HAKI KWA WOTE
JF-Expert Member
- Nov 30, 2022
- 1,108
- 1,132
Afe tu mtuondelee siasa uchwala tangu muanze kupigania madaraka na maisha bora kwa watanzania hatuoni lolote,kelele tu na kujenga mahotel
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haya majitu ni mashetani.Mliosema mama muungwana anapenda demokrasia mpo wapi tuwaone...
Hapo sasa ndio tunajenga upinzani wa kweli hutosikia kauli zile "NARUDI NYUMBANI"SUGU YUPO MAHUTUTI HOSPITALI,DAR ES SALAAM.
1.Sugu anaongea kwa taabu sana na Sauti ya chini sana, kutoka Hospitali binafsi aliyopelekwa leo asubuhi.
2.Sugu alivamiwa na kupigwa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Awadhi binafsi siyo kwa kutuma askari wa chini,
Kuanzia nje ya ofisi za Kanda ya Nyasa, Mkoani Mbeya kwa kushambuliwa kwa makofi baadae akawa anatumia rungu kabla ya askari wengine kuja kujumuika na Kamishina Awadhi Haji
3.Kamishina Awadhi Haji aliacha Kumpiga Sugu baada ya Askari wengine wengi kuja kuja kumsaidia kumshambulia Sugu sehemu mbalimbali za mwili wake.
4.Kamishina Awadhi Haji alipoacha kumpiga Sugu alihamia katika kumpiga Katibu Mkuu John Mnyika, ambapo alikuwa Mnyika anavutwa kwa nguvu na askari wanamuita mheshimiwa
Kamishina Awadhi ndiyo alikuwa mtu wa kwanza pia kumpiga Katibu Mkuu Mnyika huku akiwafokoea askari wengine kuita Mnyika Mheshimiwa,
"Waheshimiwa wapi hawa, hawa ni wahuni tu, wanataka kuvuruga amani ya nchi. Wanachezea nchi."
5. Katibu Mkuu John Mnyika na Sugu walipandishwa katika Landcruiser hardtop Pickup kwa kuwalaza kifudifudi na juu askari zaidi ya 8 waliokuwa nyuma waliwakanyaga kuanzia Mbeya hadi Makambako
Njiani, Mnyika na Sugu walipokuwa wanajitahidi kutengeneza mazingira ya kuweza vichwa vyao vizuri waweze kupua walipigwa sana marungu ya miguuni na migongoni.
6. Katibu Mkuu Mnyika alishushwa Makambako, kisha Sugu aliendelea na safari akiwa amelazwa pale chini kifudifudi vilevile.
7.Muda wote wa safari, askari waliokuwa wanawasindikiza Mnyika na Sugu walikuwa wamevaa vinyago "mask"
8.Sugu alifikishwa Iringa Juzi majira ya Saa 9 :00 usiku na kuwekwa mahabusu ya pekee yake.
9.Jana majira ya Saa 9 : 00 Jioni walimchukua Sugu kutoka Mahabusu ya Kituo cha Polisi Central, Iringa kwenda Dar es Saalam wakiwa na gari ndogo.
10 Majira ya Saa 5 :00 usiku Polisi walimfikisha Sugu katika kituo cha Polisi Central, Dar es saalam, akiwa anaumwa kiasi cha wao kuogopa kumuweka Mahabusu wala kumpa neno lolote.
11.Polisi Central, Dar es saalam walioona hali mbaya ya sugu tangu ashushwe katika gari kutokea Iringa waligoma kumpa PF (Kibali cha kwenda kutibiwa) na Waligoma wao kumpeleka Hospitali, Walimuitia teksi wakailipa Tsh 7,000/= Dereva atafute sehemu ya kulaza wageni ampeleke Sugu.
12. Kwa sasa Sugu yupo katika Matibabu, baada ya kupata majeraha sehemu za Mgongoni, Mbavuni, Kichwani na Miguuni sehemu ya ugoko.
13.Mwisho, sugu na Mnyika wameibiwa simu zao zote pamoja na fedha kiasi cha Dollar elfu tano na shilingi milioni 3 za Kitanzania.
Boniface Jacob (Ex Mayor)
=====
UPDATES: 1830HRS
======
View attachment 3068821
JamiiForums, imezungumza na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema, anaelezea:
Taarifa za Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi (Sugu) pamoja na Katibu Mkuu John Mnyika ni kati ya walioumizwa wakati Polisi wanawakamata kwenye Ofisi zetu Mbeya, hatua ya sasa wameenda kwenye matibabu.
Bahati mbaya Jeshi la Polisi hapeleka kwenye matibabu hatalalamika maumivu makali, Mnyika akipelekwa nyumbani kwake Dar, Sugu pia aliletwa Dar licha ya kuwa nyumbani kwake ni Mbeya. Wote hawana simu kwa sasa.
Sugu alipelekwa Hospitalini ndio lakini kama bado yupo amelazwa au ametoka hizo taarifa sina kwa sasa hadi niende nikamuone sababu hana simu.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa
Hata uwe mkubwa kama nyumba, ukipigwa na watu zaid ya watano at once lazima ukaeduh na ubonge wote ule kapigwa hadi mahututi? kwa maana kumpeleka mtu over weight kama yule chini unahitaji equal and opposite amount of force au zaidi, kweli duniani kuna mambo …
PointCDM acheni kutafuta huruma kwa wasiokuwa na huruma!
Toeni maelekezo watu waangie mitaani.
Hawana risasi za kuangamiza watu wote!
Sugu akamshinde spika wa bunge la Tanzania ndoto ya mchana hii ,haiwezi na haitatokea Tanzania labda nchi nyingineHuenda ni maagizo ya supika maana Sugu ni threat 2025
Kwani bi sugua gaga alishinda?Sugu akamshinde spika wa bunge la Tanzania ndoto ya mchana hii ,haiwezi na haitatokea Tanzania labda nchi nyingine
Hii ndiyo 4Rs. Awadh lazima aukwae u IGP kwa jazi nzuri hii iliyotukuka.
Mungu angekuwa anahusika na siasa wasingepigwa virungu. Acha kumchosha Mungu na mambo yenu yasiyoeleweka.Mungu ibariki Chadema
Yupo mahututi hata life supporting machine hakuna Ina maana all vital organs zinafanya kazi kwa usahihiSugu nae aache mambo kama ya Suarez kwenye mpira, maana hata akiguswa kidogo tu, anajifanya kavunjwa mguu wote..!! Aache kutafuta public sympathy
Mwamba yuko fresh,mpaka anapost!!..
Mlitaka kufanya maandamano ya gen z mbeya,tanpol siyoHaya ndiyo maandalizi ya CCM kwa chaguzi zijazo, ngumi, mateke,mabomu ya machozi na risasi za moto.
Polisi tz siyo kenyan police, mlitaka kufanya maandamano ya gen z mbeya,mmeshukiwa kama mwewe,wanna msemo wao 'dola itakuangukia'Haya ndiyo maandalizi ya CCM kwa chaguzi zijazo, ngumi, mateke,mabomu ya machozi na risasi za moto.