Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 3,558
- 7,935
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jonh Heche, amedai kuwa tangu aachiwe huru na Jeshi la Polisi amekuwa akifuatilia pasipoti yake ya kusafiria bila mafanikio.
Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa X (zamani Twitter), Heche amesema pasipoti hiyo ni muhimu kwa ajili ya safari ya kwenda kupata matibabu, lakini hadi sasa haijarejeshwa bila kupewa sababu yoyote ya kisheria.
“Wiki nzima tangu niachiwe na polisi, nimekuwa nikidai pasipoti yangu ili nisafiri kwa ajili ya kupata matibabu bila mafanikio. Hakuna sababu yoyote ya vyombo vya dola kuendelea kushikilia pasipoti yangu. Nafanyiwa haya kwa sababu ya msimamo wangu wa kisiasa,” ameandika.
Heche amesema ameamua kulifikisha suala hilo kwa umma ili Watanzania na jamii ya kimataifa wafahamu kile anachokiita ukandamizaji wa haki yake ya msingi ya kusafiri na kupata huduma za kiafya.
#D9