Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Hali mbaya waliyonayo wapalestina wa maeneo yote hakukuwa na haja ya matumizi ya diplomasia na ahadi za mazungumzo.Ilikuwa ni kuchukua maamuzi sambamba na ukatili unaofanywa na serikali ya Israel kwa wapalestina wanyonge.
Kinyume chake seikali ya mfalme Abdallah wa Jordan imemuita nyumbani balozi wake nchini Israel kama ni kutoridhishwa na mashambulizi ya jeshi la IDF huko Gaza. Saudia nayo imeelezwa kuwa imetoa onyo kali kwa Israel kutokana na kushambulia kambi ya wakimbizi ya Jabaliya kwa siku mbili mfululizo na kuuwa jumla ya watu 195 na huku wengine 120 ikikisiwa bado wamefunikwa na kifusi.
Upande wa ukingo wa mashariki na mashariki ya Jerusalem tangu kuanza vita na shambulio la Hamas kumekuwa na ongezeko la mashambulizi kwa raia wa Palestina kutoka maadui watatu.
Kwanza wanapigwa na walowezi wa kiyahudi waliopenyezwa katikati yao waliojengewa nyumba kwa lazima na kupewa silaha kila mmoja.Walowezi hawa huwa wanawapiga bila huruma kwenye majumba na kwwenye mashamba wanapokwenda kulima.
Adui wa pili ni jeshi la Israel ambalo linatumia ndege za kivita kupiga maeneo yao na misikiti bila kubagua kati ya makundi ya wapalestina wanaounga mkono Gaza au walioamua kukaa kimya kwa ahadi ya kupewa serikali vita vikiisha.
Adui wa tatu ni hiyo serikali ya Mahmoud Abbas ambayo pamoja kuzingirwa bado tu wamehadaika kuja kupewa serikali.Askari wa PLO kwa jina la sultah huwa wanawapiga wapalestina wenzao wanaolalamika kwa kuandamana kupinga vita Gaza na hapo kwao.
Kuona hivyo vijana wa kipalestina sasa wameamua kushika silaha na kuanza kuwatishia askari wa Mahmoud Abbas wanaowazuia wasilie kwa vipigo wanavyopigwa na IDF.
“When things get beyond the limit, it’s a problem,” said Abu Mohammad, 33. “When you pressure us, there will be an explosion. We’re facing both Israel and the Sultah.”
Maamuzi ya wapalestina wa Jenin yanalingana na wananchi wa mataifa ambayo katika miaka michache iliyopita walirudisha uhusiano na taifa la Israel..Wananchi katika nchi hizo wameendelea na vuguvugu la kupinga wazi wazi uhusiano huo hasa baada ya kuona jinsi vita vinavyoendelea kwenye maeneo ya wapalestina.