Joseph Haule (Prof. Jay): Sasa nipo Imara, Namshukuru Rais Samia, Mbowe, Watanzania na Familia. See you soon

Joseph Haule (Prof. Jay): Sasa nipo Imara, Namshukuru Rais Samia, Mbowe, Watanzania na Familia. See you soon

Ukoje aisee na sie tupate kujikinga
Huu unasababishwa na kuka mda mrefu na mkojo hii ni moja ya sababu ambayo watu wengi hukutwa

Dalili miguu kuvimba

Dialysis yake moja ilikuwa 120000 now wamepunguza baada ya kuona watz wengi hawawezi kulipia iyo na mwisho kupoteza maisha bodi ikakaa ikaona wapunguze iwe 100000 kuna baadhi wakati ipo bei ya zaman waliomba kupunguziwa gharama za matibabu kutokana na uchunguzu ulio fanywa mgonjwa akikutwa kweli kuwa ana staihili basi wapo walio pata mpaka 30000 lakiini wengine unakuta ombi lao la kukubaliwa kulipa ivyo huku wamekufa teyari

Kwahiyo kwa mtanznia wa kawaida anae umwa figo kupona ni kazi labda Mungu apende kulipia kwa wiki laki mbili ili wachuje figo kwa watz wengi bado hawamudu ndio maana nasema kama huna pesa unakufa
 
Anaandika Mh. Professor Jay

Salaam Ndugu zangu,

Kwanza namshukuru sana MUNGU aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai, Hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, Asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu).

Pili Kipekee namshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Dr. Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na Nje ya Nchi ,Asante sana Mama pamoja na serikali yako yote kwani viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji.

Tatu namshukuru sana Mwenyekiti wa chama changu cha CHADEMA Kamanda FreemanMbowe ,Wanachama na viongozi wote waandamizi wa chama kwa jitihada zao za kuhakikisha napata matibabu bora zaidi kwa kushirikiana na serikali, Zaidi nawashukuru sana Madaktari na Manesi wote wa muhimbili na kote nilikopitia kwa kunipa matibabu ya kiwango cha juu kwa zaidi ya mwaka mzima niliolala hapo Muhimbili hasa zile siku 127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa uwezo wenu wote kuhakikisha kuwa mnaokoa uhai wangu ,AHSANTENI SANA.

Mwisho na kwa umuhimu mkubwa sana nawashukuru sana Watanzania wote mliojitolea kwa maombi na michango ya fedha zenu kuhakikisha natibiwa na kusema ukweli ilinisaidia sana kulipa bills za awali kabla ya serikali kuamua kuingilia kati na kuubeba mzigo huu asanteni sana na sitowasahau.

Shukrani sana kwa Malisa Gj na Lyenda kwa kusimamia michango hiyo pamoja na vyombo vyote vya habari na social media nchini vilivyoshirikiana navyo kama Cloudsfmtz Millardayo wasafifm na vyombo vingine mbalimbali pamoja na Watumishi wa Mungu wote walioongoza ibada maalum ya kuniombea MUNGU awabariki sana kuanzia Wachungaji, Mashekh na Mapadre wote wa kanisa langu Katoliki Sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea MUNGU AWABARIKI SANA.

Nitakuwa mchoyo wa Fadhila nisipoishukuru Familia yangu Mke wangu (Mke wangu) kaka zangu, dada zangu Wadogo zangu na Familia yote ya Mzee Haule kwa ushirikiano mkubwa na upendo mliomipa.

Kwa sasa nipo imara na ninaendelea vizuri sana Mungu ni mwema sana siku zote🙏🏻🙏🏻🙏🏻

Ahsanteni
Joseph Haule (Prof. Jay)
#MgodiUnaoTembea
 

Attachments

  • FB_IMG_1683051056801.jpg
    FB_IMG_1683051056801.jpg
    52.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom