Joseph Haule (Prof. Jay): Sasa nipo Imara, Namshukuru Rais Samia, Mbowe, Watanzania na Familia. See you soon

Joseph Haule (Prof. Jay): Sasa nipo Imara, Namshukuru Rais Samia, Mbowe, Watanzania na Familia. See you soon

Huyu jamaa, naona bado hajapona vizuri.

Halafu mbona kakonda sana?

Wazee wa ramli chonganishi, vibuyu vinasemaje huko?

====

Salaam Ndugu zangu,
View attachment 2607620
Kwanza namshukuru sana Mungu aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai. Hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu).

Pili Kipekee namshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu Dr. Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na Nje ya Nchi.

Asante sana Mama pamoja na serikali yako yote, kwani viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji.

Tatu, namshukuru sana Mwenyekiti wa chama changu cha CHADEMA Kamanda Mbowe, Wanachama na Viongozi wote Waandamizi wa chama kwa jitihada zao za kuhakikisha napata matibabu bora zaidi kwa kushirikiana na serikali.

Zaidi nawashukuru sana Madaktari na Manesi wote wa Muhimbili na kote nilikopitia kwa kunipa matibabu ya kiwango cha juu kwa zaidi ya mwaka mzima niliolala hapo Muhimbili, hasa zile siku 127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa uwezo wenu wote kuhakikisha kuwa mnaokoa uhai wangu, ahsanteni sana.

Mwisho na kwa umuhimu mkubwa sana nawashukuru sana Watanzania wote mliojitolea kwa maombi na michango ya fedha zenu kuhakikisha natibiwa na kusema ukweli ilinisaidia sana kulipa bills za awali kabla ya Serikali kuamua kuingilia kati na kuubeba mzigo huu asanteni sana na sitowasahau.

Shukrani sana kwa Malisa GJ na Lyenda kwa kusimamia michango hiyo pamoja na vyombo vyote vya habari na social media nchini vilivyoshirikiana navyo kama Clouds FM, Millard Ayo, Wasafi FM na vyombo vingine mbalimbali pamoja na Watumishi wa Mungu wote walioongoza ibada maalum ya kuniombea, Mungu awabariki sana.

Kuanzia Wachungaji, Mashekh na Mapadre wote wa kanisa langu Katoliki sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea Mungu awabariki sana.

Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoishukuru familia yangu, mke wangu, kaka zangu, dada zangu, wadogo zangu na familia yote ya Mzee Haule kwa ushirikiano mkubwa na upendo mlionipa.

Kwa sasa nipo imara na ninaendelea vizuri sana, Mungu ni mwema sana siku zote[emoji1317][emoji1317][emoji1317].

Ahsanteni,
Joseph Haule (Prof. Jay)
#MgodiUnaotembea
#SeeYouSoon[emoji3590][emoji3590][emoji3590][emoji3590]
Yaani yeye mwenyewe kasema yupo imara. Halafu wewe ulivyo mjinga unasema hajapona vizuri.
Unashangaa kukonda wakati alikuwa anaumwa?
Kupungua mwili ni afya sana.
 
Bro!

Tafadhali weka mahaba pembeni changia ukiwa na akili huru za utu,maisha ya matibabu Tanzania ni mabaya sana usiombe yakukute hasa uwe huna hela.

Naandika haya nimeshuhudia yupo mtu anakosa 500/= ya kununua paracetamol atulize maumivu ili ajue aende akafie wapi na yupo duka la dawa la serikali na hakuna anayemsikiliza,mimi sina roho mbaya kwamba sitaki Jay apone nazungumza uhalisia wa maisha ya Mtanzania wa hali ya chini yule asiyeijua leo yake ataiishi vipi.
Sasa mtu kukosa pesa ya panadol wataka ilaumiwe serikali?
 
Sitakufa bali nitaishi ili niyasimulie matendo makuu ya Bwana. Nitakufa nikifikisha 95 yrs huko.
Kwa atttude yako hata ufikishe miaka 100 bado hutainjoi maisha , umejaa visasi na unafurahia sana mahangaiko ya watu. kama umeokoka basi dini huenda ina watu wa hovyo na wanafiki kupitiliza .
Kuna uzi ulikuwa unafurahia kuliona kaburi la mumeo , hapa unatangaza makuu ya bwana.
 
Sipendi kusema watu lakini mdomo wake umelika kwasababu ya pombe. Ujumbe hapa ukifika miaka 40 jitahidi achana na pombe za kuzidi, sukari, vyakula vya wanga, fanya mazoezi na medical check up!. Bila kuelezana ukweli na vitu vilivyo changia tatizo lakini hatuta tenda haki kutoa elimu ya afya. Pole sana Prof Jay
Mkuu hii ndio dawa na ukweli ambao wengi hawataki kuusikia.
 
Sipendi kusema watu lakini mdomo wake umelika kwasababu ya pombe. Ujumbe hapa ukifika miaka 40 jitahidi achana na pombe za kuzidi, sukari, vyakula vya wanga, fanya mazoezi na medical check up!. Bila kuelezana ukweli na vitu vilivyo changia tatizo lakini hatuta tenda haki kutoa elimu ya afya. Pole sana Prof Jay
Unataka kusema alikuwa anakunywa pombe katika kipindi chote cha mwaka mzima akiwa kitandani?.
Kwa nini usiseme dawa zimemfanya mdomo kuwa hivyo?
Tuache ujuaji
 
Kwa atttude yako hata ufikishe miaka 100 bado hutainjoi maisha , umejaa visasi na unafurahia sana mahangaiko ya watu. kama umeokoka basi dini huenda ina watu wa hovyo na wanafiki kupitiliza .
Kuna uzi ulikuwa unafurahia kuliona kaburi la mumeo , hapa unatangaza makuu ya bwana.
Wewe nawe,nilisema wapi ninafurahia?Nilisema now iam sure mme wangu yupo wapi.Sio kama zamani unaambiwa ninakwenda Mwanza,kumbe mtu yupo Serena hotel. Ninaongea facts.
 
Zile karanga wanameza kila kila siku naskia ni hatari sana...halafu zinaleta hasira sana..
Mtu wa ngwengwe unaweza kumuomba akupishe tu upite akakutolea povu hutaamini!!
Wana hasira sana,inabidi kuwaelewa tu.Akikuwekea hasira wewe mchukulie poa tu.Si yeye ni Madawa. Ila asante Mungu kuna hizo dawa,maana watu wangekufa sana.Dawa zimesaidia sana.
 
Back
Top Bottom