Joseph Haule (Prof. Jay): Sasa nipo Imara, Namshukuru Rais Samia, Mbowe, Watanzania na Familia. See you soon

Joseph Haule (Prof. Jay): Sasa nipo Imara, Namshukuru Rais Samia, Mbowe, Watanzania na Familia. See you soon

Huyu jamaa, naona bado hajapona vizuri.

Halafu mbona kakonda sana?

Wazee wa ramli chonganishi, vibuyu vinasemaje huko?

====

Salaam Ndugu zangu,
View attachment 2607620
Kwanza namshukuru sana Mungu aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai. Hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu).

Pili Kipekee namshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu Dr. Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na Nje ya Nchi.

Asante sana Mama pamoja na serikali yako yote, kwani viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji.

Tatu, namshukuru sana Mwenyekiti wa chama changu cha CHADEMA Kamanda Mbowe, Wanachama na Viongozi wote Waandamizi wa chama kwa jitihada zao za kuhakikisha napata matibabu bora zaidi kwa kushirikiana na serikali.

Zaidi nawashukuru sana Madaktari na Manesi wote wa Muhimbili na kote nilikopitia kwa kunipa matibabu ya kiwango cha juu kwa zaidi ya mwaka mzima niliolala hapo Muhimbili, hasa zile siku 127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa uwezo wenu wote kuhakikisha kuwa mnaokoa uhai wangu, ahsanteni sana.

Mwisho na kwa umuhimu mkubwa sana nawashukuru sana Watanzania wote mliojitolea kwa maombi na michango ya fedha zenu kuhakikisha natibiwa na kusema ukweli ilinisaidia sana kulipa bills za awali kabla ya Serikali kuamua kuingilia kati na kuubeba mzigo huu asanteni sana na sitowasahau.

Shukrani sana kwa Malisa GJ na Lyenda kwa kusimamia michango hiyo pamoja na vyombo vyote vya habari na social media nchini vilivyoshirikiana navyo kama Clouds FM, Millard Ayo, Wasafi FM na vyombo vingine mbalimbali pamoja na Watumishi wa Mungu wote walioongoza ibada maalum ya kuniombea, Mungu awabariki sana.

Kuanzia Wachungaji, Mashekh na Mapadre wote wa kanisa langu Katoliki sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea Mungu awabariki sana.

Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoishukuru familia yangu, mke wangu, kaka zangu, dada zangu, wadogo zangu na familia yote ya Mzee Haule kwa ushirikiano mkubwa na upendo mlionipa.

Kwa sasa nipo imara na ninaendelea vizuri sana, Mungu ni mwema sana siku zote🙏🏻🙏🏻🙏🏻.

Ahsanteni,
Joseph Haule (Prof. Jay)
#MgodiUnaotembea
#SeeYouSoon❤️❤️❤️❤️
Mungu ni mwema sana, sifa na utukufu ni kwake, ubarikiwe sana!.
P
 
Single mother, nina hela,sina Ukimwi.
Malizia kabisa "Single mother, nina hela,sina Ukimwi na sitakufa " ili at least ushtue common sense , you seems to be lacking one !
Mazuri yote duniani ni blessings, na mabaya pia ni blessings .
Idea nzima ya maisha ipo so complicated, na hakuna guarantee ya chochote.
 
mkuu kwani huo ugonjwa wa ukimwi why ukitajwa ni lazima uhitaji ruhusa ya daktari?.mbona tunataja kila siku watu kuumwa cancer, BP, nimonia, kisukari, malaria, homa, etc bila ruhusa ya madaktari?.hayo yote si ni magonjwa?.au tofauti yake ni nini hasa hadi moja kuonekana linahitaji ruhusa ya dokta kulitaja?
Mkuu kama ana ukimwi au ugonjwa mwingine si hadi yeye au daktari wake athibitishe?

Wagonjwa wengi wa moyo, pressure, cancer nk wanasema wazi kuwa wanaumwa, kama mtu hajasema kwa nini mzushe vitu hamna uhakika navyo?

Hoja hapa ni mtu kuja kujipa mamlaka ya kutangaza ugonjwa wa mwenzake wakati sio daktari wake, sio mwanafamilia wala mtu wa karibu. Huyo Victoire anadai ni Dr ila anaropokwa hovyo, hana ethics.
 
Yaani achqngiwe lkn ugonjwa wake usitajwe? Waliochangia kwenye uzi huu wanasema mwamba ana ukimwi uliosababisha Figo kufeli. Kama madai haya siyo kweli leta ya kwako
Mimi sio daktari wake, sio ndugu yake wala sio rafiki yake. Nawezaje kuleta ugonjwa wa mtu nisiyemfahamu vizuri kwenye jamii tena bila ruhusa yake. Acheni uchawi ndugu zangu, huu ni uchawi.
 
Back
Top Bottom