 192 ya mwaka 2023 mbele ya Jaji Butamo Philip dhidi ya kampuni hiyo akiidai fidia hiyo Kwa kuvunja haki yake ya msingi.
Mawakili kanjanja wamemwingiza Chaka
 
Back
Top Bottom