Joseph Mbilinyi: Prof Kabudi ashitakiwe kwa kulidanganya taifa juu ya tril 360. Aliunga mkono udikteta enzi za hayati

Joseph Mbilinyi: Prof Kabudi ashitakiwe kwa kulidanganya taifa juu ya tril 360. Aliunga mkono udikteta enzi za hayati

Kwa mazingila ya wakati ule, tutakuwa tunamuonea bure Kabudi. Hali ilikuwa tete. Hata wale waliokuwa WANAUNGA MKONO JUHUDI, haikuwa kutoka moyoni. Mkamia naye, alishatoa ushuhuda wa yule Bwana, alivyokuwa hatari!
Kuna watu bado walibaki na misimamo yao na hawakuunga juhudi.
 
Nadhani Mh. Sugu amepungukiwa hekima. Hakupaswa kutoa kauli chochezi namna hii ktk hiki kipindi. Sijui tu kwa nini watanzania wengi ni wagumu kuelewa. Mungu ambariki sana Prof. Kabudi.
Unachekesha sana.Hivi ulitegemea Sugu asemeje?Unajua maumivu waliyoyapata wakati wa hilo sakata?Unajua?Tulia.
 
Wazee wa kudandia matukio wamesnza sasa!
Dhambi ina tabia ya kuitesa nafsi.Muache Kabudi autue mzigo.Anajua kwa maneno yake na ripoti ya makinikia ni kwa namna gani kuna watu waliumia.Ni namna ya kutubu na kujutia ubaya)dhambi.Bora amesema mwenyewe akiwa hai.
 
Sugu ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter "Kwa jinsi hii, huyu mzee anatakiwa awe ‘held accountable’ kwa kulidanganya Taifa kama anavyokiri hapo… Huyu mtu ana rekodi ya ovyo sana serikalini na ni mmoja wa watu waliokuwa wakichochea udikteta (Henchmen) kwenye awamu ya Mwendazake…"

Na ameambatanisha picha ya Gazeti la Jamhuri

View attachment 2377124

View attachment 2377108
Ondoa hiyo nembo ya CDM hapo wewe kenge. Tunakujua!!
 
hivi sugu aliishia darasa la ngapi?
Ujinga ni pamoja na kutotambua hata kinachojadiliwa. Hoja ni uwongo wa Kabudi, elimu ya Sugu unaweza kuipata hata kwenye website ya Bunge.
 
Kwa mazingila ya wakati ule, tutakuwa tunamuonea bure Kabudi. Hali ilikuwa tete. Hata wale waliokuwa WANAUNGA MKONO JUHUDI, haikuwa kutoka moyoni. Mkamia naye, alishatoa ushuhuda wa yule Bwana, alivyokuwa hatari!
Tukiendelea kutoa visingizio vya kutowajibisha watu eti kwa vile walilazimika, Taifa halitakuja kubadilika. Mara zote tutakuwa na watendaji wanafiki, waongo, majuha na machawa wa watawala.
 
Ujinga ni pamoja na kutotambua hata kinachojadiliwa. Hoja ni uwongo wa Kabudi, elimu ya Sugu unaweza kuipata hata kwenye website ya Bunge.
Kwani kunasehemu kabudi kasema ni uwongo?
 
Unamshitaki Profesa Kabudi kwa kosa gani?Kabudi yeye alikuwa anaendesha majadiliano ya matokeo ya ripoti ya Mruma na Osoro ambapo TRA ndiyo waliokokotoa Kodi, penalty nk na kuja na value ya Dola bilioni 190.
Sasa tuwashitaki wataalaamu wa TRA waliompa Kabudi amount isiyo sahihi au tumshitaki Kabudi kwasababu aliongoza majadiliano ambapo tuliambulia kupata kijimnofu kwenye mapato ya madini kupitia Twiga Minerals Corporation Limited (mwaka 2021/2022 serikali imepata mgao wa Tshs bilioni 82) plus kushika uchumba cha bilioni 700 na mengine neyo!
Hati ya mashitaka ya Profesa Kabudi itaandikwaje?Mimi naona kuwatikisa Barrick kumeambulia kidogo kuliko tulivyokuwa hapo awali,nadhani tusubiri Rais mwingine mwenye akili kama Magufuli ili aendeleze mapambano,hizi chawa za Msoga ziache ziendelee na ngonjela.
 
Waliosema tutashtakiwa Miga na tukalipwa hzo 7bln , ndo washtakiwe.
 
Tutashtakiwa MIGA
553206636.jpg
 
Ujinga ni pamoja na kutotambua hata kinachojadiliwa. Hoja ni uwongo wa Kabudi, elimu ya Sugu unaweza kuipata hata kwenye website ya Bunge.
mjinga hawezi kutambua msingi wa swali langu.
 
Back
Top Bottom