Hakuna kitu kibaya kutendea akili, nafsi na roho kama ku judge jambo kwa hisia, tamaa, hulka, silka, chuki na wivu.
Ina maana mnataka kusema kikosi cha Man U ni bora zaidi ya kikosi cha Man City?
Mnataka kusema kikosi cha Man U ni bora zaidi ya kikosi cha Liverpool?
Kikosi cha Man U ni bora zaidi ya kikosi cha Chelsea?
Ina maana mnataka kusema mmekwisha sahau Mou wa Porto? Porto kulikuwa na wachezaji gani?
Mmekwisha sahau Mou wa Chelsea? Aliyeleta Chelsea toka uvunguni hadi kwenye timu ya kuchukua mikoba?
Mmekwisha sahau Mou wa Inter Millan aliyechukua treble huku akiwatoa Barca wakiwa kwenye ubora wao wa karne?
Mmekwisha sahau Mou wa Man U yule aliyekuja msimu wa kwanza kasajili wachezaji watatu tu kachukua Europa, Community Shield, n.k. msimu wa kwanza?
Mmekwisha sahau Mou yule msimu uliopita alipeleka Man U nafasi ya pili ligi kuu, nafasi ambayo Man U haijawahi kufika tangu Sir Alex astaafu?
Mmekwisha sahau kuwa Klop, Pochetino wote walikuwa England muda tu lkn hadi sasa hawana hata bakuli sembuse kombe?
Mmekwisha sahau kwamba msimu uliopita kama sio Man city walio kwenye ubora mkubwa basi kombe la ligi likeenda Man U? Akina Klop, Conte na Pochetino walikuwa wapi?
Ina maana mmekwisha sahau namna Mou alivyokuwa analialia kuhusu kupatiwa walau mchezaji mmoja tu beki?
Ina maana hamuoni namna Man City, Liverpool na Chelsea wanavyofanya manunuzi?
Ina maana mmekwisha sahau kauli ya Ed Woodward kwamba matokeo ya Man U uwanjani hayana athari zozote za kibiashara (na hiki ndicho kilichofanya pasiwepo usajili wa maana msimu huu)
Makosa yanayofanywa na mabeki wa Man U ni ya Mou?
Ok. Tuseme hayo yamepita kwenu hayana maana tena. Sasa, kama mshabiki wa Soka wewe unadhani ukipewa hicho kikosi cha Man U cha sasa utafika nacho wapi????
Kwa waelewa wa soka, mtakubalina nami kuwa Ed Woodward ndio chanzo cha ubovu wa Man U. Lazima alipokuwa Gill David na Sir Alex mambo yalikuwa yanaenda vizuri kabisa.
Na kwa kuona hilo ndio maana wanamtafuta Sporting Director ambaye yeye atakuwa anajihusisha na usajili tu na Ed Woodward kujihusisha na masuala ya commercial ya club maana anashindwa kumudu nafasi zote mbili kwa mpigo.
Na ndio maana fans wa Man U mechi ya juzi waliwa pigia makofi mengi sana wachezaji pamoja na Mou japo game walipoteza. Hii ni kwa sababu wanaelewa wazi wapi tatizo la timu lipo.
Na kwa wafuatiliaji wa soka la ushindani, Man U kumuondoa Mou pale watakuwa na options chache sana za kupata makocha bora.
Mou bado ni kocha bora sana. Man U wanashindwa kukubaliana na wakati, kwamba soka la leo ni pesa. Beki ghali zaidi duniani yupo Liverpool, Golikipa ghali zaidi duniani yupo Liverpool na Chelsea, n.k. n.k
Punguzeni wivu na chuki binafsi.