Joseph Haule (Prof. Jay): Sasa nipo Imara, Namshukuru Rais Samia, Mbowe, Watanzania na Familia. See you soon

Joseph Haule (Prof. Jay): Sasa nipo Imara, Namshukuru Rais Samia, Mbowe, Watanzania na Familia. See you soon

Mkuu kama ana ukimwi au ugonjwa mwingine si hadi yeye au daktari wake athibitishe?

Wagonjwa wengi wa moyo, pressure, cancer nk wanasema wazi kuwa wanaumwa, kama mtu hajasema kwa nini mzushe vitu hamna uhakika navyo?

Hoja hapa ni mtu kuja kujipa mamlaka ya kutangaza ugonjwa wa mwenzake wakati sio daktari wake, sio mwanafamilia wala mtu wa karibu. Huyo Victoire anadai ni Dr ila anaropokwa hovyo, hana ethics.
mkuu nafikiri ni dhana na hofu tu na labda unafiki wetu watz kuhusu ukimwi...mm sijawahi kusikia watz hata kumi kuanzia wagonjwa wenyewe hata ndugu zao wakisema wanaumwa au wamekufa kwa ukimwi but hayo magonjwa mengine yote tunayasema bila hofu yoyote..inashangaza sana kuogopa kusema ukimwi wakati statistics zinaonesha tuna waathirika zaidi ya 1.7miln..sasa hawa watu hawaumwi wala kufa?.hii taboo ya kuona ukimwi kama kitu kibaya sana na hakipo wakati ni ugonjwa kama malaria, cancer, TB, etc nadhani sio sahihi...au kwakuwa fikra ni kuwa ugonjwa unaotokana na tabia mbaya?sasa si bora kusema tu ili wengine wajue upo na kuacha!
 
Huyu jamaa, naona bado hajapona vizuri.

Halafu mbona kakonda sana?

Wazee wa ramli chonganishi, vibuyu vinasemaje huko?

====

Salaam Ndugu zangu,
View attachment 2607620
Kwanza namshukuru sana Mungu aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai. Hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu).

Pili Kipekee namshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu Dr. Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na Nje ya Nchi.

Asante sana Mama pamoja na serikali yako yote, kwani viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji.

Tatu, namshukuru sana Mwenyekiti wa chama changu cha CHADEMA Kamanda Mbowe, Wanachama na Viongozi wote Waandamizi wa chama kwa jitihada zao za kuhakikisha napata matibabu bora zaidi kwa kushirikiana na serikali.

Zaidi nawashukuru sana Madaktari na Manesi wote wa Muhimbili na kote nilikopitia kwa kunipa matibabu ya kiwango cha juu kwa zaidi ya mwaka mzima niliolala hapo Muhimbili, hasa zile siku 127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa uwezo wenu wote kuhakikisha kuwa mnaokoa uhai wangu, ahsanteni sana.

Mwisho na kwa umuhimu mkubwa sana nawashukuru sana Watanzania wote mliojitolea kwa maombi na michango ya fedha zenu kuhakikisha natibiwa na kusema ukweli ilinisaidia sana kulipa bills za awali kabla ya Serikali kuamua kuingilia kati na kuubeba mzigo huu asanteni sana na sitowasahau.

Shukrani sana kwa Malisa GJ na Lyenda kwa kusimamia michango hiyo pamoja na vyombo vyote vya habari na social media nchini vilivyoshirikiana navyo kama Clouds FM, Millard Ayo, Wasafi FM na vyombo vingine mbalimbali pamoja na Watumishi wa Mungu wote walioongoza ibada maalum ya kuniombea, Mungu awabariki sana.

Kuanzia Wachungaji, Mashekh na Mapadre wote wa kanisa langu Katoliki sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea Mungu awabariki sana.

Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoishukuru familia yangu, mke wangu, kaka zangu, dada zangu, wadogo zangu na familia yote ya Mzee Haule kwa ushirikiano mkubwa na upendo mlionipa.

Kwa sasa nipo imara na ninaendelea vizuri sana, Mungu ni mwema sana siku zote🙏🏻🙏🏻🙏🏻.

Ahsanteni,
Joseph Haule (Prof. Jay)
#MgodiUnaotembea
#SeeYouSoon❤️❤️❤️❤️
Mwamba bado anaumwa aisee! Mpaka sura imebadilika!
 
mkuu nafikiri ni dhana na hofu tu na labda unafiki wetu watz kuhusu ukimwi...mm sijawahi kusikia watz hata kumi kuanzia wagonjwa wenyewe hata ndugu zao wakisema wanaumwa au wamekufa kwa ukimwi but hayo magonjwa mengine yote tunayasema bila hofu yoyote..inashangaza sana kuogopa kusema ukimwi wakati statistics zinaonesha tuna waathirika zaidi ya 1.7miln..sasa hawa watu hawaumwi wala kufa?.hii taboo ya kuona ukimwi kama kitu kibaya sana na hakipo wakati ni ugonjwa kama malaria, cancer, TB, etc nadhani sio sahihi...au kwakuwa fikra ni kuwa ugonjwa unaotokana na tabia mbaya?sasa si bora kusema tu ili wengine wajue upo na kuacha!

Nachokiona kwa jamii yetu kuna watu bado wapo na tabia za unyanyapaaji ndio mana hata kama mtu ana hiyo shida wengi hawapendi kuweka wazi. Kwanza hakuna mwenye uhakika kama ni umeme kweli ama vipi na pia hata kama ni kweli si vyema kumtangaza kama mwenyewe hajataka iwe wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Malizia kabisa "Single mother, nina hela,sina Ukimwi na sitakufa " ili at least ushtue common sense , you seems to be lacking one !
Mazuri yote duniani ni blessings, na mabaya pia ni blessings .
Idea nzima ya maisha ipo so complicated, na hakuna guarantee ya chochote.
Sitakufa bali nitaishi ili niyasimulie matendo makuu ya Bwana. Nitakufa nikifikisha 95 yrs huko.
 
Back
Top Bottom